'Tanzania ina vilema vitatu' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Tanzania ina vilema vitatu'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 26, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WAKATI mwaka huu Tanzania inaadhimisha Jubilei ya miaka 50 tangu kupata uhuru wake, imeelezwa kuwa itaendelea kuwa nchi ya chini kimaendeleo
  ikilinganishwa na nchi nyingine duniani kutokana na watu wake kutopenda kufanya kazi na kuathiriwa na 'vilema vitatu'.

  Tahadhari hiyo imetolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, mkoani Kilimanjaro, Mhashamu Isaac Amani, wakati akitoa salamu zake za Pasaka katika ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kristu Mfalme, mjini Moshi, jana.

  Alivitaja vilema hivyo kuwa ni ulevi wa kupindukia, kuishi kinyumba na utandawazi.

  Alisema wengi wa Watanzania bado wako vijiweni, hawataki kufanya kazi na kwamba tabia hiyo imesababisha kidogo kinachopatikana kutokana na wachache wanaojituma, kitumiwe kwa taabu na watu wengi, wengi wao wakiwa ni wale wasiotaka kujituma.

  Askofu Amani alisema suala hilo na mambo mengine yamekuwa yakirudisha nyuma maendeleo ya nchi, na kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na ulevi wa kupindukia ambao alisema ni moja ya vilema vitatu ambavyo vimelikumba Taifa la Tanzania katika wakati huu linapoadhimisha miaka 50 ya Uhuru wake.

  “Kuna vilema vinavyopatikana kwa ajali, kuzaliwa na vingine vya kujitakia, hivi vya kujitakia ni pamoja na ulevi wa kupindukia, kuishi kinyumba na utandawazi, kwa kweli hivi vitatu vinaelekea kuipeleka nchi yetu pabaya,” alisema.

  Alisema ulevi wa kupindukia umewamaliza na unaendelea kuwamaliza watu wengi haswa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa ambapo alisema kuna baadhi ya viongozi na wananchi ambao si waaminifu na ambao wamekuwa wakiyaona haya na kuyafungia macho.

  “Pombe hizi zinauzwa katika maeneo tunayokaa, baadhi ya viongozi wanayajua haya na kuyaona lakini wanayafumbia macho hii imesababisha watu wengi kutokufanya kazi kutokana na nguvu kazi ya Taifa kumalizwa na ulevi wa gongo tena katika kipindi hiki ambapo Taifa linaadhimisha Jubilei muhimu ya Uhuru wake,” alisema.

  Kuhusu kuishi kinyumba, askofu huyo alisema kuwa tabia hiyo imekithiri miongoni mwa wakristu wengi na kwamba umepora haki na uhalali wa ndoa kama alivyoelekeza Mwenyezi Mungu, ambapo alisema kitendo hicho kimekuwa mfano mbaya katika maisha ya kila siku, kiasi cha hata watoto na vijana kuona ya kuwa ni jambo la kawaida katika maisha.

  Aidha Askofu Amani alisema utandawazi ni kilema kingine ambacho kinaiweka nchi mahali pabaya na kwamba tayari umeshaanza kuwadhuru Watanzania wengi wakiwemo watoto wadogo.

  “Mfano mzuri ni matumizi ya simu za mkononi ambazo kwa sasa zinatumika vibaya, ambapo watu wanazitumia kwa kutumiana ujumbe wa matusi, vitisho, uchochezi, kupanga ujambazi na mambo ya fitina, hivyo kupoteza maana halisi ya matumizi ya vyombo hivi muhimu ambayo vililengwa kurahisisha mawasiliano,” alisema.

  Aliagiza ya kuwa wakati Taifa likiendelea kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wake kuwe kunafanyika sala maalumu ya kuliombea taifa kila siku kila baada ya ibada, katika Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristu na mashirika yote
  ya kikatoliki jimboni humo hadi kilele cha sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, zinazotarajiwa kufanyika Desemba, mwaka huu.

  Ujasiri wa kukemea maovu

  Waumini wa Kanisa Katoliki na Watanzania kwa ujumla wametakiwa kuiombea nchi ili ipate watu wenye ujasiri wa kukemea maovu nchini, ukiwemo ufisadi, kwa kuwa watu wengi wameshindwa kusimamia haki kutokana na kufungwa midomo yao kwa kununuliwa.

