Tanzania Foreign Debt watcher

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,660
1,801
Sasa deni la nje la Tanzania limefikia bilioni 30 USD rasmi. Niliweka thread hapa juu ya hatari ya deni hili, ikang'olewa na mods.
Deni linazidi kwa dola milioni+ kila saa 24. Kwa maana hata mtoto wa mtoto wako anadaiwa!
Sijui kwa nini suala hili halimo katika general discourse ya Tanzania, na maswali kuulizwa kwa nini tumeingia deni kubwa namna hii kwa muda mfupi? Pesa hizi zimetumika katika nini? nani aliyeidhinisha kuchukua deni? Kwa nini bunge halina kauli juu ya kukopa?
Katika miaka ya 80 tulikuwa tunadaiwa bilioni 7 USD zikatushinda kulipa hadi tukasamehewa. It will be interesting to see how can we pay off this debt with accumulating interests.
 
gesi.
 
Hapo mjadala wa deni hilo ni janga. Utaondoka na watu ndipo ujadiriwe.

Chama chetu cha dola hakiruhurusu kutolea majibu maswali magumu kama hayo. Tuombe tu tutakiwe kuwa wavumilivu kwani serikali ya Magufuli imedhamiria kubana matumizi hata ya kulipa hilo deni.
 
Na hii thread inaweza kuondolewa maana wote tunaogopa kujadili kuhusu deni letu maana ni utata mtupu na tukiamua kujadili kuna ambao wataguswa wakati hawatakiwi kuguswa,vumilia tu mpwa wangu mpaka wajukuu zetu waje watutukane.
 
Deni sio tatizo bali hela za mkopo zilitumika kufanyia nini, kwa manufaa ya nani, na walitarajia kulipaje? Sithani tulipewa mikopo bila serikali kujieleza inakwenda kufanyanini na mikakati jinsi ya kuzilipa. Kwani hili deni ni la watanzania wote na vizanzi vijavyo.
 
Na hii thread inaweza kuondolewa maana wote tunaogopa kujadili kuhusu deni letu maana ni utata mtupu na tukiamua kujadili kuna ambao wataguswa wakati hawatakiwi kuguswa,vumilia tu mpwa wangu mpaka wajukuu zetu waje watutukane.
Kwa hiyo hadi mjukuu wangu naye anadaiwa?
 
Sasa deni la nje la Tanzania limefikia bilioni 30 USD rasmi. Niliweka thread hapa juu ya hatari ya deni hili, ikang'olewa na mods.
Deni linazidi kwa dola milioni+ kila saa 24. Kwa maana hata mtoto wa mtoto wako anadaiwa!
Sijui kwa nini suala hili halimo katika general discourse ya Tanzania, na maswali kuulizwa kwa nini tumeingia deni kubwa namna hii kwa muda mfupi? Pesa hizi zimetumika katika nini? nani aliyeidhinisha kuchukua deni? Kwa nini bunge halina kauli juu ya kukopa?
Katika miaka ya 80 tulikuwa tunadaiwa bilioni 7 USD zikatushinda kulipa hadi tukasamehewa. It will be interesting to see how can we pay off this debt with accumulating interests.
Serikali ya Awamu ya Tano (SAT) ifanye yafuatayo kudhibiti kujua kwa deni hili: 1. Ukopaji usimame kwa angalau mwaka mmoja ilikufanya tathimini ya value for money kwa mikopo yote 2. Mikopo yote iidhinishwe na Bunge 3. Kuwe na taasisi ya kuchambua mipoko ya serikali kabla haijawasilishwa bungeni, kufuatilia na kutathimini utumiaji na ulipaji wa mikopo na 4. Kuwe na taarifa ya hali ya deni la taarifa kila mwezi na ipatikane kwa umma kupitia aina zote za mawsiliano
 
Ni muhimu kwa serikali kuchukua hatua za makusudi za kufanya FORENSIC AUDIT ya den la taifa ili kubaini jinsi tulivyoingia kwenye hayo madeni; jinsi mikopo hiyo ilivyotumika na kujiwekea mbinu za kuweza kulipa hayo madeni!! Tathmini hii itatasaidia nchi kugundua mapungufu [ kama yapo] yaliyosababisha nchi kujitwisha mzigo mkubwa kiasi hiki na pia kujua watu waliohusika na kuingiza nchi katika LAANA [ CURSE} hii ya madeni!!
 
