Tanzania iige mfano wa Botswana

Kessy Wa Kilimanjaro

JF-Expert Member
Jan 23, 2016
327
208
Tanzania inahitaji fikra ya Libertarianism.

Kwenye Kiswahili hamna neon linalo tafsiri kuwa Libertarianism. Kwa ambao hamuelewi, Libertarianism ni philosophia inayo sisitiza umuhimu wa uhuru. Mtu ambaye ni Libertarian, jitihada zake ziko kwenye kuongeza uhuru wa wananchi kuchagua jinsi wanavyotaka kuishi, kuwapa wananchi uhuru wa kufanya siasa jinsi wanavyotaka, kuhakikisha kuna uhuru wa kuweza kuchagua kama unataka kujihusisha na watu au biashara au serikali, na ubinafsishaji.

Libertarianism (Latin: liber, "free") is a political philosophy that upholds liberty as its principal objective. Libertarians seek to maximize autonomy and freedom of choice, emphasizing political freedom, voluntary association, and the primacy of individual judgment.

Ukiangalia nchi zote duniani, au ukiangalia hata Africa, nchi iliyo endelea kuliko zote ina wapa wananchi uhuru mkubwa sana na serikali yake ni ndogo. Inalinda haki za kumiliki mali kwa wananchi wenyeji na haki za kumiliki mali kwa wawekezaji wa nje ya nchi. Ina kusanya kodi ndogo na HAPANA sheria za kunyanyasa wafanya biashara. Kuna uhuru wa kufanya biashara na uhuru wa kuwekeza.

Ukiangalia Tanzania, wawekezaji wa nje hawana haki za kumiliki mali ambayo wao wenyewe wameilipia. HAPANA uhuru wa kuwekeza au kuanzisha biashara. TUNA WIZARA 22. Hii ni hali mbaya kwasababu wizara hizi zote zinatumia hela ya wananchi na zinavyokuwa zina sababisha KODI kuongezeka. Alafa hizi wizara zote zinakusanya kodi zao zenyewe kwenye sekta ya biashara. Umaskini Tanzania unatisha lakini bado serikali inataka kuongeza kodi.

Kama tusipo fwata fikra ya Libertarianism hatuta fika kwenye maendeleo.
 
Kichwa cha habari kinasema Tanzania iige mfano wa Botswana. Unafungua post kuangalia huo mfano wa Botswana, hukutani hata na sentensi moja yenye neno Botswana. Hii ndiyo reflection ya aina ya elimu tunayoipata au ni sisi wenyewe tunajitoa ufahamu deliberately?
 
Kuna sehemu umeandika serikali inakusanya kodi ndogo ( kidogo).........hizo nchi zinaendeleaje bila kodi?
 
Hii mada ni nzuri zaidi kuwahi kuiona humu JF,ushauri ulioutoa ni mujarabu kabisa.Hata mimi kilio changu siku zote kimekuwa ni juu ya uwepo wa serikali ndogo itakayosaidia kupunguza matumizi makubwa; uwepo wa kodi affordable itakazozifanya bidhaa na huduma kuwa za gharama nafuu sana, kodi ambazo zitavutia wawekezaji wakubwa kwa wadogo kwa wingi kutoka ndani na nje ya nchi, kodi ambayo itaongeza ukubwa wa purchasing power (customer/consumer base);halafu ndio tunakuja kwenye uhuru wa kuchagua (free market) sasa ambayo inaweza kuwa impetus ya innovation and creativity kwa wazalishaji wetu wa ndani. Tunapokuwa na soko huru (free market) linalompa Mtanzania uhuru wa kuchagua bidhaa anayotaka kununua tunatengeneza competitive environment ya kibiashara itakayomlazimisha local producer kubadilika kuendana na mazingira ya kibiashara yalivyo, ndiyo innovation na creativity yenyewe hiyo.So nimeipenda sana hoja yako.

Mimi sikubaliani na wewe kwa Tanzania kufata mfumo huo:

1. Serikali ndogo: Hao wasomi na vijana walohitimu masomo watafanya kazi gani?. Ajira kutoka serikalini ndio njia moja kubwa ya wealth distribution Tanzania. Na ukubwa unaouona wa serikali yetu lakini bado kazi hazifanywi, jee itakuwaje kukiwa na wafanyakazi kidogo? Ziko sehemu za kubana matumizi lakini si kupunguza waajiriwa serikalini. Tatizo kubwa ni kuwa hela wanakula wachache kwa kupeana upendeleo wa ajira na tenda na sio kugawia kampuni tofauti tofauti.

2. Kodi ndogo: Tanzania kodi ni kubwa kwenye karatasi (averaging 25%) na VAT on import ya 18% na kesi chache excise duty (0-50%). Lakini ki uhalisia kodi inayolipwa haizidi 5%. Kwa sababu karibu bidhaa zote zinazoingizwa nchini zimekuwa under-valued ikiwa na maana thamani yake inayotumiwa kutolezwa kodi ni chini sana in most case 15% ya actual value. Kwa maana hiyo 25% ya import duty inageuka inakuwa 3.75%. Sasa Serikali ikiweka 5% itageuka kuwa 0.75% hatima yake.

3. Uhuru wa kununuwa na kuuza bidhaa: Mpaka sasa Tanzania hakuna control ya kutosha (narudi kwenye waajiriwa kidogo) inayosababishwa na wataalamu haba ama waajiriwa wachache wa kulinda maslahi na afya ya mlaji. Tukiachiwa kuuza na kununuwa tunachotaka, tutauziana mavi ya panya kama ni dawa na chakula. Mimi (nakubaliana na wewe) siamini kwamba kuzuwia bidhaa kuagizwa nje kutainua uchumi wetu, kitakachotokea ni kujaza mifuko ya wachache kwa sababu Tanzania ni kubwa na inategemewa na mpaka majirani zetu kwa bidhaa. Ukiunganisha na uhaba wa teknolojia na umeme wa kuaminika bila kusahau wizi, bidhaa lazima zitakuwa bei ya juu na adimu.

Tanzania tuna nafasi nyingi tu za kuinua uchumi wetu, tusilazimishe mbinu ambazo kwa kwetu haziwezi kufanya kazi. Hatuwezi kuwa nchi ya viwanda kwa sababu ya uhaba wa advanced technology ambayo inapunguza gharama za uazlishaji bila ya kusahau umeme wa uhakika ikiwemo miundo mbinu ya huo umeme. Kuwa na gesi hai guarantee uhakika wa umeme ikiwa miundo mbinu ni mibovu. Kilimo na mazao ya ufugaji kwetu sisi ndio best option kama tutaamua kuwa makini nayo. Kama hatuwezi kushindana kwenye soko la saruji nje kwa nini tusiuze kokoto na mchanga (kigezo cha mazingira kufatwa). Kama sukari yetu ina bei kubwa soko la nje kwa nini tusiuze na kuagiza ya rahisi tukatumia? Kama tuna graduates wengi hawana kazi kwa nini Serikali isiingie mkataba na nchi kama Dubai wakaenda kufanya kazi kwa miaka 2-5 wakatoka kimaisha na kupata experience. Kwa nini serikali isishushe rates za kodi (kushawishi EAC partners) ili zionekane zina mvuto kwa investors lakini zi reflect close to real valuation ya bidhaa au investment ili kodi inayokusanywa iwe ni kubwa na investors au wafanyabiashara wajuwe kama hawajafanyiwa usanii. Bado hatujawa serious!
 
Kwa hiyo nchi zote zilizoendelea zilifuata hiyo Libertinism???

Zilifuata principles ambazo ziko kwenye libertarianism bila kujiwakilisha kama full libertarians. Kama marekani unaona wao ndiyo waliifuata principle ya private property rights, right to bear arms, freedom of speech, a right to trial by an unbiased jury, rule of law na hata zamamani marekani baarabara zilikuwa zinajengwa na wawekezaji binafsi. Marekani imeeanza kupata matatizo ya kiuchumi ilivyo acha hizi Libertarian Principles na ikaanza kuongeza kodi na ukubwa wa serikali.
 
Kichwa cha habari kinasema Tanzania iige mfano wa Botswana. Unafungua post kuangalia huo mfano wa Botswana, hukutani hata na sentensi moja yenye neno Botswana. Hii ndiyo reflection ya aina ya elimu tunayoipata au ni sisi wenyewe tunajitoa ufahamu deliberately?

