Tanzania iige mfano wa Botswana

Tanzania iige mfano wa Botswana

Kwanza uelewe kwamba mimi si muajiriwa wa taasisi yoyote Tanzania.

Pili inaonesha upeo wako ni mdogo sana kwenye hesabu za kibiashara. Ikiwa ushuru wa Kitenge ni 50% + VAT @18%. Kama sheria za ushuru ungekuwa unafatwa hasa, kitenge kilitakiwa kilipwe si chini ya 250 milioni kwa container ya 40 ft badala yake inalipiwa 70 milioni.

Makadirio ya kodi ya mapato ya wafanya biashara wingi Kariakoo ya mwaka 2016-17 wameambiwa ni mil 3 kutoka 750,000 kwa mwaka waliyozowea, wote wanapiga kelele. Hii ni sawa na kusema mfanya biashara hapati net profit ya 1,500,000 kwa mwezi? Lakini mfanya biashara huyo huyo anao uwezo wa kulipa pango 2,000,000 kwa mwezi.

Tatizo kubwa katika ukusanyaji wa kodi ni kuwa 50% ya kodi haikusanywi kwa sababu ya kukosa ubunifu wa mbinu za kukusanya hiyo kodi. Kwa hiyo wanaemkamata na ngozi ndiye hummalizia machungu yao. Ingekuwa kodi inakusanywa kama inavyotakiwa basi ungekuwepo uwezo wa kuipunguza na mapato bado yangepanda!

Kwanini kodi isikusanywe inavotakiwa Na iko kwenye sheria au hii Nchi inaendeshwa bila sheria? Mashine zilizosambazwa madukani zinakatwa kodi Asilimia ngapi? Huu Ndio utaratibu mbovu wa kuwabahatishia wateja kodi zilizokuwa haziko wazi. Mnalipisha kodi kwa kumuangalia mtu?
 
Botswana wana Gold mining ipo mupane 30km toka Fransistown...wana Copper,Nikel,Coal na Almasi ambayo De beers wanachimba wanagawana 50/50 kila kinachochimbwa..
 
Tanzania inahitaji fikra ya Libertarianism.

Kwenye Kiswahili hamna neon linalo tafsiri kuwa Libertarianism. Kwa ambao hamuelewi, Libertarianism ni philosophia inayo sisitiza umuhimu wa uhuru. Mtu ambaye ni Libertarian, jitihada zake ziko kwenye kuongeza uhuru wa wananchi kuchagua jinsi wanavyotaka kuishi, kuwapa wananchi uhuru wa kufanya siasa jinsi wanavyotaka, kuhakikisha kuna uhuru wa kuweza kuchagua kama unataka kujihusisha na watu au biashara au serikali, na ubinafsishaji.

Libertarianism (Latin: liber, "free") is a political philosophy that upholds liberty as its principal objective. Libertarians seek to maximize autonomy and freedom of choice, emphasizing political freedom, voluntary association, and the primacy of individual judgment.

Ukiangalia nchi zote duniani, au ukiangalia hata Africa, nchi iliyo endelea kuliko zote ina wapa wananchi uhuru mkubwa sana na serikali yake ni ndogo. Inalinda haki za kumiliki mali kwa wananchi wenyeji na haki za kumiliki mali kwa wawekezaji wa nje ya nchi. Ina kusanya kodi ndogo na HAPANA sheria za kunyanyasa wafanya biashara. Kuna uhuru wa kufanya biashara na uhuru wa kuwekeza.

Ukiangalia Tanzania, wawekezaji wa nje hawana haki za kumiliki mali ambayo wao wenyewe wameilipia. HAPANA uhuru wa kuwekeza au kuanzisha biashara. TUNA WIZARA 22. Hii ni hali mbaya kwasababu wizara hizi zote zinatumia hela ya wananchi na zinavyokuwa zina sababisha KODI kuongezeka. Alafa hizi wizara zote zinakusanya kodi zao zenyewe kwenye sekta ya biashara. Umaskini Tanzania unatisha lakini bado serikali inataka kuongeza kodi.

Kama tusipo fwata fikra ya Libertarianism hatuta fika kwenye maendeleo.

Kichwa cha Habari chako na maudhui yako ni vitu viwili tofauti, nilitegema maudhui yako yesheheni jinsi gani nchi ya Botswana ilivyofanikiwa na kwamba ni kipo tunapaswa tuige badala yake umeishia tu kutoa maana ya Misamiati migumu, sasa kwa nini usingeweka kichwa chako cha Habari kwamba ulitaka kutufundisha maana ya hiyo unayooita sijui libertariasm?
 
kessy upo vizuri katika Political Economy ilo somo lilishafutwa muda ndio maana wengi hawakuelewi...ila Botwana ulichoongea ndio wanachofata Raia kodi sio mzigo na wanalipa kweli na hasa pale unapokua mfanyabiashara mkubwa...
 
Kichwa cha habari kinasema Tanzania iige mfano wa Botswana. Unafungua post kuangalia huo mfano wa Botswana, hukutani hata na sentensi moja yenye neno Botswana. Hii ndiyo reflection ya aina ya elimu tunayoipata au ni sisi wenyewe tunajitoa ufahamu deliberately?
Hao ndio watoto wahanga wa kansa ya kijamaa waliochafuliwa na mfumo ccm. Huwa kwao kila kitu wanataka waitwe leaders, kwa vile kwao kila kitu ni cha maonyesho tuu.

