Tanzania has started to build its own helicopters

Mkuu ni kweli wamegundua Chopa????????? Nauliza tu
Hakuna ugunduzi wa chopa unaoweza kufanywa ndani ya miezi miwili kama ilivyoandikwa. Tusijidanganye na theory tulizokariri madarasani, ukiacha ugunduzi wa wazungu, wengine wote kama Japan, China, Afrika Kusini nk wamekuwa wakijifunza na kumodify teknolojia ya wazungu.

Nauliza, Chuo kinayo chopa ya mafunzo ili kujua/kujifunza walao katika hali halisi kwamba chopa ina vitu gani ndani na inafanyaje kazi? Adisai Msongole ni Mhasibu, ugunduzi ni kitu kinachotaka ubobezi, sasa huyu mhasibu alibobea lini kwenye teknolojia ya kutengeneza chopa na kugundua aina mpya ya chopa, au ugunduzi huu ni wa aina gani?

Tuchukulie kwamba ni kweli, chuo kitafanya mass production ya chopa hiyo au tunafanya just for funny?. Ikiwa inafanywa for the sake of humor, ni nini uhalali wa rasilimali zote zitakazokuwa zimetumika?

Wasomi, wanasayansi na wanateknolojia huwa wanahangaika na ugunduzi wa vitu vitakavyotatua matatizo yanayoikabili jamii inayowazunguka. Hivi, tatizo linaloikabili jamii ya watanzania katika kuendesha maisha yao ya kila siku ni kukosekana kwa usafiri wa chopa? .....
 
Helkopta prototype yenyewe hii hapa.

 
Helkopta prototype yenyewe hii hapa.

View attachment 362014
Sikatai, tuendelee na maigizo tu, wakati utasema wenyewe. Watu wanachukua faida ya watanzania kuwa wasahaulifu tu, maana inajulikana kwamba ikifika mwaka huo wa 2018 ambao ndio wa majaribio ya kurusha chopa hiyo wengine watakuwa hawapo na wengine watakuwa wamesahau.

Tukumbushane kuhusu shamba la Oljoro ambalo miaka mitano iliyopita Waziri aliahidiwa kama angerudi baada ya miaka mitatu angekuta shamba likiwa kijani tupu, leo imekuwaje? Licha ya kupata misaada mbalimbali ikiwemo ya shirika la misaada la Uingereza (DIDF) kiasi cha milioni 300,000,000/=, fedha hiyo inasadikika kuishia mifukoni mwa wajanja wachache, na hatima ya mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya wanafunzi wa fani ya ujenzi na umwagiliaji kwenye shamba hilo imebaki kwenye kiza kinene.

Hivyo, si dhambi kusema, kinachodaiwa kuwa ugunduzi wa chopa ni wimbo wa kusindikiza wakati tu
 
Ninaogopa kusikia kuwa uvumbuzi wa chopper unachukua muda mfupi kama vile kutengeneza toy. RIP watakaotest hizo chopper
 



District Irrigation Development Fund (DIDF) inadhaminiwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) na sio shirika la misaada la Uingereza. kwanza Uingereza haina shirika la Misaada sijui wewe umelipata wapi ?....... upo bize na upotosha umma. Hivi ile kesi yenu kwenye Tume ya usuluhishi na Uamuzi (CMA) inaendeleaje ?
 
Shirika la misaada la Uingereza lipo na linafahamika kama Department for International Development (DFID). Kuna error, badala ya DFID niliandika DIDF

Kesi za CMA unazozungumzia hazinihusu, mimi siyo msemaji wa hao wenye kesi, pengine ungewatafuta wahusika ukawauliza. Sikumbuki kama kuna mahali popote kwenye michango yangu kwenye jamvi hili nimeandika huhusu kesi au neno CMA. Nimeandika kuhusu Bodi inayolalamikiwa ambavyo inayolea ufisadi, matumizi mabaya ya ofisi na kufumbia macho malalamiko ya wafanyakazi kuhusu mishahara.

Tumedanganywa sana mpaka tumechoka na kwa kuwa Uongozi hausikii njia pekee ni kuambia umma ufahamu ni nini kipo Chuo cha ufundi Arusha. Huo uchafuzi au upotoshaji unaousemea hapo uko wapi? Kusema kuna ufisadi unaofanywa na wajanja wachache ni upotoshaji? Kama kusema ukweli ni upotoshaji acha umma ujue hivyo kuwa ufisadi ni upotoshaji kwa tafsiri yako.

Badala ya kutafuta fedha za kulipa mishahara ya wafanyakazi mliyokula, badala ya kulipa stahili za wafanyakazi, na badala ya kurudisha mabilioni ya pesa mlizochukua kwa njia ya ufisadi mnataka kuuwa so kwa kuvuta hisia za wananchi kwa chopa? Wananchi waamini kuna kitu kinafanywa na chuo kwamba chopa itarushwa na chuo hivi karibuni? Cha kushangaza, tutadanganya umma kiasi hiki mpaka lini?
 
 
 
Shirika la misaada la Uingereza lipo na linafahamika kama Department for International Development (DFID). Kuna error, badala ya DFID niliandika DIDF

hii inaonanesha kwa jinsi gani ulivyo na Roho Chafu... I can image jinsi povu linakutoka kupotosha umma kuhusu serikali na chuo cha Ufundi Arusha. lakini kumbuka kuwa kuna sheria ya Makosa ya Mtandao Mangi
 
Sijawahi ona mpare akitengeneza helicopter aisee. Hongera mtani ila usikubali kutest. Uta-RIP mtani.
 
It ll be an honor to die for such project,even the choppers you see today have cost peoples life for you to enjoy.mawazo ya watu kama nyie ndio yanatufanya siku zote tuwaze kutengeneza vitu kama spare parts badala ya kufikiria vitu kama hivi.

Moja ya mambo tunayo pungukiwa Afrika Ni kukosa Watu wa aina yako
 
Sijawahi ona mpare akitengeneza helicopter aisee. Hongera mtani ila usikubali kutest. Uta-RIP mtani.

hii inaonesha kwa jinsi gani uwezo wako wakufiri ulivyo mdogo. Mpare kwa ko sio Mtu au Tanzania. ulitaka nani atengeneze hiyo chopper ? pengine ungewajulisha Watanzania ili wajue ! kwa hiyo povu linakutoka kila siku hapa JF kupotosha umma kuhusu serikali na Chuo cha Ufundi Arusha kwa sababu tu anayetengeneza helikopta ni Mtanzania mwenzetu ambaye Kabila lake ni Mpare ?!!
 
Wewe unanunua kesi ambayo haikuhusu. Mpare ni mtani wangu acha kutoka povu.
 
Sijawahi ona mpare akitengeneza helicopter aisee. Hongera mtani ila usikubali kutest. Uta-RIP mtani.
Athee,wana milima thana huko Thame athee,ndio maana wamegundua helikopta athee.
Thatha Raithi anaenda kuchukua wanyalu huko Rwanda,wakati Thame kumejaa nachuro bon thayantithti kibaoo,thi apande hii helikopta akawachukue maIT huko Kihurio jamani!tena kuna yule mtoto wa mthee Mshana pale anajua thana Mathe,kompyuta hatoishindwa athee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…