MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 850
Kwani ni lazima wa kwetu wawe sawa na wa huko?
Watanzania wengi ni malimbikeni tu. Lakini sio kosa lao, wanapata umaarufu ghafla mno kiasi kwamba wanashindwa kuumudu. Nchi zilizoendelea wanaadaliwa kisaikolojia kwanza kabla. Mfano kabla ya kuingia NBA unafundishwa mambo mengi ukiwa college ikiwemo Financial Literacy and Management. Lakini pia kuna watu maarufu wa USA na wameanguka kiuchumi kama Mike Tyson. Alifika mahali akawa anapigana ili tu apate pesa za kuendelea kuishi!
Umesema wakwetu wanapata umaarufu ghafla kwani wenzetu hakuna wanaopata umaarufu ghafla? Wapo wengi tu na huko wanaopata umaarufu ghafla.
Umesema nchi walizo endelea wanaandaliwa kisaikolojia kwanza unamaanisha maisha kiujumla au kupata umaarufu tu? Maan umetoa mfano wa chuo sijui NBA wakati si kweli kuwa kila celebrity wa marekani au ulaya wamepitia chuo na mifano ipo mingi tu tena kuna wengine hata kumaliza high school hawaku maliza.
Otherwise mkuu nakubaliana na kila kitu kingine ulicho sema. Tanzania malimbukeni wengi. Pesa kidogo tu mtu anaanza kumwaga hela kila sehemu aonekane ana uwezi kuliko hata alio nao mwishoni ni kufilisika tu. Ni wachache sana wanaoona mbele na ni wachache sana wanaokua wajasiriamali. umetoa mfano mzuri sana wa bwana Kipanya.
Kwani ni lazima wa kwetu wawe sawa na wa huko?
kama silazima wawe sawa na wa kule Ulimwengu wa kwanza, sasa inakuwaje wanajipachika majina kama hilo macelebrite ,wakati hawana viwango hivyo.
Post murua kabisa bro, kuna time huwa najiuliza huw najiuliza hivi inakuwaje kuna thread hazina logic kabisa kama hii.wanajipachika majina kama yapi ambayo yanakukera mkuu??
as far as i am concerned tuna utofauti mkubwa sana na wamarekani(na dunia ya kwanza in general) kwenye kila kitu,KILA KITU..kila mahali kuna viwango vyake katika nyanja zote..kuna celebrity wa bongo na celebrity wa marekani mkuu!sivyo hata Dar halina hadhi ya kuitwa jiji basi sababu kuna NYC,London,Paris nk ambayo nayo ni majiji lakini kwa utofauti mkubwa mno na letu...najua unanielewa!
najaribu kusema kwamba,kwa viwango vyetu wao ni celebrities...
ni mtazamo tu!