Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 433
Wataalamu wa fasihi najua sitakua mgeni kwenu mimi bawabu wa pili niliekuwa nasimama geti la ua wa ndani wa Bi kilembwe.
Sasa hivi Tanzania kiongozi huruhusiwi kuziona changamoto za wananchi kama Bi. Kilembwe hajaziona, wananchi wanaweza wakawa wanakufa mbele yako lakini kama Bi. Kilembwe hajaona na wewe unatakiwa usione. Ukiona kabla yake kuona huna chako tena, wanazengo wanasema you are in ''bad shape''
Kwani mmesahau majuzi bungeni Rais Samia alivyoonyesha kutambua kuwa kuna watu walifariki siku ya maandamano, si mliona wabunge walivyopiga makofi kana kwamba wao sio watanzania na wala hawakuwa Tanzania namna ambavyo walikuwa wametulia?
Katika utawala wa Giningi ya Bi. Kilembwe huruhusiwi kusema mpaka uambiwe sema, na hata baada ya kuambiwa sema husemi tu vile wewe unataka bali utaambiwa kipi useme. Wanazengo wanasema wanakumezesha maneno na baadae kukuamlisha uyateme.
Katika utawala wa Bi. Kilembwe rangi hamzitambui vile ninyi mnataka bali vile yeye anavyotaka. Yeye nyeusi akiiona nyeupe na nyinyi mnatakiwa kuiona hivyo hivyo kama yeye alivyoiona.
Lakini jamaa mmoja anaitwa Mtolewa, sijajua atakuja lini ila huyo atakapokuja ndie atakaekuja kufanya mapinduzi ya kweli.