ArchAngel
JF-Expert Member
- Oct 11, 2015
- 4,514
- 3,757
Kutokana na utafiti ambao umefanywa na nchi nyingi duniani, inaonyesha kwamba watu wanaovuta Bangi ni wengi kuliko wale wanaovuta Sigara..!! Pamoja na kwamba bangi inavutwa zaidi kuliko Sigara, lakini inavutwa siri na kwa maana hiyo Serikali haipati kodi yoyote kutoka katika zao hilo ambalo hulimwa sana, huuzwa sana na huvutwa na walipakodi wengi kifichoni..!! Sigara ambayo ni moja kati bidhaa chache sana zinazochangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la taifa duniani, bado inavutwa na watu wachache sana, wakati bangi inayovutwa na watu wengi kote duniani haina kodi au kwa maneno mengine kodi imefutwa…!!!Mwaka jana mwishoni Serikali ya Uruguay ambayo ipo kwenye bara la Amerika ya kusini ilikuwa nchi ya kwanza kuanza kutoza kodi kwenye zao la bangi, baada ya kuruhusu wananchi wa nchi hiyo kulima kwa wingi zao la bangi, kuuza na kuvuta bila ya kificho. Wataalamu wa uchumi wa nchi hiyo ya Uruguay wanasema kwamba baada ya Serikali kuruhusu zao la bangi kulimwa kwa wingi, wavutaji wa Sigara wameanza kupungua kwa vile wengi wamehamia kwenye kuvuta bangi; pia wakulima wapya wakubwa wa bangi katika nchi hiyo wameongezeka kwa kiasi kikubwa kwa kipindi kifupi tu cha miezi michache tangu Serikali iruhusu ukulima wa zao hilo; kujitokeza kwa wakulima wakubwa wa zao hilo kumeweza kupunguza idadi ya wasiokuwa na kazi katika nchi hiyo; kwa maneno mengine ni kwamba ukulima wa bangi umepunguza tatizo la ajira kwa vijana katika nchi hiyo. Kilimo cha zao la bangi kimepanua sekta ya kilimo kwa kiasi kikubwa; viwanda vinavyotengeneza pembejeo za kilimo zikiwemo mbolea na zinginezo shughuli zake zimepanuka jambo ambalo limechangia kutengeneza ajira mpya za moja kwa moja na zile ajira tegemezi (direct and indirect jobs), pia bila kusahau mapato ya taifa yameongezeka. Wachumi hao wa Uruguay wanaendelea kutabiri kwamba pato la taifa la nchi hiyo mwaka huu wa 2014 litaongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na kichocheo cha kuruhusu kilimo cha bangi katika nchi hiyo.
Hivi karibuni mwezi January 2014 jimbo la New Mexico huko nchini Marekani limepeleka musuada wa sheria bungeni ili bunge la nchi hiyo liangalie uwezekano wa kuruhusu zao la bangi kulimwa, kuuzwa na kuvutwa bila ya kikwazo chochote, na wakati huo huo Serikali kutoza kodi kwa wadau wote wa zao hilo. Kulingana na wachambuzi wa mambo ya uchumi kwenye jimbo hilo na Amerika kwa ujumla ni kwamba uwezekano wa bunge la nchi hiyo kupitisha musuada huo ni mkubwa kwa vile bangi inavutwa na watu wengi zaidi kuliko Sigara inavyovutwa, na hakuna kodi yoyote inayoenda serikalini..!!! Rais Barrack Hussein Obama wa Marekani amekuwa ndiye rais wa kwanza wa nchi hiyo ambaye serikali yake imeweza kutilia mkazo wa utafiti wa zao la bangi kwenye sekta ya matibabu, watangulizi wake waliomtangulia walikuwa hawakulitia sana maana zao la bangi ambalo ni zao linalotumika kwa wingi katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa kuliko nchi nyingine yoyote duniani; hata watu wengi wan chi hiyo bado wana amini kwamba huenda Serikali ya Barrack Obama ikalegeza masharti ya matumizi ya bangi kwenye siku za usoni.
Serikali ya Uingereza hivi karibuni nayo imekuwa katika majadiliano na washauri wa mambo ya uchumi wan chi hiyo juu ya uwezekano wa kuruhusu zao la bangi kulimwa, kuuzwa na kuvutwa au kuliwa bila ya kikwazo chochote na huku Serikali nayo ikitoza kodi kuhusu zao hilo. Serikali ya Uingereza pia inakiri kwamba inapoteza mapato makubwa ambayo ni mabilioni ya Pound (Billions of Pounds) kwa mwaka kutokana na bidhaa ya bangi kutoruhusiwa na Serikali; Watu waengi wan chi hiyo wanavuta bangi zaidi kuliko wale wanaovuta Sigara. Sigara ni moja kati ya bidhaa chache zinazochangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la nchi hiyo..!! Pamoja na kwamba bangi inatumiwa na kuliwa na watu wengi zaidi lakini serikali haipati mapato yoyote..!!! Miaka ya nyuma Serikali ya Uingereza na Serikali zingine za nchi za Ulaya walikuwa wanapinga kuingizwa kwa Mirungi kwenye nchi zao wakidai kwamba ni madawa ya kulevya, lakini hivi sasa Mirungi inaingia na inauzwa na kuliwa kama mboga za majani zinavyoliwa, na wakati huo huo serikali zikijitahidi kukusanya kodi zake.