Nimeweka hicho kichwa kuvutia watu. Lakini pia Botswana imeiga libertaarianism na ndiyo maan wana hizo rights na rule of law ambayo inawezesha biashara yao ya zahabu iwe na mafanikio.
 
Kuna sehemu umeandika serikali inakusanya kodi ndogo ( kidogo).........hizo nchi zinaendeleaje bila kodi?

Uongo mkubwa duniani ni kwamba serikali ndiyo inaleta maendeleo ya nchi na kwamba inahitaji kukusanya kodi kubwa. Ukweli ni kwamba serikali ikikusanya kodi kubwa inauwa sekta ya biashara. Kodi ikiwa ndogo wafanya biashara wanaajiri watu wengi zaidi, wana wekeza zaidi, watu wenye kiwango kidogo cha pesa wanaweza kuanzisha biashara wenyewe kwasababu kuna faida.
Ukiangalia Tanzania bidhaa bora, huduma bora, na vingine vingi vinatokana na sekta binafsi. Ukiongeza kodi gharama ya watu kuishi inakuwa na umaskini unakuwa. Lakini ukishusha kodi gharama ni ndogo na watu wnakuwa na uhuru wakutumia hiyo hela kwenye uchumi wa nchi.
 
Mimi sikubaliani na wewe kwa Tanzania kufata mfumo huo:

1. Serikali ndogo: Hao wasomi na vijana walohitimu masomo watafanya kazi gani?. Ajira kutoka serikalini ndio njia moja kubwa ya wealth distribution Tanzania. Na ukubwa unaouona wa serikali yetu lakini bado kazi hazifanywi, jee itakuwaje kukiwa na wafanyakazi kidogo? Ziko sehemu za kubana matumizi lakini si kupunguza waajiriwa serikalini. Tatizo kubwa ni kuwa hela wanakula wachache kwa kupeana upendeleo wa ajira na tenda na sio kugawia kampuni tofauti tofauti.

2. Kodi ndogo: Tanzania kodi ni kubwa kwenye karatasi (averaging 25%) na VAT on import ya 18% na kesi chache excise duty (0-50%). Lakini ki uhalisia kodi inayolipwa haizidi 5%. Kwa sababu karibu bidhaa zote zinazoingizwa nchini zimekuwa under-valued ikiwa na maana thamani yake inayotumiwa kutolezwa kodi ni chini sana in most case 15% ya actual value. Kwa maana hiyo 25% ya import duty inageuka inakuwa 3.75%. Sasa Serikali ikiweka 5% itageuka kuwa 0.75% hatima yake.

3. Uhuru wa kununuwa na kuuza bidhaa: Mpaka sasa Tanzania hakuna control ya kutosha (narudi kwenye waajiriwa kidogo) inayosababishwa na wataalamu haba ama waajiriwa wachache wa kulinda maslahi na afya ya mlaji. Tukiachiwa kuuza na kununuwa tunachotaka, tutauziana mavi ya panya kama ni dawa na chakula. Mimi (nakubaliana na wewe) siamini kwamba kuzuwia bidhaa kuagizwa nje kutainua uchumi wetu, kitakachotokea ni kujaza mifuko ya wachache kwa sababu Tanzania ni kubwa na inategemewa na mpaka majirani zetu kwa bidhaa. Ukiunganisha na uhaba wa teknolojia na umeme wa kuaminika bila kusahau wizi, bidhaa lazima zitakuwa bei ya juu na adimu.

