Tanzania Daima ilitabiri haya

MWAKATA KWETU

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
562
319
GAZETI LA MTANZANIA DAIMA LILISHAWAHI KUANDIKA HAYA
source jamii foram

KWA jinsi lilivyo sasa taifa letu lipo njia panda, sheria hazifuatwi. Kila mmoja wetu aliyeko madarakani anataka ajifanye au afanyiwe lile analolitaka bila kuwaangalia au kuwajali wengine.

Masikini wanazidi kuumia kila siku, lakini nao kwa nafasi zao wameamua kufanya kila wanaloweza ilimradi nao wasiwe nje ya mparaganyiko huu unaoendelea.

Wale wa vijijini na wanaoishi karibu na misitu hawajaachwa nyuma, nao wameamua kuteketeza misitu kwa kuchoma mkaa na kukata kuni! Pia wanaoishi karibu na barabara kuu wamehakikisha wanang'oa alama za barabarani na vyuma vya madaraja. Kila kilicho mbele yao wanaona ni heri waambulie.

Masikini wana hasira kuona maisha yao yanazidi kuwa magumu, na watoto wao wanasoma wakiwa wameketi chini, huku magari ya kifahari yanayotokana na kodi zao yakipita usiku na mchana.

Wanahujumu miundombinu ya umeme kwa kuiba mafuta kwenye transfoma. Wapo wanaowaona wakifanya uhalifu huo, lakini hawajishughulishi kuwazuia. Wanafanya hivyo kwa sababu wanaona wakubwa wanagawana nchi, wanasafiri kadiri wanavyotaka, ilhali wakiwaacha wao wakiwa hoi bin taabani.

Dawa za serikali hasa zinazopaswa kupelekwa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali za umma ndizo zinazouzwa kwenye maduka binafsi yaliyoenea hadi mlangoni mwa zahanati, vituo vya afya na hospitali za umma. Wagonjwa wanajua wanalalamika kwenye uongozi husika, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.

Wauguzi nao kwa kuona madaktari, wafamasia, na wenzao wengine ndio wanaofaidi, nao hawako nyuma. Wameamua kuchukua kila linalowezekana. Pale walipokosa chochote cha kuwafaa, wameamua bila soni kudai rushwa kutoka kwa wagonjwa au ndugu wa wagonjwa wanaowahudumia hospitalini.

Hata wapishi wanaopaswa kuwapikia wagonjwa wasio na uwezo, wamehakikisha ama wanagawana chakula na wagonjwa au wanawakosesha kabisa hata hicho kidogo walichonacho. Wagonjwa sasa wanasaidiwa na wagonjwa wenzao wodini.

Madereva wa magari ya umma ambao wanaona mabosi wao wanavyojitungia safari na kuyatumia kukagua miradi yao binafsi, nao wameelekeza hasira zao kwenye ununuzi wa mafuta na matengenezo ya magari.

Kila wanapokwenda kuweka mafuta madereva hao sharti wawe na yao pembeni. Wameshirikiana na wakubwa wao wa kazi kuhakikisha kuwa karakana za serikali zinakufa ili magari yatengenezwe chini ya miembe! Huko wanajua wanachofaidi.

Kwa miongo kadhaa sasa tunalia kuwa reli zetu zimekufa, kuna habari kwamba barabara zinatumika kusafirisha asilimia zaidi ya 99 ya mizigo yote, huwezi kujenga uchumi imara na kuwapa unafuu wa maisha wananchi kama unatumia mfumo huu.

Kwanini reli hazitengenezwi? Kwanini hatupati reli mpya? Hapa tunaambiwa kuwa nguvu za wakubwa. Sakata lililotokea wiki kadhaa zilizopita la mgomo wa wamiliki wa malori, ni dalili ya wazi kwamba kwa kuwaangukia matajiri hawa, hakuna reli wala treni itakayofanya kazi.

Wenye malori ni matajiri. Wenye malori wengi ni wanasiasa wanaopaswa kuibana serikali ihakikishe wanakuwa na reli. Hapa ndipo ugumu wa mambo unapoanzia. Tunamhitaji kiongozi mwenye roho ngumu kuweza kuweka mambo sawa.