Je, Sigara na Bangi Kipi Hatari kwa Maisha ya Binadamu..?
Sigara pamoja na kwamba imeruhusiwa na kila Serikali duniani kulimwa, kuuzwa na kuvutwa, lakini sigara ni hatari sana kwa afya ya binadamu; Sigara ina sumu ya “Nicotine” ambayo inasababisha cancer ya kwenye mapafu. Bangi pamoja na kwamba inapigwa vita na ni marufuku kuonekana unalima Bangi, unauza bangi au unavuta Bangi, lakini Bangi ni bidhaa salama ambayo haina sumu ya aina yoyote kama ile iliyoko kwenye Sigara.
Kwanini Bangi Imekatazwa na Nani Hasa Yupo Nyuma ya Hili..?
Dunia ina nchi nyingi na ina mabara saba, pamoja na dunia kuwa na nchi nyingi zenye uhuru kamili wa kujiamulia mambo yake zenyewe bila ya kuingiliwa na nchi nyingine, lakini bado dunia inatawaliwa na Marekani na Uingereza, nchi ambazo zina ushawishi mkubwa kiuchumi, kitekinolojia, kisiasa na kidiplomasia. Nchi hizi mbili bado zinaitawala dunia kifikra na kiuwezo wa kutoa maamuzi mbalimbali duniani. Waingereza na Wamarekani ndizo nchi za kwanza duniani kuanzisha mashamba ya zao la Tumbaku ikiwa ni nchini Marekani kwenyewe na nchi zingine mbalimbali duniani ambapo Uingereza ilikuwa inazitawala; hivyo kutokana na ukweli huo Waingereza na Wamarekani wakawa ndiyo watu wa kwanza duniani kujenga viwanda vikubwa vya kutengeneza Sigara kwenye nchi zao na vingine vidogo vidogo kwenye nchi zingine na zile makoni yao. Kulingana ukweli huo Uingereza na Marekani wakawa ndiyo wanamiliki biashara ya zao la tumbaku na bidhaa zake (Monopoly), hivyo wakaona kwamba pamoja na kwamba Sigara ina sumu inayoleta ugonjwa wa cancer ya mapafu kwa watumiaji, lakini wakaona Sigara iendelee kuhalalishwa kama bidhaa halali, isipokuwa bidhaa zingine zote zinazoweza kuvunja soko la Sigara kama vile Bangi zipigwe marufuku kwamba ni madawa ya kulevya. Na hili limewezekana kwa vile wenye viwanda vya kutengeza Sigara wana ushawishi mkubwa kwenye Serikali zao na dunia kwa ujumla; pia Serikali za nchi hizo zinapata mapato makubwa yanayotokana na kodi ya Sigara licha ya kwamba wanajua fika kwamba wanawalisha wananchi sumu..!! Nchi hizi za Magharibi pia zinaogopa sana ushindani wa kibiashara, kwa vile wanafahamu fika kwamba wakiruhusu zao la Bangi kulimwa kama inavyolimwa Tumbaku, basi watakuwa hawana mamlaka yoyote tena sokoni ya zao hilo jipya la Bangi kwenye soko la dunia (Market Power) kwa vile kila nchi itacheza mchezo wake..!!!
Umefika muda ambao sasa dunia imeanza kufahamu siri ya kukatazwa bangi isivutwe kwamba sababu za kukatazwa kwa zao hilo ni za kiuchumi zaidi kuliko kiafya kama ambavyo miaka yote tumekuwa tukidanganywa. Nchi za Magharibi zina maslahi makubwa sana na zao la Tumbaku na nchi hizo zimewekeza kwa kiasi kikubwa hivyo ni hasara kimapato kuruhusu bangi itumike kwa vile italiuwa soko la Sigara moja kwa moja. Hata hivyo watawala hao wa dunia (Uingereza na Marekani) wapo kwenye meza ya mazungumzo na matajiri wa nchi hizo ambao hasa ndiyo wamewekeza zaidi kwenye bidhaa ya Sigara, ili waangalie uwezekano wa wao kuiruhusu dunia kwamba ianze kutumia Bangi kwa vile haina madhara; mazungumzo yapo mezani kwa miaka mingi, lakini bado wanavutana, ila kwa zile nchi za dunia ya tatu ambazo viongozi wao wana fikra huru wao wamechoka kuwa watumwa wa fikra kwa miaka mingi na wameshaanza kuwaruhusu wananchi wao kulima, kuuza na kuvuta zao la Bangi bila wasiwasi ili mradi walipe kodi.
Tanzania ni Taifa Lililoshindwa Maisha Ambalo Limekuwa ni Taifa la Kuigaiga na Kufuata Mkumbo Hasa wa Nchi za Magharibi..!!!