Tanzania tuna nafasi nyingi tu za kuinua uchumi wetu, tusilazimishe mbinu ambazo kwa kwetu haziwezi kufanya kazi. Hatuwezi kuwa nchi ya viwanda kwa sababu ya uhaba wa advanced technology ambayo inapunguza gharama za uazlishaji bila ya kusahau umeme wa uhakika ikiwemo miundo mbinu ya huo umeme. Kuwa na gesi hai guarantee uhakika wa umeme ikiwa miundo mbinu ni mibovu. Kilimo na mazao ya ufugaji kwetu sisi ndio best option kama tutaamua kuwa makini nayo. Kama hatuwezi kushindana kwenye soko la saruji nje kwa nini tusiuze kokoto na mchanga (kigezo cha mazingira kufatwa). Kama sukari yetu ina bei kubwa soko la nje kwa nini tusiuze na kuagiza ya rahisi tukatumia? Kama tuna graduates wengi hawana kazi kwa nini Serikali isiingie mkataba na nchi kama Dubai wakaenda kufanya kazi kwa miaka 2-5 wakatoka kimaisha na kupata experience. Kwa nini serikali isishushe rates za kodi (kushawishi EAC partners) ili zionekane zina mvuto kwa investors lakini zi reflect close to real valuation ya bidhaa au investment ili kodi inayokusanywa iwe ni kubwa na investors au wafanyabiashara wajuwe kama hawajafanyiwa usanii. Bado hatujawa serious!

Hata ikitokea kupunguza hao wafanyakazi wewe huwezi kutoka lakini usiseme uwongo kuwa kodi ya 18pacent iko kwenye makaratasi. Serikali Duniani kote haiwezi Kuleta mabadiliko ikiwa inategemea kodi iliyokuwa haina uhuru wa kufanya Biashara.
Serikali ya Tanzania inakusanya kodi kubwa kuwabana wafanyabiasha Na wanunuzi.
 
Mtoa mada amelonga madini tupu. Ingefaa asikilizwe japo nasikitika kwamba hataeleweka kwa sababu maudhui yake yako juu kuliko uwezo wa wengi kufikia.

Ni wangapi wanafahamu kuwa benki kuu ya marekani ni shirika binafsi? Ya kwamba barabara na madaraja mengi huko ni mali za makampuni binafsi pia?
 
Hata ikitokea kupunguza hao wafanyakazi wewe huwezi kutoka lakini usiseme uwongo kuwa kodi ya 18pacent iko kwenye makaratasi. Serikali Duniani kote haiwezi Kuleta mabadiliko ikiwa inategemea kodi iliyokuwa haina uhuru wa kufanya Biashara.
Serikali ya Tanzania inakusanya kodi kubwa kuwabana wafanyabiasha Na wanunuzi.
Kwanza uelewe kwamba mimi si muajiriwa wa taasisi yoyote Tanzania.

Pili inaonesha upeo wako ni mdogo sana kwenye hesabu za kibiashara. Ikiwa ushuru wa Kitenge ni 50% + VAT @18%. Kama sheria za ushuru ungekuwa unafatwa hasa, kitenge kilitakiwa kilipwe si chini ya 250 milioni kwa container ya 40 ft badala yake inalipiwa 70 milioni.

Makadirio ya kodi ya mapato ya wafanya biashara wingi Kariakoo ya mwaka 2016-17 wameambiwa ni mil 3 kutoka 750,000 kwa mwaka waliyozowea, wote wanapiga kelele. Hii ni sawa na kusema mfanya biashara hapati net profit ya 1,500,000 kwa mwezi? Lakini mfanya biashara huyo huyo anao uwezo wa kulipa pango 2,000,000 kwa mwezi.

Tatizo kubwa katika ukusanyaji wa kodi ni kuwa 50% ya kodi haikusanywi kwa sababu ya kukosa ubunifu wa mbinu za kukusanya hiyo kodi. Kwa hiyo wanaemkamata na ngozi ndiye hummalizia machungu yao. Ingekuwa kodi inakusanywa kama inavyotakiwa basi ungekuwepo uwezo wa kuipunguza na mapato bado yangepanda!
 
Mimi sikubaliani na wewe kwa Tanzania kufata mfumo huo:

1. Serikali ndogo: Hao wasomi na vijana walohitimu masomo watafanya kazi gani?. Ajira kutoka serikalini ndio njia moja kubwa ya wealth distribution Tanzania. Na ukubwa unaouona wa serikali yetu lakini bado kazi hazifanywi, jee itakuwaje kukiwa na wafanyakazi kidogo? Ziko sehemu za kubana matumizi lakini si kupunguza waajiriwa serikalini. Tatizo kubwa ni kuwa hela wanakula wachache kwa kupeana upendeleo wa ajira na tenda na sio kugawia kampuni tofauti tofauti.

