ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,065
- 61,403
TANZANIA imeibuka kinara katika tuzo ya utalii kwa kuonekana ni eneo bora zaidi la utalii duniani kwa mwaka 2018, ‘The Best Destination to the World in the Category of Exotic Destination 2018’ Urusi.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Damas Ndumbaro. Alisema mwaka 2012 hadi 2017, utalii nchini umeongezeka kwa asilimia 200.
Waziri Ndumbaro alisema Tanzania imeshinda tuzo hiyo baada ya kuzibwaga nchini za Cuba na Japan huku vivutio vyake vya Mlima Kilimanjaro na fukwe nzuri za Zanzibar zikichagiza ushindi huo.
“Novemba 21 Tanzania ilifanikiwa kushinda tuzo moja kubwa Urusi; mashindano haya yalianza ngazi mbali mbali kwa njia ya mtandao ‘online’ kwa lugha ya Kirusi. Katika mashindano hayo nchi tatu ziliingia kati hatua ya tatu bora ambapo zilishindanishwa na Tanzania kuibuka kinara.” alisema Alisema Tanzania ilishinda kwa kura 27 ikifuatiwa na Cuba iliyopata kura 19 na Japan kura 17 na kuwa tuzo hiyo imechapishwa kwenye jarida maarufu nchini Urusi la “National Geographic Magazine.
“Tanzania imepata ushindi huo kutokana na kura zilizopigwa kwenye mtandao wa jarida hilo la “National Geographic Magazine” lililoshirikisha wapiga kura 263,000 kwa njia ya mtandao,” alisema Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla alisema hii ni mara ya tatu katika miaka saba tangu mwaka 2011, raia wa Urusi kupitia jarida hilo kuichagua Tanzania kama eneo bora zaidi la utalii.
“Mwaka 2011, Zanzibar ilipata tuzo ya ‘Star Travel’ kama eneo bora zaidi la utalii wa ufukweni Afrika na mwaka jana, Tanzania ilipata tuzo ya NGT na ilishinda nafasi ya pili katika tuzo hiyo katika kundi la eneo bora la utalii duniani… National Geographic Traveller Awards” (NGT Awards) ni tuzo ya kifahari zaidi katika sekta ya utalii Urusi na hutolewa na Jarida la kirusi la “National Geographic Magazine”.
“Mafanikio hayo yanatokana na jitihada za Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wetu Urusi, Wizara za Utalii za Tanzania Bara na Zanzibar na taasisi zote zinazosimamia masuala ya utalii za ndani na nje ya nchi katika kutangaza vivutio vya utalii kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Urusi,” alisema Kigwangalla alisema watalii wanaokuja Tanzania kutoka Urusi wameongezeka mwaka hadi mwaka.
Mfano, idadi hiyo imeongezeka kutoka watalii 4,021 mwaka 2012 hadi watalii 10,060 mwaka 2017. Alisema moja ya vigezo vilivyofanya Tanzania kupata ushindi ni ukarimu wa wananchi wake pamoja na Mlima Kilimanjaro na usafi wa jiji la Moshi na pia fukwe za Bahari ya Hindi uwepo wa amani na utulivu. Katika hatua nyingine, Kigwangalla alisema kuwa serikali imefungua milango kwa nchi tano kwa ajili ya kukuza utalii na tayari wameshaanza matangazo katika nchi ya China kwenye majimbo makubwa matano.
Alisema nchi hizo ni China, Urusi, Israel, Oman na Australia na serikali inaongeza jitihada za kujitangaza ili kukuza utalii nchini na kuanzia Februari 2019, ATCL itaanza safari za Guangzhou kupitia Bangkok. Kwa upande wake, Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Yuri Popov alisema kuwa Tanzania inastahili kupata tuzo hiyo na kwamba haijashinda kwa bahati mbaya kutokana na kusheheni vivutio luluki.
Popov alisema fukwe za bahari ya Hindi visiwani Zanzibar, mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro na hali ya utulivu na ukarimu mkubwa wa watu wa Tanzania ndio umefanyaa Tanzania ishinde tuzo hiyo. “Warusi ni watu hawapendi vurugu, ndio maana wanapenda kukaa kwenye fukwe za Zanzibar zilizotulia, na hili ndilo linalofanya idadi ya Warusi wanaokuja Tanzania kutalii kuongezeka maradufu,”alisema.