  Kutokana na baadhi ya watu kushindwa kusimamia haki kumewafanya kushindwa kutofautisha dhambi na isiyo dhambi hatua inayokwamisha hata kumwogopa Mungu.

  Alikwenda mbali zaidi na kuwakumbusha waumini utendaji kazi wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage, ambapo alisema kuwa kutokana na kuwa na moyo wa kuwatumikia kwa dhati Watanzania ilifika mahali hata akaisahau familia yake na ikabaki ya kawaida sana ambayo haina tofauti na familia za wananchi wa kawaida.

  "Baba wa Taifa ilifika mahali akawashangaa hata wanaogombania kwenda Ikulu, alihoji sana na ndio maana familia yake ni ya kawaida tofauti na watoto wa viongozi wa siku hizi ambao wana fedha kibao na sijui wanazitoa wapi, hivyo kama waumini tunatakiwa kuiombea nchi yetu amani," alisema.

  Hayo yalisemwa Dar es Salaam kwenye mkesha wa pasaka na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kitunda, Padri Maximilian Wambura wakati akitoa mahubiri katika ibada hiyo.

  "Katika kipindi hiki tuna kila haja ya kuliombea taifa letu amani...viongozi wetu wanatakiwa kuombewa sana kwa kuwa hata magamba wanayodai kujivua hakuna kitu chochote, imefika mahali watu wameshindwa hata kutofautisha dhambi na neema kwa kuwa muda wote wako ndani ya dhambi na wengine wameshindwa kusimamia ukweli kutokana na midomo yao kufungwa na plasta," alisema Paroko Wambura.

  Ibada hiyo ya pasaka pia ilikuwa na matukio mbalimbali yakiwemo ya baadhi ya waumini kuokea sakaramenti za ndoa, ubatizo na kipaimara ambao nao aliwataka kudumu katika imani yao na kuachana na tabia ya kuhama hama makanisa kwa kuwa kufanya hivyo ni kukwepa kubeba misalaba yao.

  Alisema kuwa ukwepaji wa kila mmoja kubeba msalaba wake umewafanya baadhi ya wananchi kudanganyika kutokana na matatizo yanayowakabili yakiwemo maradhi, kufarakana kwa ndoa, tamaa ya mali yanayofanya kujikuta wakihangaika na kubadili makanisa kwa kukimbilia mengine ambayo yameanzishwa kwa tamaa za kifedha.

  "Kuna wimbi la watu kuhama hama makanisa lakini wengi ukiwachunguza utabaini wamekata tamaa, wapo wanaotaka watajirike kwa kuombewa, wapo wanaokwenda kwa kusumbuliwa na maradhi lakini Mungu wetu anasema kama unaumwa nenda hospitali na ndio maana kawaweka madaktari na kama unahitaji mali unatakiwa ufanye kazi sana...pamoja na kuwepo kwa watu ambao wamepewa nguvu za kiroho lakini kama muumini unatakiwa kuubeba msalaba wako," alisema.

  Akiwaasa wanandoa aliwataka kuwa wavumilivu na kutokuwa na makuu kwa wenza wao kwa kuwa siri ya ndoa ni uvumilivu.

  "Ndoa nyingi zinasambaratika kwa kuwa wengi wanataka makuu, wanataka kulipiza visasi kwa wenzao wao na matokeo yake huwa ni mabaya zaidi, hivyo kama ndani ya ndoa mmetofautiana mnatakiwa kuwaona hata wazazi na mkishindwa zipo taratibu hata za kumwona padri ili awasaidie kumaliza tatizo lenu," alisema.
   