2. Kodi ndogo: Tanzania kodi ni kubwa kwenye karatasi (averaging 25%) na VAT on import ya 18% na kesi chache excise duty (0-50%). Lakini ki uhalisia kodi inayolipwa haizidi 5%. Kwa sababu karibu bidhaa zote zinazoingizwa nchini zimekuwa under-valued ikiwa na maana thamani yake inayotumiwa kutolezwa kodi ni chini sana in most case 15% ya actual value. Kwa maana hiyo 25% ya import duty inageuka inakuwa 3.75%. Sasa Serikali ikiweka 5% itageuka kuwa 0.75% hatima yake.

3. Uhuru wa kununuwa na kuuza bidhaa: Mpaka sasa Tanzania hakuna control ya kutosha (narudi kwenye waajiriwa kidogo) inayosababishwa na wataalamu haba ama waajiriwa wachache wa kulinda maslahi na afya ya mlaji. Tukiachiwa kuuza na kununuwa tunachotaka, tutauziana mavi ya panya kama ni dawa na chakula. Mimi (nakubaliana na wewe) siamini kwamba kuzuwia bidhaa kuagizwa nje kutainua uchumi wetu, kitakachotokea ni kujaza mifuko ya wachache kwa sababu Tanzania ni kubwa na inategemewa na mpaka majirani zetu kwa bidhaa. Ukiunganisha na uhaba wa teknolojia na umeme wa kuaminika bila kusahau wizi, bidhaa lazima zitakuwa bei ya juu na adimu.

Tanzania tuna nafasi nyingi tu za kuinua uchumi wetu, tusilazimishe mbinu ambazo kwa kwetu haziwezi kufanya kazi. Hatuwezi kuwa nchi ya viwanda kwa sababu ya uhaba wa advanced technology ambayo inapunguza gharama za uazlishaji bila ya kusahau umeme wa uhakika ikiwemo miundo mbinu ya huo umeme. Kuwa na gesi hai guarantee uhakika wa umeme ikiwa miundo mbinu ni mibovu. Kilimo na mazao ya ufugaji kwetu sisi ndio best option kama tutaamua kuwa makini nayo. Kama hatuwezi kushindana kwenye soko la saruji nje kwa nini tusiuze kokoto na mchanga (kigezo cha mazingira kufatwa). Kama sukari yetu ina bei kubwa soko la nje kwa nini tusiuze na kuagiza ya rahisi tukatumia? Kama tuna graduates wengi hawana kazi kwa nini Serikali isiingie mkataba na nchi kama Dubai wakaenda kufanya kazi kwa miaka 2-5 wakatoka kimaisha na kupata experience. Kwa nini serikali isishushe rates za kodi (kushawishi EAC partners) ili zionekane zina mvuto kwa investors lakini zi reflect close to real valuation ya bidhaa au investment ili kodi inayokusanywa iwe ni kubwa na investors au wafanyabiashara wajuwe kama hawajafanyiwa usanii. Bado hatujawa serious!

Hao wasomi watalazimika kuwa wabunifu na kuanzisha biashara zao wenyewe. Wealth distribution ni uongo mwingine ambao wanasiasa wameanzisha ili kuhalalisha unyang'anyaji wa mafanikio ya wengine kupitia kodi. Wealth Distribution inacho fanya ni kuondoa motisha ya watu kufanya kazi na kuongeza uroo wa nguvu za kiserikali. Tatizo Tanzania kila mtu anataka kuwa mbunge au kiongozi lakini ikija kwenye kuwa mjasiriamali, mwekezaji au mbunifu hawapo. Kwasababu serikali na mfumo wa nchi imeifanya vigumu kuwa mfanya biashara na imeifanya siasa na kukusanya kodi ovyo ovyo, kama biashara. Watu waroho kila siku watataka mali za watu wachapakazi na siasa imewapa njia watu wavivu na waroho uwezo wakuchukua mali ambazo hawajazifanyia kazi.