Hatuhitaji ushahidi zaidi ya huu wa kuona leo wazazi wakiungana na wanafunzi kuwapiga walimu. Kupigwa kwa walimu kwa sababu tu ya kusimamia nidhamu ya masomo darasani ni mparaganyiko katika taifa.

Pia, kwanini walimu wasipigwe kama wao ndio hao wanaoongoza kuwatia mimba watoto wa kike? Ni majuzi tu tumesoma habari za mwalimu aliyekamatwa akiuza bangi shuleni! Haya yote yanalifanya taifa letu liwe njia panda.

Tuna wanafunzi wanaopiga walimu, lakini pia tuna walimu wanaowatia mimba wanafunzi.

Katika magazeti mengi siku hizi huwa kuna habari ya maofisa wanyamapori wanaoshiriki ujangili. Hawa wamepewa bunduki na risasi ili wawalinde wanyamapori ambao ni chanzo kikuu cha mapato katika nchi yetu. Ndovu, nyati, simba na wanyamapori wengine ambao wangependa wakimbilie kupata hifadhi kwa walinzi hao, sasa waende wapi?

Fikiria, watu wamepewa bunduki na risasi kuwakabili majangili, lakini sasa wameamua kushirikiana na majangili na kwa kutumia bunduki na risasi hizo hizo za kuwalinda, wanawaua wanyama wasio na mtetezi.

Tunahangaika kusaka majangili ndani na nje ya hifadhi ya mbuga, kumbe majangili wakuu ndio hao walioaminiwa na serikali.

Polisi ambao kimsingi mwananchi mzalendo anapaswa kuwakimbilia kuomba hifadhi, leo inaonekana wamekuwa ndio wahalifu wakuu. Tena wapo wanaodai kuwa heri ukutane na jambazi mtaani kuliko polisi kituoni! Wamedaiwa kuwa watesaji na washirika wakuu wa uhalifu.

Polisi wanadaiwa kuwa ndio wachora ramani za uhalifu. Ndio wanaowaelekeza wahalifu mahali zilipo fedha. Wanapoitwa kwenye tukio la ujambazi hawahangaiki kuokoa roho na mali za wananchi, bali wanachoangalia ni mifuko ya fedha zilizoporwa, wanaondoka nayo na kwenda kugawana.

Polisi wamekuwa ndio wataalamu wa kuharibu kesi. Wamekuwa walimu wa wahalifu wakiendesha mafunzo ya kuwawezesha kujinasua kutoka kwenye kesi. Wanasaidia kuharibu ushahidi na mwisho wa siku lawama zinaelekezwa kwa mahakimu na majaji.

Katika nchi ambayo unakuwa na polisi wanaotumia mafuvu ya watu kama vyanzo vya mapato, ujue hali sio shwari. Tunahitaji mabadiliko ya kweli ya kuondoa na hatimaye kumaliza kadhia hii.

Na kweli haishangazi sasa kuwaona polisi wakitaka mlalamikaji ndiye awe mtunzaji wa mtuhumiwa! Yaani mtu aibiwe, amkamate mtuhumiwa halafu huyo aliyeibiwa atakiwe kumhudumia kwa chakula, sabuni na mambo mengine huyu aliyekamatwa.

Mambo haya yanaweza kuonekana kuwa ni madogo, lakini ndiyo yanayochochea baadhi ya walalamikaji waone njia rahisi ya kupata haki ni kujichukulia sheria mkononi- maana haiwezekani mwenye tatizo ndiye tena aingizwe matatizoni kwa kumhudumia aliyesababisha matatizo.

Tunapaswa kujitazama upya kuona kama kweli huu mwenendo wa polisi kudaiwa kugeuka na kuwa waporaji utatufikisha tunakotaka. Walinzi wa amani wanapojigeuza na kuwa maadui wakuu wa hiyo amani, lazima tutafute njia ya kurejea kwenye mstari.

Mahakama zetu zina matatizo makubwa. Yapo matatizo yanayotokana na bajeti ya nchi, lakini mengine pia ni ya kutengenezwa. Tunao mahakimu na majaji wanaofanya kazi katika mazingira magumu, lakini ni watenda haki.