hebu naomba mnisaidie wadau hivi katika hilo deni kiasi gani ni deni la ndani na lipi la nje, pia kiasi gani ni deni la muda mrefu na lipi muda mfupi na mwisho lipi ni la kibiashara(commercial loan) na lipi la masharti nafuu maana tukipata huo mchanganuo ndo tutajua maumivu na lini hili deni litakwisha
 
Nakuamini rais Magufuli,huwa husiti kufanya maamuzi magumu pale inapopaswa.Deni la taifa ni msalaba mzito kwa Watz na kwa ukuaji wa uchumi wa taifa letu.Deni si jambo la kulichekea,tunakuomba uiagize TAKUKURU ifanye uchunguzi jinsi fedha hizi za mikopo zilivyotumika na ikibainika kwamba kuna watu walizutumia fedha hizi kinyume na malengo wachukuliwe hatua kali za kisheria,hapa usiangalie sura,wewe wasulubu tu, usiangalie kama waliwahi kuwa viongozi wakubwa wa nchi hii ktk serikali za awamu zilizopita,acha sheria uchukue mkondo wake,na ikiwezekana mali zao zote zifilisiwe ili hizo fedha zitumike kulipia madeni.
 
Kwa hiyo hadi mjukuu wangu naye anadaiwa?
Kwa deni linavyo endelea kukua basi jua wajukuu zetu watatutukana tu kua sisi maboya tumewaingiza shimoni,haiwezekani hatuna uthubutu wa kujua hela tunazokopa zinatusaidiaje tabaka la chini ukiacha nadharia zao.
 
Hapo mjadala wa deni hilo ni janga. Utaondoka na watu ndipo ujadiriwe.

Chama chetu cha dola hakiruhurusu kutolea majibu maswali magumu kama hayo. Tuombe tu tutakiwe kuwa wavumilivu kwani serikali ya Magufuli imedhamiria kubana matumizi hata ya kulipa hilo deni.

Deni la nje halilipwi kwa fedha za madafu, hivyo kukusanya kodi na kubana matumizi ya madafu kamwe hatuwezi kulipa deni la nje
 
Deni la nje halilipwi kwa fedha za madafu, hivyo kukusanya kodi na kubana matumizi ya madafu kamwe hatuwezi kulipa deni la nje

Sawa nusu; kukishakuwa na saving ni rahisi kuzibadiri kwenye hela ya kulilipia. Ni kweli nakumbuka kuna wazir Mrema alitaka mauzo yote ya madini yafanywe Benki Kuu. Tulikusanya dhahabu nyingi sana wakati huo. Ina maana kwa fedha za ndani kama hizo za madini tunaweza kuzitumia kulipa madeni.

Cha msingi siyo pesa kama pesa ila ni nidhamu ya usimamizi wa fedha na kuelekeza kunakolazimika. Deni la nje hakuna aliyejali kulifanyia kazi. Ni kama tabia ya watawala wetu na akili ya omba omba na kutegemea kusamehewa. Siyo kuwa hatuna uwezo wa kulilipa.

Kuna suala zito Zaidi hiyo mikopo imetusaidia nini? Nina uhakika ukiulizia utapewa maelezo mengi yasiyojitosheleza.
 
Watu wanashangaa hili deni limefikaje hapo ? Kwa sababu tunasikia kila siku "Tanzania yapewa msaada wa ......
.. na wafadhili " wanafkiri huo ni msaada wa bure kama wa Mama Theresa, kumbe ni mkopo wenye riba, halafu tunawashukuru kwa kuwaita " Nchi wahisani"..siku wahisani na wafadhili wanapodai chao tunawaita " Wanyonyaji" a.k.a Mabeberu
 
Bali kila sekunde. Fanya mahesabu ikiwa saa 24 linakuwa kwa milioni 1.3 litakuwa kwa dola ngapi kwa sekunde? Ukitaka kujua
Tanzania Economy

google;countrymeter select country then tz economy,...
ni true dohhhhh deni linaongezeka mmmmhhhh hiii si htr
 
Back
Top Bottom