Tanzania hatujapata kiongozi mzalendo baada ya Nyerere

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,684
149,887
Nyerere peke yake ndie aliekataa tusichimbe madini kwasababu tulikuwa bado hatujajiandaa na akasema maadam hayaozi ni bora yabaki ardhini.

Huyu ndie Baba wa Taifa ingawa nae alikuwa na mapungufu yake lakini sio kama haya ya kibinafsi na kifisadi.

Kama tuna au tumewahi kupata Nyerere mwingine niambieni ni nani huyo ambae mikataba anayoingia kwa niaba ya nchi iko wazi na analishirikisha au amewahi kulishirikisha Bunge.

Nyerere alilinda maliasili zetu ila ni nani ana uhakika maliasili zetu leo hii zinalindwa ili hali mikataba haijui/hajaiona?

Naombeni mnitajie kama yupo huyo wa kufanana na Nyerere.
 
nyerere alimjali mwananchi wahali ya chini mf mkulima,mfugaji nk. Saivi vijijini hawana mtetezi mipango yote daslam ili kumwinua bashte aonekane bora kukomoa wanaompinga!! Mambo za ajabu
 
Nyerere peke yake ndie aliekataa tusichimbe madini kwasababu tulikuwa bado hatujajiandaa na akasema maadam hayaozi ni bora yabaki ardhini.

Huyu ndie Baba wa Taifa ingawa nae alikuwa na mapungufu yake lakini sio kama haya ya kibinafsi na kifisadi.

Kama tuna au tumewahi kupata Nyerere mwingine niambieni ni nani huyo ambae mikataba anayoingia kwa niaba ya nchi iko wazi na analishirikisha au amewahi kulishirikisha Bunge.

Nyerere alilinda maliasili zetu ila ni nani ana uhakika maliasili zetu leo hii zinalindwa ili hali mikataba haijui/hajaiona?

Naombeni mnitajie kama yupo huyo wa kufanana na Nyerere.
Wazee wa zamani wangekuwa wanaingia humu JF nao wangekubishia sana.Wao walimwita Nyerere "haambiliki".Maana yake alikuwa hashauriki.Pia aliitwa dikteta.Lakini kweli kila alichofanya ilikuwa kwa nia njema.Hakuwa mbinafsi.Nadhani wanafanana na Magufuli.
 
Hata huyu naye ana deal lake la Bilioni nane kivuko Kibovu cha mwaka 1928,nina wasi hata hii reli ikija haitafanya kazi yale yale madeal ya GAS yatageuka kuwa miundo mbinu,tutegemee Reli ya mwaka 1940
 
Wazee wa zamani wangekuwa wanaingia humu JF nao wangekubishia sana.Wao walimwita Nyerere "haambiliki".Maana yake alikuwa hashauriki.Pia aliitwa dikteta.Lakini kweli kila alichofanya ilikuwa kwa nia njema.Hakuwa mbinafsi.Nadhani wanafanana na Magufuli.

Hata kwa 1% hawafanani na Magufuli,usimpe sifa mtu ambaye hana hata chembe.

JKN hakuwa na Chuki,Ukabila wala Visasi.Hakuwahi kuiba wala kuwa na madeal.
 
Nyerere atabaki kuwa nyerere.. hakutatokea nyerere mwingine.
Though kuna viongoz miungu watu wanajaribu ku copy... lakin hawatokaa wamfikie
 
Ila wa sasaivi ndo mhuni kuliko wote.....
Keshaanza kujijengea airport chato huku wanafunzi wakikosa mikopo elimu ya juu na elimu bure ikiwa mdomoni mwake huku wazazi wakiendelea kuchangia elimu kwa kiwango zaidi hata kabla yeye hajatangaza....
HUYU NDO RAIS WA WANYONGE
HUYU NDO RAIS KANJANJA WA TZ YA VIWANDA HUKU ANANUNUA NDEGE AMBAZO HAZINA FAIDA YOYOTE KWA MNYONGE....
rais dikteta na mvunja katiba na sheria za nchi hatumtaki....
rais mwenye double standard anayetetea waharifu km BASHITE hatumtaki
 
Mwalimu Nyerere alikuwa mzalendo aliyejali wananchi wa chini kwa vitendo. Hakuwa na haja ya kutamka hayo kila wakati na aliacha watu wajionee wenyewe.
 
Back
Top Bottom