Hata wewe mwenyewe unakubali kwamba serikali ni kubwa lakini hamna kazi inayofanyika. Kuwa na wafanyakazi kidogo haimaanishi hamna kazi itakayo fanyika lakini inamaanisha wasomi wataacha kuzifuata kazi za serikali na wataanza kujiajiri wenyewe wakijua hamna sehemu yao bungeni au kwenye serikali.

Siyo kazi yao kuchagua kampuni gani inatakiwa kugawiwa hela. Hiyo ni coperatism ambapo serikali ina zuia mashindano kwenye sekta alafu kampuni zinapandisha bei na kutoa bidhaa au huduma mbaya.

Tatizo unaloshindwa kuelewa ni hali ya watu wanaolipa hizo kodi. Haijalishi kama ni 25% au 5%, bado tatizo ni kwamba hiyo kodi ni kikwazo kwenye wafanya biashara wadogo na wanshindwa kuendelea kwasababu yake. Ufumbuzi wa hili tatizo ni kuleta mashindano kwenye ujenzi wa mabandari. Serikali inahitaji kuachia kampuni binafsi zijenge mabandari ili garama ya kuingiza vitu ishuke. Alafu baadala ya kukusanya kodi kutoka kwa wafanya biashara iikusanye kutoka kwa hizo kampuni za bandarini.

Hakuna kontrol ya kutosha? Naona Tanzania mnavyo lelewa na kufundishwa huko shuleni kwa vitisho na kuonewa ndiyo mnafikiri ndiyo njia pekee ya kuleta mafanikio. Unavyo sema watu watauziana mavi ya panya kama dawa ya chakula kwani hilo ni kosa la muuzaji au anayenunua. Kama mtu hafanyi utafiti wakutosha akagundua anacho nunua, huo ni uzembe wake. Kontrol ya uchumi inawafanya watu wategemee serikali na wawe wazembe. Lakini angalieni elimu yenu hata baada ya kuwa na kontrol juu ya wanafunzi haijaendelea. Angalieni serikali yenu. Hata baada ya kuwa na kontrol kwenye uchumu zaidi ya nusu ya nchi iko kwenye umaskini. Hata baada ya kontrol kwenye ardhi bado wananchi wanalala mitaani. Ukifikiria watu watakao uza mavi ya panya unafikiri wakigunduliwa wataweza kufanya biashara tena. Hamna wafanya biashara wengi wanao chukua risk zakijinga kama hizo. Hao ni wahuni wamitaani na kama unafanya biashara na wahuni unapaswa kupata kitakacho kupata.

Matatizo ya Tanzania yanafuatana na kutegemeana. Tatizo la umeme linafuatana na serikali kuto kuweka mashindano kwenye sekta hiyo ya uzalishaji wa umeme. Serikali, kwa sheria ilizo weka kutoka mwanzoni wa hii nchi, inadhibiti kampuni ambazo zingeweza kutuletea hiyo technology na umeme hapa hapa tanzania. Wanasiasa wanauhusiano na hizo kampuni walizochagua kutuzalishia umeme na ndiyo maana wanazuia uhuru wa hiyo sekta. Zipo sehemu mia kidogo Tanzania ambazo hidroelectric power inge zalishwa na kampuni za nje. Miundo mbinu pia iko chini ya majukumu ya serikali kwasababu serikali inamiliki Ardhi yote tanzania. Watanzania wanahitaji kulalamikia umiliki wa ardhi kama wanataka hii nchi iendelee kwasababu wawekezaji wanje hawata weza kuijenga hiyo miundo mbinu bila kuwa na motisha ya kumiliki mali na kupata faida. Angalia kote kuliko endelea miundo mbinu imejengwa kwasababu watu walikuwa na motisha ya kupata faida.

Siyo swala lakuwa serious bali ni swala la kuacha kutegemea serikali ifanye haya mambo. Serikali inacho hitaji ni kuondoa sheria zinazo zuia mashindano kwenye ujenzi wa sekta za umeme, miundombinu, elimu, afya, na viwanda na pia inahitaji kuruhusu na kulinda umiliki wa mali kwa wananchi na wawekezaji wa ndani na wa nje ya nchi. Pia serikali inahitaji kuondoa wizara zote na kuwa na wizara mbili tu. Wizara ya biashara na wizara ya ulinzi.
 
Back
Top Bottom