Tanzania hatuna viongozi tuna watawala. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania hatuna viongozi tuna watawala.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 28, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwaka 2005 ulikuwa mwaka wa matumaini kwangu,mwaka ambao niliona huenda Tanzania ikageuka kutoka safari yake ya kuelekea kusini,na ikaanza safari kwenda kaskazini.Na hotuba ile nzuri ya Kikwete ikagongelea msumari wa matumaini ya angalau maisha bora kwa wanachi wetu maskini.Kwa kweli mimi sikujifikiria sana, kwa vile angalau nilikuwa naweza kupata mhogo na chai ya rangi asubuhi,na siku ikiwa na neema kidogo, andazi na chai ya maziwa, kifungua kinywa ambacho kwa wananchi wengi wa Tanzania,ni ndoto ya alinacha.Kumbe nilikuwa naota ndoto za mchana,niliyokuwa nayaona yalikuwa maruerue.Siku zilivyozidi kupita, matumaini yale yakaanza kufifia, na hatimaye yakapotea kabisa na giza nene likaanza kutanda mbele.Leo hii ninapo andika makala hii ni watanzania wachache ambao utasikia wakiongea jema kuhusu serikali ya awamu ya nne.Wananchi waliyo beba ni majeraha yasiyopona ambayo hutoneshwa kila kukicha na tuhuma nzito nzito za wizi wa fedha za wananchi, aidha moja kwa moja au kupitia kwenye mikataba mibovu nk. Tuliotegemea wangekuwa viongozi wetu wamegeuka kuwa watawala na watesi wetu.Kwa maana kiongozi ni yule anayeonyesha njia katika yale waliyokubaliana na waliomchagua au katika yale ambayo kiongozi anaona ni ya manufaa kwa wale anaowaongoza.Na katika hili lazima kuwe na nia njema.
  Tunacho ona leo ni kinyume kabisa na matarajio yetu.Viongozi hawa wamekuwa mwiba mrefu ambao kila utembeapo huingia kwenye nyama.Wanafanya wanayotaka wao, sio tuliyo watuma sisi wafanye.Kama vinyonga hugeuza maneno kuhalalisha hata yale ambayo kwa akili za kawaida kabisa ni upuuzi.Watawala hawa hawana aibu kabisa katika yale wayafanyayo.Kwao shida yetu ni furaha yao.Mbaya zaidi hushirikiana moja kwa moja na washirika wao wa mataifa ya nje katika uovu wao.Sina shaka kwmba yanayofanywa nyuma ya migongo yetu ni magumu hata kuyaongelea.Watu hawa wamepoteza sifa za kuongoza na imani kwa wanachi kabisa.Kiongozi anapokosa imani kwa wanachi,hiyo itoshe kumfanya asifae kuwa kiongozi tena.Haijalishi kama kupotea kwa imani ni halali au sio halali.La msingi ni kwamba wananchi hawana imani na yeye.Hiyo itoshe yeye kuondoka. Tunachoona katika viongozi wetu ni tofauti kabisa.Wanaendelea kung'ang'ania madaraka hata pale ambapo wananchi hawana imani nao kabisa.Maswali ya kujiuliza ni kwamba wana muongoza nani,katika yapi na wanachong'ang'ania hasa nini?Inapopofika hatua hii,hawa sio viongozi tena,ila watawala.Hawaongozi tena kwa ridhaa ya wananchi.Ni vema viongozi wetu wakajihoji,kwa vile kwa sasa, wengi wako katika hatua hii.Imani kwao imekwisha kabisa.Aidha ni vema wakajirekebisha au wakapisha wengine ambao wana nia ya kweli ya kuwasaidia wananchi wa Tanzania katika matatizo yao.Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ndio hiyo sisiemu inayojidai kuwa inakubarika kwa wadanganyika.
  Ukweli haikubariki maana waliomo ni wezi tupu. Sioni wa kumu exclude katika kundi hili. ndio maana mahali pengine chama hiki cha wezi kinaitwa chukua chako mapema. Mtanisamehe.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Tusiwahukumu wote kwa ule msemo wa samaki mmoja akioza basi wote wameoza....Kuna watu waadilifu na wenye kupenda kuitumikia nchi na wananchi wake... tatizo ni kuwa unapotaka kufanya kweli...wenzio wote wanafanya uongo! matokeo yake nadhani tunayajua. Nini basi kifanyike? wengine watasema bora kujiondoa au kujitenga na uongozi mbaya/mwovu kwa kujiuzulu.Lakini pia kuna msemo unaosema " ukisusa, wenzio wala" .Bora ukae humohumo ili ujue kinachoendelea na ikiwezekana kupambana ukiwa ndani.Sijui lakini kama kweli tuna critical mass ya wenye uchungu wa kweli na nchi ndani ya system ambao wanaweza kuleta mabadiliko ya kweli.Vinginevyo tutaishia kulalamika bila action yoyote na wahusika watasema " kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji" kazi tunayo wananchi/wenyenchi!
   
 4. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hapa mkuu umeongea suala muhimu sana,kuna watawala na viongozi.Ebu niambie kwa mtazamo wako,nani ni kiongozi unaedhani CCM tukiifukuza madarakani tutampa atuendeshee nchi.Ukiangalia kwa makini hakuna mwenye afadhali,ukiangalia hao wapinzani wenyewe kila siku wanagombana,kisa pesa.

  Cha muhimu ni sisi wananchi tujenge tabia ya kuwawajibisha viongozi wetu,kama hivi sasa ccm inaonekana haina jipya tunakiwajibisha kwa kukiweka pembeni ya madaraka.Hii ingeleta discipline na uwajibikaji kuanzia kwa wenyeviti wa mtaa mpaka kwa rais,kwani watakuwa wakijua ya kwamba wasipofanya tulichowatuma ni lazima tutawawajibisha.Vinginevyo tutalalamika sana huku hali ikiendelea kuwa ngumu kila siku.
   
 5. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Wakati mwingine hata mie uamini hivyo,kwamba katika system wapo wenye uchungu na nchi hii na watu wake.Unajua wakati mwingine watu wanshindwa kuelewa kuwa hata siasa ni fani,si kila mtu ataingia nakuanza kupiga soga kisha akatufikisha tunapotaka.kwani bongo flavor hii.Kuna haja hawa watu wangekuwa wanajiuliza mara mia mia,kwanini waliamua kuingia kwenye siasa.Hii ndo sababu hawawezi kusimama pale wanapoitajika kufanya hivyo.Hata kama wewe ni kiongozi mzuri na muadilifu,but you are doing nothing to change the situation,what is the diference;Na wewe umeoza bwana
   
Loading...