Nimebaini: Mkataba wa madini na ACACIA/Barrick ulisainiwa baada ya kifo cha baba wa taifa

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
37,890
43,782
Hivi kuna uhusiano wowote wa kifo chenye utata cha baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere mwaka 1999, huko London kwenye hospital ya St.Thomas na kusainiwa kwa mikataba (inayosemekana ni ya kinyonyaji) kati ya serikali ya Tanzania na Barrick/ACACIA mwaka huo huo wa 1999. Nauliza tu.

==========================================================
[Samuel Kasori, aliyekuwa Katibu Myeka wa Mwalimu, amezungumza na JAMHURI na kusema; “Mwalimu anakuwa kwenye rekodi ya kufa haraka sana kwa ugonjwa wa saratani ya damu. Ugonjwa huo huua taratibu, lakini kwa Mwalimu ilikuwa tofauti kabisa. Kuna nini kilichotokea? Sitaki kuhoji sana, lakini naamini kuna siku Watanzania na walimwengu wataujua ukweli.”]
Source: Jamhuri 10/2013

==========================================================
Nyerere peke yake ndie aliekataa tusichimbe madini kwasababu tulikuwa bado hatujajiandaa na akasema maadam hayaozi ni bora yabaki ardhini.

Huyu ndie Baba wa Taifa ingawa nae alikuwa na mapungufu yake lakini sio kama haya ya kibinafsi na kifisadi.

Kama tuna au tumewahi kupata Nyerere mwingine niambieni ni nani huyo ambae mikataba anayoingia kwa niaba ya nchi iko wazi na analishirikisha au amewahi kulishirikisha Bunge.

Nyerere alilinda maliasili zetu ila ni nani ana uhakika maliasili zetu leo hii zinalindwa ili hali mikataba haijui/hajaiona?

Naombeni mnitajie kama yupo huyo wa kufanana na Nyerere.

=========================================================
[Maneno ya Kasori yanaendana na ya Mwalimu James Irenge (Mwalimu wa Baba wa Taifa), aliyoyatoa mwanzoni mwa mwaka jana baada ya mvutano wa kisiasa kati ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa, na Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema).
Baada ya kauli ya Mbunge Nyerere kumtaka Mzee Mkapa aeleze chanzo cha kifo cha Mwalimu, Mwalimu Irenge alijitokeza na kusema amefurahishwa mno kusikia kuwa amepatikana kiongozi jasiri wa kuhoji namna Mwalimu alivyougua hadi kufariki dunia.

“Mfikishieni pongezi nyingi Mbunge Nyerere... huyo mtoto amefanya jambo la maana sana kuuliza jambo hili, miaka yote nalia kwa sababu naamini Mwalimu aliuawa.

“Kwa kuwa suala hili limeulizwa hadharani, sasa nipo radhi kufa. Nikifa nitakwenda moyo wangu ukiwa na furaha kwa sababu nimekuwa nikijiuliza ni nani anayeweza kuhoji namna Mwalimu… mwanafunzi wangu alivyokufa,” alisema Mwalimu Irenge.] Source: Jamhuri 10/2013
 
naomba kujuzwa.... hivi wale migodi mingine kama GGM etc hawasafirishi makanikia nje ya nchi? nina hasira na Che Nkapa yaani acha tu..
Kuna utofauti wa mfumo wa uchimbaji wa dhahabu wa GGM na Buzwagi au Bulyanhulu mfumo wa Bulyanhulu na Buzwagi ni mmoja ndo huo unapelekea kuwa na hayo makinikia Tofauti na GGM me siyo mtaalam subiri waje watakupatia mchanganuo
 
JPM anapitia wakati mgumu sana maana anataka kuvunja mfumo ambao umeasisiwa na kukita mizizi. Kwa hakika kama huu mfumo ungelikuwa unanufaisha walau asilimia 35% ya Watz unaweza kuupotezea lakini tatizo unanufaisha chini ya 1% ya Watanzania!
Hii 1% iko tayari kwa lolote na wana vitisho sio mchezo lakini tukiungana kwa zaidi ya 95% tunaweza kuwashinda. Tatizo hata tunaotaka kusapoti kuna vitu hatuvielewi and is not clear on what should we unite to fight for.
 
upload_2017-6-1_12-55-3.jpeg
 
Hivi kuna uhusiano wowote wa kifo chenye utata cha baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere mwaka 1999, huko London kwenye hospital ya St.Thomas na kusainiwa kwa mikataba (inayosemekana ni ya kinyonyaji) kati ya serikali ya Tanzania na Barrick/ACACIA mwaka huo huo wa 1999. Nauliza tu.

==========================================================
[Samuel Kasori, aliyekuwa Katibu Myeka wa Mwalimu, amezungumza na JAMHURI na kusema; “Mwalimu anakuwa kwenye rekodi ya kufa haraka sana kwa ugonjwa wa saratani ya damu. Ugonjwa huo huua taratibu, lakini kwa Mwalimu ilikuwa tofauti kabisa. Kuna nini kilichotokea? Sitaki kuhoji sana, lakini naamini kuna siku Watanzania na walimwengu wataujua ukweli.”]
Source: Jamhuri 10/2013

==========================================================
Nyerere ikibidi afe ili kupisha magumashi hayo
 
Back
Top Bottom