Tanzania haijawahi kuwa na Rais mwenye Upendo kama Magufuli. Tumuombee Upendo huu uenee kote nchini

Ni kweli anatembea na fedha nyingi mfukoni akiwapa maskini ila wafanyakazi hataki kusikia shida zao kuwaongeza mishahara yaani bora atumie fedha nyingi kwa ajili ya Chato lakini asiongeze mishahara huu ni upendo wa Agape
Ameanza kwa kuhakikisha watumishi wanapata mishahara na stahiki zao kwa wakati bila longolongo,ikiwemo kuboreshewa mazingira yao ya kazi. Miradi mikubwa itakapokamilika,mishahara itaongezwa zikiwemo ajira, hatuwezi kuelewana sasa,lkn muda ndio utaongea.
nalielewa na kuliamini sana jembe hili.
 
Ni kweli Rais Magufuli ana upendo na katika ziara zake maeneo yote hapa nchini hawezi kupita na kukuta watu wamekusanyika alafu asisimame, ni lazima atasimama na kuzungumza na hao wananchi.

Wananchi watamweleza shida zao na yeye anazitatua hapo hapo,tumeshuhudia baadhi ya maeneo amekuwa akiwachangia fedha cash kutatua matatizo yao katika maeneo mengi.

Rais Magufuli akimwona mtu kwenye TV anamatatizo na anatafuta msaada,kesho yake tu atamtuma Msaidizi wake kwenda kumtafuta mtu mwenye shida na atamkabidhi huo msaada.

Juzi juzi tu tumeona amewasaidia wabunifu waliotengeneza umeme wa maji ambao walionyeshwa kwenye kipindi cha Hadubini cha TBC aliwaita Ikulu na kuagiza wasaidiwe na yeye binafsi aliwasaidia.

Haya ni maeneo machache tu ambayo nimeyataja lakini yapo mambo mengi sana ambayo ameyafanya kusaidia wananchi wa Tanzania,hivyo watanzania tuzidi kumuombea na kumuunga mkono Mhe Rais Magufuli katika jitihada zake za kulikwamua Taifa hili kutoka kwenye umasikini.
 
HAKEMEI UTEKWAJI WATU UTASEMAJE ANA UPENDO???
WANAFUNZI WANABAGULIWA KUPATA MIKOPO
 
Huyu ndo Rais anayetupeleka kwenye Uchumi sahihi kama Nchi,Shida wezi na wapiga deal wote hili hawalikubali kabisa
Tatizo kubwa la awamu hii ukisikia kitu ukweli ni kinyume chake! ukiambiwa wezi, wapiga dili wanabanwa siyo wale wezi au wapiga dili wa mali ya umma, bali ni jamii fulani, kabila, ukanda au hata mtu binafsi asiyecheza ngoma ya mheshimiwa.
 
Kwa upendo wake huo hawezi maliza mwezi akiwa raisi kwa kwenye nchi ya shemeji zetu apo kaskzn ata Zambia tu.raia wao wanajitambua kiasi.sio mazwazwa kama wadanganyika.
 
raisi ana upendo ea dhati sana ila mabwenyenye mafisadi na wale wasio fuata sheria itakula kwao
naomba nitoe mfano mmoja
wakati nipo secondary kuna mwalimu mmoja alikuwa mkali sana alitufuatilia kwa kila jambo mr haule wa malenga sec ulitufanya vijana tukasoma kwa bidii na tulifaulu sana.
magufuli anataka kutengebeza taifa la watu wawajibikaji tuache kulia lia kwenye mtandai
 
Kipindi tupo seminarini tulikuwa tunasema "Kusifu na kuabudu kunawapasa wanyoofu wa moyo"

Ila huku mtaani hali ni tofauti sana.

Watu wa mataifa wanasema
"Kusifu na kuabudu kunawapasa wazee wa kujipendekeza na kujikomba kwa tabibu Pombe."
 
mhola ngosha, nakuombea kwa MUNGU ukamilishe project yako ndipo tutajua
 
Paskali, awamu hii ilikuja na mfumo wa wazi wazi wa kuwagawanya watanzania kutokana na makabila, dini, ukanda wao n.k. Kuna watumishi waliondolewa kwenye nafasi zao simply kwa kuwa wanatoka sehemu fulani ya TZ, wengine hawakuvunjiwa nyumba walizojenge maeneo yasio yao lakini wengine wakavunjiwa bila huruma yoyote. Sasa unapozungumzia upendo wa mkuu kwa watu wake, ni watu gapi hao unaomaniisha?
 
uwe unasoma basi......unatia aibu
 
Hahahaa Pascall bwana unakuwa na heading mbaya sana lakini content ni murua, ni kweli haijawahi tokea nchi hii mwenye upendo kama rais Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…