Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,589
- 1,679
'Tanzania, kutoka kuwa ndovu kuja kuwa kunguni'.
Hakika Tanzania katika ushawishi wa kidiplomasia Afrika, duniani, imekuwa si chochote. Jana, mkataba muhimu wa amani baina ya Ethiopia na wapiganaji wa TPLF wa Tigray ulitiwa saini huko Afrika ya Kusini. Nani alikuwepo huko? Kenya, Afrika Kusini yenyewe na Nigeria!
Siku hizi si ajabu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa nchi kubwa duniani akaamua kutembelea Afrika, akaanza ziara yake Uganda, kisha akaruka kwenda Rwanda, Kenya na kisha kurudi alikotoka!
Tanzania inarukwa tu kama doa jeusi. Kinachonitia wasi wasi ni kwamba kila nikichunguza sioni dalili kwamba jambo hili linawakera walio na dhamana ya diplomasia.
Wasi wasi wangu mkubwa ni kuwa Wizara hiyo, hasa baada ya rais Mkapa, imekuwa , kama nyinginezo, ikikabidhiwa watu kwa misingi ya ukaribu wa kisiasa na hata urafiki binafsi, na si juu ya misingi ya taaluma na uweledi wa kusuka diplomasia na mahusiano.
Najua kuna wale walionyweshwa maji ya uzalendo bandia watakaosema 'ah, acha tujali mambo yetu tu!' Hawa hawafahamu, maskini!
Kuwa diplomasia inachangia katika kila kitu, hata uchumi wa nchi. Tena wakati diplomasia yetu ilipokuwa kilele wakati wa Mwalimu, kulikuwa na faida nyingine kuwa Watanzania walikuwa na uwelewa mkubwa wa mambo ya dunia, kuliko sasa.
Kabla sijamaliza, kwa vile nimefananisha kipindi hiki na cha nyuma, hasa cha Mwalimu, huenda ikadhaiwa ningependa kuona diplomasia ile ile ya kipindi cha Mwalimu. La hasha! Kipindi hicho nimekiishi na nikaona jinsi gani diplomasia ya nje ilikuwa ikichukua muda wote wa siasa zetu, hata kusahahu kutatua matatizo ya ndani.
Kibaya zaidi, ilitumika kwa kuwachagulia wengine jinsi gani waendeshe nchi zao. Tukawa twawaunga mkono 'Wajamaa' akina Mugabe dhidi ya Abel Muzorewa na Nkomo, Neto dhidi ya Holden Roberto, Samora Machel dhidi ya Andre Matsangaisa na Afonso Dhlakama n.k.
Baya zaidi, diplomasia hiyo haikuwa na malengo ya kuleta faida za kiuchumi, isipokuwa kui 'bleed' tu Tanzania.
Hapana! Ninachokikusudia ni kuwa tuwe na diplomasia ya kuitangaza nchi yetu na kuwa shina la utatuzi wa matatizo ya Waafrika wenzetu. Kwa nini hatuanzi kwa kusuluhisha mgogoro wa Rwanda/Uganda, Rwanda/ DRC?
Unapojulikana Kimataifa, inakuwa rahisi pia kuwa na mahusiano ya kiuchumi, kibiashara, kiutalii, kitaaluma, kiutamaduni n.k.