Huyu ukimuuliza km hayo anayoyasema yanaweza hata sikilizwa na CCM? Kabla hajaja makamba au Jk , sijui atawaambia tayari ipo na wananchi wapo ktk huo mfumo long time.

Huyu dogo haoni shida kwa alichoandika, na wala hajui nani anaambia afuate huo mfumo. Kwa vile watz ni too general kuweza fanya kitu chochote serious.
 
kessy upo vizuri katika Political Economy ilo somo lilishafutwa muda ndio maana wengi hawakuelewi...ila Botwana ulichoongea ndio wanachofata Raia kodi sio mzigo na wanalipa kweli na hasa pale unapokua mfanyabiashara mkubwa...
Hivi wewe kweli upo serious, hiki ulichokiandika ndio kinathibitisha hiyo unayoiita kweli?Kodi kutokuwa mzigo kwako ndio,uthibitisho wa kweli yako. Hivi waathirika wa mfumo ccm km waliojaa humu uwape uhuru huku hawawezi timiza wajibu, wala kufirikiri wenyewe si disaster? pengine angeshauri kwanza namna ya kufuta madhara ya CCM, kidogo mngeonyesha jitambua na kutambua mazingira..
 
Dhahabu= zahabu
Zahabu ni mojawapo ya maneno yaliyobadilishwa majina sana ktk nchi tofauti, zilizokopa mashariki ya kati. Ni km neno Mohamed, kuna wanaoita mehmet, mamadou, moahamedi, etc. Michael, Mike, mikel, etc. Kwa hiyo si eneo zuri sana la kujenga ubishi. labda kwa wabongo wa L na R, wanaposema haya maneno km vile ni sawa Light=Right, Lice=Rice, kula=Kura and the sort.
 
Hivi wewe kweli upo serious, hiki ulichokiandika ndio kinathibitisha hiyo unayoiita kweli?Kodi kutokuwa mzigo kwako ndio,uthibitisho wa kweli yako. Hivi waathirika wa mfumo ccm km waliojaa humu uwape uhuru huku hawawezi timiza wajibu, wala kufirikiri wenyewe si disaster? pengine angeshauri kwanza namna ya kufuta madhara ya CCM, kidogo mngeonyesha jitambua na kutambua mazingira..
Mkuu ivyo vitu alivyoongea mtoa vipo sio vipo katika makaratasi nenda Botswana hapo au South Africa uone kodi inavyokusanywa...huku makampuni makubwa ndio yanapata msamaha wengi wa kati na wa chini ndio wanalipa sana kodi au unadhani tunaongea vitu ambavyo havipo....
 
Tatizo langu sio kuwa kweli au uongo,ila umetumia ktk wrong place kuthibitisha kitu kingine kuwa ni kweli.
 
Hao ndio watoto wahanga wa kansa ya kijamaa waliochafuliwa na mfumo ccm. Huwa kwao kila kitu wanataka waitwe leaders, kwa vile kwao kila kitu ni cha maonyesho tuu.

Huyu ukimuuliza km hayo anayoyasema yanaweza hata sikilizwa na CCM? Kabla hajaja makamba au Jk , sijui atawaambia tayari ipo na wananchi wapo ktk huo mfumo long time.

Huyu dogo haoni shida kwa alichoandika, na wala hajui nani anaambia afuate huo mfumo. Kwa vile watz ni too general kuweza fanya kitu chochote serious.

Nafikiri hauelewi kwamba Libertarianism siyo ujamaa. Ujamaa unahitaji nguvu za serikali kuzuia uhuru wa watu na kunyang'anya mali kwa waliozifanyia kazi na kuwapa wasio fanya kazi. Libertarianism ni uhuru wa watu kufanya na mali zao jinsi wanavyotaka.
Mimi sikubaliani na CCM hata wangenilazimisha kwa bunduki. CCM na ujamaa ndiyo chanzo cha umaskini na fikra za kijinga Tanzania.
 
Sidhani km nimesema ni sawa na ujamaa.
 
Hii mada ni nzuri zaidi kuwahi kuiona humu JF,ushauri ulioutoa ni mujarabu kabisa.Hata mimi kilio changu siku zote kimekuwa ni juu ya uwepo wa serikali ndogo itakayosaidia kupunguza matumizi makubwa; uwepo wa kodi affordable itakazozifanya bidhaa na huduma kuwa za gharama nafuu sana, kodi ambazo zitavutia wawekezaji wakubwa kwa wadogo kwa wingi kutoka ndani na nje ya nchi, kodi ambayo itaongeza ukubwa wa purchasing power (customer/consumer base);halafu ndio tunakuja kwenye uhuru wa kuchagua (free market) sasa ambayo inaweza kuwa impetus ya innovation and creativity kwa wazalishaji wetu wa ndani. Tunapokuwa na soko huru (free market) linalompa Mtanzania uhuru wa kuchagua bidhaa anayotaka kununua tunatengeneza competitive environment ya kibiashara itakayomlazimisha local producer kubadilika kuendana na mazingira ya kibiashara yalivyo, ndiyo innovation na creativity yenyewe hiyo.So nimeipenda sana hoja yako.

Wenye hoja zao bana! hawana mbwembwe!.... hongera mkuu vile umeelewa hoja ya msingi na kuchangia, looks like huna makuu hata kwenye maisha yako yakawaida...... kuliko wale Mazuzu badala ya kuchangia mada kwa hoja inayoeleweka na kuendana na Mada, ataanza kuzungumzia nukta iliyokaa bahati mbaya mwanzo sababu ya typing error! kumbe hawana point, wanakua kama wahaya!
 
Back
Top Bottom