Kulingana na utafiti wangu wa miaka mingi toka utotoni hadi ukwengweni hivi sasa, nimegundua na kuthibitisha kwamba zao la bangi nchini linalimwa zaidi kuliko yanavyolimwa mazao ya mahindi na maharage..!!! Licha Bangi kulimwa sana kuliko mahindi na maharage, lakini pia Bangi inavutwa na kuliwa na watanzania wengi zaidi kuliko wale wanaovuta Sigara..!!! Pamoja na serikali ya Tanzania kuiga sheria za nchi za Magharibi na kuzikumbatia kwa miaka yote 53 ya uhuru, lakini ni kwamba viongozi wengi tena wa ngazi za juu kabisa wa Serikali hii ya TANU/CCM wamekuwa ni wadau wazuri sana wa zao hili la bangi; hakika kuna wengi ikipita siku bila kulitia zao hili mdomoni mwao, basi wanajiona kama siku hiyo haikukamilika..!! Maofisa wengi wa Serikali wanatumia bidhaa hii huitumia wakati wanapoenda msalani (chooni) kujisaidia. Kuna majina makubwa kwenye uwanja wa siasa za Tanzania ambao hivi sasa wameshatangulia mbele ya haki, basi hao walikuwa wadau wazuri na wakubwa wa zao hili la Bangi licha ya kwamba walilipiga vita kwenye majukwaa yote ya siasa..!!! Walilipiga marufuku zao hili kwa vile walikuwa viongozi wa kunukuu yale yanayosemwa na nchi za magharibi, lakini hawakuta kuwa wabishi na watundu wa kutaka kufanya utaffiti wa kisayansi na kujua ikiwa kwamba Sigara itaitwaje halali, lakini Bangi ipigwe marufuku…!!! Utafiti pia unaonyesha kwamba viongozi wengi wa ngazi za juu wa Serikali za dunia nzima wanatumia sana zao la Bangi; hivi majuzi Rais wa 42 wa Marekani Bill Clinton alinukuliwa na vyombo vya habari akisema:
{ 'I Never Denied That I Used Marijuana' Former President Bill Clinton said he "never denied" smoking pot.
“I didn’t say I was holier than thou, I said I tried,” Clinton told Fusion's Jorge Ramos recently. “I never denied that I used marijuana. I told the truth, I thought it was funny."
When asked about drugs during the presidential race in 1992, Clinton famously said he experimented with marijuana but "didn't inhale."
"When I was in England, I experimented with marijuana a time or two, and didn't like it," Clinton said. "I didn't inhale and I didn't try it again."}
Kwa vile tumekuwa taifa la kusikiliza wazungu wanasema nini? Tumeambiwa eti Mirungi ni madawa ya kulevya na tumeamini na kupiga marufuku, bila hata ya kumtumia mkemia wetu mkuu kuchunguza kama kweli Mirungi ina “Nicotine” ndani yake, bali tumekubali na kuwapiga wananchi wetu marufuku na wengine wanaozea jela kwa kukutwa na bidhaa hiyo haramu..!! Kwa vile sisi ni taifa la kufuata mikumbo, tumepiga marufuku ukulima wa Mirungi na matumizi yake kwa ujumla, lakini nchi za jirani kama vile Kenya wao wanaruhusu Mirungi ilimwe na utumiwe kwa matumizi mbalimbali ya binadamu na wanyama; kulingana na ukweli huo Kenya imekuwa ikipokea maelfu ya tani za zao la Mirungi inayolimwa nchini Tanzania kwa kificho na kusafirishwa kupitia njia za panya kwenda Kenya, ambapo Serikali ya nchi hiyo inajipatia mapato makubwa ya kodi kupitia bidhaa hiyo haramu Tanzania, lakini halali nchini Kenya..!!!
Tumepiga marufuku ukulima na matumizi ya Mirungi hapa nchini, lakini kulingana na utafiti unaonyesha Mirungi inaliwa zaidi kuliko zao la kabichi linavyoliwa hapa nchini; pia utafiti unaonyesha kwamba zao la Bangi linalimwa zaidi hapa nchini kuliko yanavyolimwa mazao ya mahindi na maharage..!! Ukitaka kuthibitisha utafiti huo mtafute IGP Mangu atakuambia, ila usimpigie simu, bali mtafute umvute pembeni kwa faragha atakuambia. Naamini hata Rais Kikwete hafahamu kuhusu hilo, na kama angelijua kwamba Bangi angelitoa tamko la Serikali la kuidhinisha kisheria zao hilo ili lilimwe, liuzwe na liliwe na kuvutwa hadharani na wananchi; na kwa kufanya hivyo Serikali ingelipa mapato makubwa kodi yatokanayo na bidhaa hiyo; pia Serikali ingeliweza kupanua wigo wa sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kutengeneza ajira nyingi za moja kwa moja na zile shirikishi (direct and indirect jobs).
Dr. Noordin Jella
SOURCE: Tanzania Ihalalishe Bangi: Watu Wengi Wanavuta Bangi Kuliko Wale Wanaovuta Sigara…!!!
katika pitapita zangu za mtandaoni nimekutana na hiki kitu, karibu tujadiliane wanajamvi bila kejeli, dharau, wala matusi.
nawasilisha