 2. D

  Diva Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 28, 2006
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nakubaliana na hivi vilema vitatu kweli tunavyo hapa Tanzania. Pia nahisi vinahusiana na jambo linalofanana. Nalo ni kuporomoka kwa uchumi. Nasema hivi kwa sababu kadhaa. Nitahusianisha chache hapa:
  1. Kuongezeka kwa "Kukaa kinyumba" kunatokana na wanaume wengi kuwa na uchumi dhaifu. Kwa vile wanaume ni chanzo cha kipato, kwa jamii zenye mfumo dume kama wetu, basi hujikuta wakikosa ushujaa wa kuanzisha familia thabiti na kuacha iende hivyo hivyo tu bila kuwajibika. Hili pia linahusiana na utandawazi kuongeza mahitaji ya msingi ya maisha, kwa mfano chakula, mavazi na malazi sasa sio mahitaji ya msingi pekee. Kuna usafiri, mawasiliano. Hata makazi sasa yanamaanisha TV, Radio, Friji, Decoder nk. Simu ya mkononi cjui itaingia wapi ktk mahitaji ya msingi ya binadamu. Mahitaji yameongezeka kutokana na utandawazi lkn kipato hakijaongezeka sambamba!

  2. Ulevi wa kupindukia pia wana saikolojia watanirekebisha lkn nimeshawahi kusoma mahali pia kuwa unatokana na kuvurugikiwa mawazo kwa sababu ya uchumi mbovu. Hili hasa huwatokea wanaume kama njia ya kujiliwaza. Vinginevyo kama uchumi ungekuwa thabiti, wangekaa wakala vzr na familia zao, au wakaenda beach kupunga upepo nk. Lkn kwa hali ilivyo, hata usingizi watu hawapati kwa kuwaza na kuwazua. Wale wenye ajira au biashara pia hawashawishi waliopo kijiweni kutamani maisha yao, kwa vile nao pia uchumi wao dhaifu, labda waibe huko maofisini! Kwa hio walipo kijiweni hawajaona sababu ya kutoka huko kwa vile hata hao waliotoka hali ni ileile kama yao. Working poors wanaongezeka!

  3. Kutothamini kazi: huwezi kuithamini kazi isiyokuthamini, yaani isiyokulinda, isiyo na matumaini. Jana kama leo watanzania ndio wanayoyapata sasa.

  4. Utandawazi: watanzania tumevamiwa na utandawazi. Sisi hatujapeleka fursa za kutosha huko kwenye utandawazi. Tumekuwa wapokezi tu. Basi tulindwe na mifumo imara ili nasi tujenge misingi ya kupeleka vyetu huko utandawazini. Si kweli kwamba wazungu hawalindi watu wao dhidi ya utandawazi!! Watanzania wengi hadi leo hajafahamu dunia inaendaje. Sasa kuwabebesha zigo la utandawazi si kuwatafutia dhahama tu jamani? Wanaofaidika ndio wanaowanyonya wengi. Mfumo wa kuwalinda ni dhaifu kabisa kama upo.

  Kwa hio mwisho wa siku la kuhusisha vyote hivi ni UCHUMI uliodhoofishwa na ulafi wa viongozi wa nchi hii. Uchumi usiolinda maslahi wa watu wake isipokuwa unaochukua kodi kibao na kuwastarehesha wachache wanaojiita viongozi, pamoja na familia zao. Leo hii ukitaka kuwa mfanyabiashara huku umesimamia imani yako kwa Mungu basi ujue utapata shida sana Tanzania kufanya biashara. Watawala wala rushwa watakuandama, wezi watakuandama, kuuziwa bidhaa feki itakupata, fitina, uchawi... mwisho na wewe unajifunza kuchakachua mizani ya sukari!

  Nashauri viongozi wa dini wasimamie mabadiliko na mapinduzi ya kweli ili mtanzania apate heshima yake. Kusali peke yake hakusaidii. Vinginevyo tutaona migogoro ya kati ya dini na ndani ya dini. Makanisa na misikiti vitazaliwa na kumegeka kila cku, lkn suala la ndani kabisa ni NJAA inayowakabili watz, tena wengi wao bila kujali wamesoma, wameajiriwa au wafanyabiashara.

  Tunahitaji UHURU na MAPINDUZI Part 2 inayohusisha kujitwalia uchumi wetu kwa wengi kama ilivyo kwenye KURA wengi ndio hushinda na uchumi uwe hivyo hivyo.

  Mungu ibariki AFrika, Mungu ibariki Tanzania
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  bado kutegemea nguvu za giza hasa lamli na vikombe wewe viongozi wanashinda kwa shekhe yahaya unategemea tutabadilika kweli
   
Loading...