Tanzania inaandaa magaidi bila kujijua. Sababu ni hizi.

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Asalamu aleikumu wanajamvi. Nimekuwa nafuatilia sababu za kuwepo kwa magaidi na majambazi ya kutisha katika baadhi ya mataifa hapa Africa na mabara mengine juu ya uwepo wa magaidi na majambazi ya kutisha. Niligundua kuwa Magaidi wanaandaliwa na nchi huska. Hizi ni sababu:

1. Kutoa mafunzo ya kijeshi kwa watu bila kuwaajiri. Tanzania ipo katika wakati mgumu sana maana ipo katika wakati wa kuaandaa magaidi na majambazi hatari sana katika nchi yetu maana inatoa mafunzo ya kijeshi bila kuwaajiri. Mfano kuna maafisa ambao wamepewa mafunzo ya kijeshi(precadate one) bila hata kupelekwa monduli kumalizia mafunzo yao ili wawe maafisa kamili. Hawa watu ni hatari sana kwa taifa maana wamechukizwa na serikali maana hata haiwapeleki kumalizia kozi yao. Ni hatari kwa Taifa.

2. Viongozi wapenda visasi. Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa serikali ya awamu ya Tano na hakika nimegundua inaendekeza visasi either kutokana na harakati za kupinga kisiasa au kuogopa kupata challenge kutoka kwa wapinzani wao wa kisiasa mfano ndani ya CCM. Hii ni hatari. Watu wanachoshwa na visasi na matokeo yake ni kuandaa magaidi na majambazi hatari kwa nchi yetu. Serikali lazima iliangalie hili. Ni hatari kwa nchi yetu.

3. Kuendekeza tabia ta kulindana kwa baadhi ya watumishi wa umma wanapofanya makosa ya jinai. Hili halina ubishi nadhani hata nyinyi mumeliona. Nchi yetu ni kisiwa cha amani. Lakini serikali yenyewe ndiyo itaiharibu amani ya nchi yetu. Mtumishi wa umma anapofanya kosa la jinai bila kuchukuliwa hatua za kisheria ibajenga chuki na hasira kwa wananchi na matokeo yake magaidi na majambazi hatari hutokea. Haya magaidi yanatumika kuua viongozi wanaolindwa na serikali kama wamefanya makosa. Naiomba serikali itimize wajibu wake. Nchi yetu inaeleka kubaya sana. Amani tunayojivunia kuna siku Moja tutaitafuta. Ni hatari kwa nchi yetu.

4. Kutengeneza kundi kubwa la watu wasio na ajira. Nchi yoyote hasa zenye historia ya kutengeneza magaidi zilitokana na kushindwa kutengeneza ajira kwa wananchu wake. Hali hii hupelekea kutengeneza taifa la watu wenye ujasiri. Taifa la waty wenye kujitoa muhanga either kwa kubeba mabomu au kuua viongozi ili tu waweze kulisha familia zao. Kadri siku zinavozidi kwenda mbele naona kabisa kuna Giza huko mbeleni. Serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka sana ili kudhibiti hali hiyo.

5. Kushindwa kutimiza mahitaji muhimu kwa majeshi yetu nchini. Nchi kupinduliwa inatokana pia na serikali kushindwa kuwapa mahitaji yote maaskari wa nchi yetu wakiwemo wanajeshi,askari magereza,askari polisi etc. Mpaka sasa kuna manung'uniko kila kona ya maaskari. Je manung'uniko haya yanaashiria nini kwa askari wetu juu ya nchi yao. Kwa kifupi naweza kusema kuwa nchi inaandaa majambazi na magaidi bila kujijua.

6. Kuminya Uhuru wa habari na Uhuru wa kutoa mawazo. Ikumbukwe ni haki kikatiba kila Raia kutoa maoni yake bila kupangiwa na MTU bila kuathiri sheria za nchi. Serikali inapoingilia uhuru wa habari na uhuru wa kutoa maoni huepeleka kutengeneza magaidi na majambazi maana watu wakizuiwa kuongea huonesha vutendo either kwa kuteka viongozi wa kiserikali au kuua viongozi. Serikali naiomba iangalie kwa jicho kubwa sana. Inaandaa majambazi na magaidi bila kujijua.

7. Kauli tata za viongozi zenye vitisho. Ni hatari sana kuwa na kiongozi anayetumia lugha Kali na yenye vitisho kwa wananchi wake maana ni njia bora kabisa ya kutengeneza majambazi na magaidi. Serikali waliangalie hili.

Mwisho:Mchawi wa Tanzania nia Tanzania yenyewe.

Hizi ndiyo sababu nilizokutana nazo katika harakati za kutengeneza magaidi na majambazi nchini. Naiomba serikali iliangalie kwa mapana sana swala hili vinginevo tutaiingiza nchi yetu katika hali ngumu sana.
Ndugu mwanajamvi una maoni gani juu ya hili? Ongezea.

NB: 1. Usi quote uzi.

Nawasilisha

Rais2020.
 
Very true yaani huku kuna askari wa wanyama pori wamehitimu lakini hadi sasa bado wapo mtaani hivi unategemea nini kwa watu kama hawa kuzidi kukaa mtaani bila ya ajira ebu serikali iangazie haya maswala kwani baada ya muda itakumbuka kufanya hivo wakati umechelewa sana
 
Very true yaani huku kuna askari wa wanyama pori wamehitimu lakini hadi sasa bado wapo mtaani hivi unategemea nini kwa watu kama hawa kuzidi kukaa mtaani bila ya ajira ebu serikali iangazie haya maswala kwani baada ya muda itakumbuka kufanya hivo wakati umechelewa sana
Mchawi wa Serikali ya awamu hii ni viongozi. Kupenda kiki badala ya kutatua changamoto za kijamii.
 
Nini ugaidi; hivi sasa unaweza hata ku-mobilize kikosi cha uasi na ukapata watu wa kutosha wenye uwezo wa angalau kufyatua risasi!!!
 
Magaidi tayari washatengenezwa wengi tu,mtakuja kujua wakianza matukio.kuna madogo kibao wametoroka shule na kuchukuliwa na makundi ya kigaidi kama alshabaab,wale wa pangani tanga nao wale sio magaidi?.
 
Nini ugaidi; hivi sasa unaweza hata ku-mobilize kikosi cha uasi na ukapata watu wa kutosha wenye uwezo wa angalau kufyatua risasi!!!
Nakubaliana na wewe. Mitaani kuna watu wengi sana ambao ni maaskari na wanautaalamu na silaha za moto. Hawa watu hawakutakiwa kuwa idle kiasi hicho. Muda ni Mwalimu mzuri sana
 
Magaidi tayari washatengenezwa wengi tu,mtakuja kujua wakianza matukio.kuna madogo kibao wametoroka shule na kuchukuliwa na makundi ya kigaidi kama alshabaab,wale wa pangani tanga nao wale sio magaidi?.
Serikali inatakiwa kuchukua hatua za dhalula kwa hili
 
Message to CCM na kibaraka wao Lipumba- tupo imara tutakilinda chama. Tupo imara tutazua kasheshe ikibidi.HAKI!
 
Back
Top Bottom