Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 2,237
- 4,384
Tanzania dhaifu ni furaha kwa dunia!
Hii ni sababu kuu inayoniogopesha kwamba, itakuwa vigumu (but not impossible) kwa ICC (The Hague), kufungua mashitaka dhidi ya utawala wa Rais Samia Suluhu - na yeye akiwemo. Sababu ya kimaoni juu ya hili, inachagizwa na ustaarabu wa maamuzi ya kidunia, uliosimikwa baada ya vita vya pili vya dunia na ukasakafiwa vema na vita baridi na matokeo yake ambayo bado yana shape geopolitics za ulimwengu wa sasa.
Japo kuna ushahidi usio na shaka wa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu nchini Tanzania, ila kwa narrative ya jicho la kimataifa, bado uvunjifu huu unaonekana kama ni mimba changa, kwa sababu haujapelekea kudhoofika na kushindwa kwa dola kama ilivyo kwa nchi kama Sudan, Syria, Congo n.k ambako ICC wana historia ya kuwafungulia mashitaka viongozi wa hizo nchi.
Lakini kwa upande mwingine, narrative ya dunia ni kwamba, baada ya Oct 29, na uking'ang'anizi wa CCM kuendelea kuongoza dola, ilihali imekataliwa na wananchi, inaashiria kwamba, Tanzania ya kesho na baadae itakithiriwa na mlolongo wa machafuko ambayo yatadhoofisha uchumi kama ilivyoshuhudiwa. Kudhoofika kwa uchumi na kukosekana kwa amani ya kudumu ni matokeo yatayowafurahisha dunia; watashangilia! Ni anguko la Tanzania. Na hao wageni wanaosingiziwa, watakuja kipindi hicho nchi ikiwa kwenye udhoofu na sio sasa. Ni kama ilivyokuwa kwa M23 kule Congo; historia ni mwalimu mzuri.
Hii ina maana gani?
Wenu,
MC

> Tusiwategemee nchi za nje au taasisi za nje kutupatia suluhisho la huu mgogoro. Hii ngoma lazima tuitatue sisi: whether ni kuendeleza maandamano ya amani bila ukomo, sala, au ulozi, au twende kwenye hizo mahakama za CCM kufungua mashauri nchi nzima ya mgogoro wa kikatiba. Huko social media pressure iwe non-stop dhidi ya utawala wa CCM mpaka akili ziwarudie na kuleta mabadiliko.
Wenu,
MC