Tanzania haimo kwenye nchi 50 zenye amani

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,128
18,733
Huko nyuma Tanzania ilijulikana duniani kama nchi ambayo ilikuwa kisiwa cha amani. Sasa kutokana na matukio mengi ya kuvunjwa kwa haki za binadamu pamoja na migongano ya kisiasa na vitendo vya polisi dhidi ya raia Tanzania haionwi tena kuwa nchi yenye amani.

Badiliko kubwa la kuitoa Tanzania toka kuwa mojawapo ya nchi za amani limetokea katika uongozi wa awamu ya tano. Hivyo serikali ya awamu ya tano ipongezwe kwa kujitahidi kuimarisha uchumi na kumaliza ufisadi, lakini isutwe kwa kuiondoa Tanzania kweye listi ya nchi zenye amani duniani.

Mataifa 50 yanayoongoza kuwa na amani duniani mwaka 2018 ni kama ifuatavyo;

1537790332609.png

Chanzo: Global Finance Magazine - The Most Peaceful Countries In The World 2018
 
Siioni Marekani. Siioni Kenya. Siioni Uganda. Siioni Uingereza. Siioni China.

Botswana pamoja na deni lao naona wamo.
 
Huko nyuma Tanzania ilijulikana duniani kama nchi ambayo ilikuwa kisiwa cha amani. Sasa kutokana na matukio mengi ya kuvunjwa kwa haki za binadamu pamoja na migongano ya kisiasa na vitendo vya polisi dhidi ya raia Tanzania haionwi tena kuwa nchi yenye amani.

Badiliko kubwa la kuitoa Tanzania toka kuwa mojawapo ya nchi za amani limetokea katika uongozi wa awamu ya tano. Hivyo serikali ya awamu ya tano ipongezwe kwa kujitahidi kuimarisha uchumi na kumaliza ufisadi, lakini isutwe kwa kuiondoa Tanzania kweye listi ya nchi zenye amani duniani.

Kwa Afrika nchi zilizomo kwenye listi ni Mauritius, Botswana, Sierra Leone, Madagascar, Ghana, Namibia, Malawi na Zambia.

Mataifa 50 yanayoongoza kuwa na amani duniani mwaka 2018 ni kama ifuatavyo;

View attachment 876351
Mara ya mwisho tz ilikuwa ya ngapi?
 
Mara ya mwisho tz ilikuwa ya ngapi?
Hahaha! ILikuwamo katika nchi 50 zenye amani kabla ya utawala huu. Nchi kama Sierra Leone, Malawi hazikuwamo.

Suala la kujiuliza kama Watanzania ni kwamba, hivi tunapenda sana uchumi ukue na ufisadi ukomeshwe kwa gharama ya kukosa amani nchini? Ndio maana nilisema kwamba ikiwa Magufuli angeweka jitihada kidogo tu ya kuifanya Tanzania kuwa ya amani, kuvumilia siasa za upinzani na kutokuwa mbele kukiuka haki za binadamu, basi angekuwa the best president sio tu Tanzania bali hata Afrika na duniani kwa ujumla. Lakini sasa huyu jamaa pamoja na jitihada kubwa katika ufisadi na uchumi ni kinara wa kuvunja haki za binadamu na demokrasia. Kwa nini? Ni sawa na kama unaoa mke bora sana kwenye kupika na usafi wa ndani, lakini kwenye kulea watoto na mambo mengine ya ndani ndani anakuwa zero kabisa. Huyo ni mke bora? Wengine watsema ndio wengine hapana, mie ninasema hapana. Mke bora ni yule anaejua kubalance kila kitu.
 
Guys ukitaka kujua tanzania ipoje nje nenda malawi ama africa kusini. Watanzania tunaogopwa kama sisi tunavyowaogopa wa nigeria
 
Kuokotwa maiti zisizojulikana mto ruvu, kudungwa risasi hadharani kwa mwanasiasa Tundu Risu na mpaka sasa hakuna taarifa za kushikiliwa mtu kwa makosa hayo kutaiwekaje Tanzania kwenye moja ya nchi zenye amani?
 
Siioni Marekani. Siioni Kenya. Siioni Uganda. Siioni Uingereza. Siioni China.

Botswana pamoja na deni lao naona wamo.

Marekani.- wanaua watu kila siku, polisi wanaua, raia wanaua, wabakaji wanaua, nk
Kenya - kuna El Shabab, kuna mauaji ya wao kwa wao, kuna mauaji ya polisi
Uganda - risasi nje nje hasa ukiwa mpinzani wa Museveni.
Uingereza - japo polisi wao sio wauaji, kuna sualaa terorism kubwa tu, pamoja na uuaji wa mitaani na ubakaji wa watoto, watu kutekwa nk
 
Huko nyuma Tanzania ilijulikana duniani kama nchi ambayo ilikuwa kisiwa cha amani. Sasa kutokana na matukio mengi ya kuvunjwa kwa haki za binadamu pamoja na migongano ya kisiasa na vitendo vya polisi dhidi ya raia Tanzania haionwi tena kuwa nchi yenye amani.

Badiliko kubwa la kuitoa Tanzania toka kuwa mojawapo ya nchi za amani limetokea katika uongozi wa awamu ya tano. Hivyo serikali ya awamu ya tano ipongezwe kwa kujitahidi kuimarisha uchumi na kumaliza ufisadi, lakini isutwe kwa kuiondoa Tanzania kweye listi ya nchi zenye amani duniani.

Kwa Afrika nchi zilizomo kwenye listi ni Mauritius, Botswana, Sierra Leone, Madagascar, Ghana, Namibia, Malawi na Zambia. Tukumbuke kuwa habari kama hizi zinaharibu sana soko la utalii na uwekezaji.

Mataifa 50 yanayoongoza kuwa na amani duniani mwaka 2018 ni kama ifuatavyo;

View attachment 876351

Source: Institute for Economics and Peace (IEP)
Hata USA na Russia siwaoni
 
Back
Top Bottom