Tanzania imekuwa Wild West?

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Nimekuwa nikisoma habari mara kwa mara kwa wamiliki wa bastola kuzitoa na kutishia watu hadharani pale wanapoona wanabughudhiwa. Kikomo cha hali hiyo kilitokea pale marehemu Ditopile alipotoa bastola yake na kumpiga risasi dereva wa daladala aliyemgonga. Kumekuwa na vituko vingine kama vile njemba kutoa bastola akiwa disco na kupiga hewani kwa vile alikuwa hamuoni msichana wake. Njemba mwingine, (au ni huyohuyo?) alimtolea bastola kumtishia msichana aliyekuwa anataka kumnyima penzi! Sasa juzi nimesoma kuwa njema mmoja mwiigizaji wa filamu aliwatishia watu kwa bastola waliomtaka aondoe gari lake ambalo liliziba njia. Nauliza hivi: Je Tanzania siku hizi imekuwa wild west ambapo kila ugomvi unaamliwa kwa bastola? Ni vigezo vipi vinavyotumika kuwapa watu silaha? Kwa wale tuliopitia jeshini na wenye uzoefu wa silaha za moto, silaha hizo zinatakiwa zitumike kwa uangalifu mkubwa sana, ama sivyo unaweza kumuua/kumuumiza mtu, au hata wewe mwenyewe. Kwa wale tuliopitia mafunzo ya silaha, tunasisitiziwa kwamba, usimnyooshee mtu bunduki/bastola, kama hauko tayari au huna uhakika kuwa utafyatua risasi. Hivyo kitendo cha kumuelekezea mtu silaha kitokee kama njia zingine zimeshindikana, au maisha yako yapo hatarini. Sasa itabidi hata wale wenye mapanga, marungu, bakora waanze kutembea nazo ili wasikerwe kerwe na binadamu wenzao. Mwenzako akikuambia nipishe nipite...mara anaona tungu kama la Kipepe mbele ya pua yake!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom