mkafrend
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 3,047
- 1,503
Wanajf, salaam!!
Mara nyingi nimekuwa nafuatilia mijadala ihusuyo ufisadi - hapa wengi hujielekeza kwenye wizi, utoroshaji au utakatishaji wa fedha na kusahau tabia zingine za kishetani.
Ili kiongozi apambane na ufisadi lazima yeye mwenyewe akubali kukosa Kaka, mama, baba, rafiki, mkabila nk nk nk.
Sababu za mtizamo huo ni kuwa:-
1. Katika hali isiyokuwa ya kawaida ukiletewa tuhuma kuhusu wizi, njama au kufoji vyeti vya taaluma lazima kiongozi bila kujali ukaribu wako na mtuhumiwa uchukuwe hatua kiasi kwamba watu wafahamu kwamba huna ubiya na mtu kwenye uongozi wako,
2. Rushwa katika vyombo vinavyoshughulikia usalama barabarani, uvuvi, nyara na mazao ya misitu bado ni kubwa - hapa fedha huchukuliwa mchana kweupe (huwezi kusikia watu hao wametiwa mbaroni),
3. Mikataba mibovu ya uuzwaji wa nyumba, viwanja na milki za serikali - mikataba ilitaja wazi kuwa kila aliyenunua asiendeleze ujenzi mpk miaka 25 tangu anunue. Pamoja na kuwa watu wengi hawaungi mkono uuzwaji huo lkn bado hakuna utashi wa kisiasa wa kurejesha miundombinu hiyo serikalini (Ifahamike kuwa wananchi kuwatoza michango ya ujenzi wa nyumba za watumishi wakati zilizokuwepo zilichukuliwa na kundi dogo ni kuwakosea heshima),
Kama kuna mtu anayefahamu zaidi ya haya niliyoandika - aongezee kwa madhumuni ya kukumbusha watunga sera kujirekebisha ili kulijengea taifa letu heshima.
3.