Tanzania ikishindwa kuingia AFCON 2019 basi ni baada ya miaka 100 tena

Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,327
1,684
Katika dokezo lililotolewa juzi la makundi ya timu kuwania kushiriki AFcon 2019 Tanzania ina fursa ya kuingia. Je watanzania tufanye yapi ili timu yetu nayo iweze kushiriki na ikiwezekana ichukue kombe AFCON 2019?
 
Ligi yenu mbovu

Juzi nilikuwa natizama game ya simba vs yanga ,mpira ulikuwa mbovu ,butua butua hamna ladha

Tanzania bado sana labda miaka 50 ijayo kizazi kijacho kikijielewa ..

Uganda ya akina okwi nimewatizama Qualifier za afcon majamaa wanajuwa na ndio maana wameingia Afcon..okwi anakula mkeka Uganda lakini Tz anaonekana fundi sana

Cape Verde wamempiga ureno magoli 2 wamebadilika sana na wachezaji wao wanacheza nje saizi

Kwa game ya juzi ya yanga&Simba haki ya Mungu hatutoboi ,naweza kuweka dau kabisa

NB:Taifa stars hujengwa na yanga&Simba .
 
Wanasema watanzania wamedumaa njoomana qualifiers zote inakua nguma kupita kwasbabu inakutana na miamba iliyokula na ikashiba.
 
Kiwango chetu bado kibovu, hakuna ile hali ya kuwa na uhakika wa ushindi.....kila game ni mawazo tuuuuu
 
mimi mwenyewe nilishangaaa okwi anakaa benchi uganda.. anaingia mtu akiumia au wakichoka ila bongo eti ndio fundiiiiii...

tanzania bado sana... hatuwez cheza afcon kwa wachezaj wa simba, yanga na azam... samatta peke yake hatoshi.. tujae jae ulaya na timu kubwa africa kwanza
 
Back
Top Bottom