N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,111
- 10,214
SHANGHAI - Ndege ya kwanza ya abiria iliyojengwa nchini China kwa mara ya kwanza imefanyiwa majaribio kwa kuruka Ijumaa hii ya Mei 5,2017, jaribio hilo linatajwa kuwa ni hatua kubwa katika malengo ya muda mrefu ya Taifa hilo kuvunja utawala wa soko la ndege hizo kutoka nchi za Magharibi.
Kuruka kwa ndege hiyo aina ya C919 kuliibua shangwe na vifijo kutoka kwa wageni waalikwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Shanghai Pudong ambapo tukio hilo lilirushwa mubashara na runinga ya Taifa.
Mara baada ya kuruka muda mfupi ilipotelea mawinguni katika anga lililojaa utusitusi wa anga jeusi lililosindikizwa na upepo na wingu la ukungu katika jiji la Shanghai
Kufanikiwa kwa jaribio hilo kwa mujibu wa Shirika la Habari la China
Xinhua kunaifanya Uchina kuwa Taifa la nne kwa uundaji wa ndege kubwa za abiria baada ya Marekani,Ulaya na Urusi.
Ndege hizo C919 zinatarajiwa kutoa ushindani mkubwa kwa chapa maarufu duniani ambazo ni Airbus A320 na Boeing 737 zinazoundwa Ulaya na Marekani.
Ndege hizo zilikuwa zijaribiwe mwaka 2014 kabla ya kuruhusiwa sokoni, lakini hitilafu za kiufundi zilichelewesha mpango wa majaribio hadi mwaka huu.
Hata hivyo,kukamilika kwa ndege hizo hakuifanyi C919 kuanza kazi ya kusafirisha abiria mapema hadi hapo 2019.
Baada ya ripoti ya jaribio kuwasilishwa mtengenezaji wa ndege ambalo ni Shirika la Taifa Commercial Aircraft Corp. of China Ltd., au Comac, litaanza mchakato wa kuomba kibali cha ndani na nje ili ndege zake zianze kuzalishwa.
Meneja Msaidizi wa Comac Bao Pengli, anasema kampuni yao itaunda ndege mbili kwa mwaka kuanzia sasa hadi 2019 ili kupata uhakika wa ubora kabla haijaanza uzalishaji mkubwa.
Comac inasema tayari imepokea oda kutoka kwa wateja 570 nyingi ya oda ni kutoka ndani na nje,ambapo oda za nje ni pamoja na zile za Shirika la GE Capital Aviation Services na Thailand City Airways.
C919 itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 155-175 na kiwango chake cha uwezo wa masafa ni kilomita 4,075.
Comac inasema kampuni 200 za China kwa pamoja na Vyuo Vikuu 36 vimehusishwa kufanikisha mradi huo katika eneo la Utafiti na Ujenzi wa ndege ambapo Injini zimeundwa nje ya Uchina kutoka CFM International. Hata hivyo injini zilizoundwa China zitakuwa tayari 2020.
Ikumbukwe kwamba hii ni hatua ya mbele zaidi baada ya mwaka 2016 nchi hiyo Kufanikiwa kuunda na kuiingiza sokoni ndege ya wastani ya abiria aina ya ARJ-21,ambayo tayari imeleta ushindani wa soko kwa ndege za Canada Bombardier zinazoundwa na Bombardier Inc. sanjari na Embraer SA za Brazil.
First large Chinese-made passenger jet makes maiden flight
MY TAKE: Tanzania tufikirie kuhamisha focus yetu ya uteja na Westerners kwenye hii biashara ukizingatia kuna wasiwasi wa kupigwa hata bei zao ni juu sana $90 and above wakati Comac wanasema ndege zao zitakuwa bei chee na za kuvutia,hata bombardier nyingine tununue kwao.