Lakini pia wapo wasiotenda haki. Hao wanalalamikiwa na kwa kweli wanachangia kuwafanya wananchi waishukie serikali.

Tunahitaji mabadiliko makubwa miongoni mwa viongozi na watumishi wa umma. Tuondokane na hii tabia ya kuona kuwa kutenda haki ni jambo la hisani. Haki itendwe bila kujali hali ya mtu.

Je, haya yatamalizwa na katiba mpya ijayo? Naweza kusema kwa kujiamini kabisa kuwa haya hayatamalizwa na katiba mpya kama baadhi yetu wanavyoamini. Wapo wanaodhani kuwa kwa ujio wa katiba hiyo basi kila kitu kitakwenda sawa. Tunajidanganya!

Tatizo la nchi yetu kwa sasa ni mfumo. Kama katiba mpya itasaidia kuufumua mfumo huu wa sasa, hilo litakuwa jambo jema na kwa kweli hiyo katiba itakuwa imekidhi kiu ya wengi.

Mfumo wa sasa hauruhusu watenda makosa kupata adhabu wanayostahili. Kuna mlolongo mrefu wa kumwadhibu mtumishi wa umma aliyefanya makosa. Kuna waziri mmoja wa zamani alipata kusema kuwa mfumo tulionao unakwamisha mambo mengi serikalini.

Akatoa mfano kuwa kama dereva ataamua kumpiga waziri, kiongozi huyo hatakuwa na uwezo wa kumwondoa mtumishi aliyekamatwa na mali ya wizi wa vifaa vya ofisi, ni kazi ngumu.

Waziri huyo akasema hata kwenye mlolongo wa utendaji wa kazi serikalini, waziri anakuwa hana mamlaka ya kumbana katibu mkuu, mkurugenzi wa wateule wengine. Kwanini hawezi? Hawezi kwa sababu wote ni wateule wa rais.

Mkuu wa wilaya anakuwa mbabe mbele ya mkuu wa mkoa kwa sababu wote ni wateule wa rais. Hakuna nidhamu. Hapo ndipo unapokuta mkurugenzi hamheshimu katibu mkuu, katibu mkuu naye hatii maelekezo ya naibu waziri, na naibu waziri hatii neno la waziri. Hakuna utii kwa sababu wote ni wateule wa rais.

Katiba mpya pamoja na kuainisha mambo mengi ya nchi, inapaswa itoe nguvu ya kikatiba za kubadili mfumo mbovu tulionao sasa.

Waziri fulani na wananchi kadha wa kadha walipata kumwomba Rais Jakaya Kikwete aongeze ukali. Wapo wanaosema hilo amelitekeleza, lakini wapo wanaosema hajafanikiwa.

Wapo wanaoamini kuwa rais ajaye anapaswa kuwa mkali. Anapaswa kufumua mfumo huu tulionao sasa ambao ni mfumo wa kulea maovu.

Tunapaswa kuwa na serikali inayoheshimiwa, lakini inayoogopwa pia. Heshima inapaswa ianzie kwenye woga. Mataifa yaliyoendelea wananchi wake wengi wanaheshimu sheria. Heshima yao kwa sheria imetokana na kuogopa sheria. Wanajua kuvunja sheria sio jambo la mchezo.

Katika nchi zilizoendelea kama Marekani, hata dereva anayeendesha gari anajua asipoheshimu na kuogopa sheria, akinyang'aywa leseni ataaibika na hatapewa tena maisha yake yote. Hapa kwetu dereva wa basi akiua wanadamu 50 bado ataendelea kuendesha mabasi! Hakuna woga. Na serikali iliyo dhaifu inaona kuwa ni sawa.

Tanzania kwa kadiri hali ilivyo sasa, tunahitaji kuwa na rais dikteta, lakini anayeweza kurejesha hali ya mambo kwenye mstari. Tunamhitaji rais atakayejitoa mhanga kuleta mapinduzi ya mabadiliko, rais asiyeogopa watu na asiye mbabaishaji katika mambo yanayohusu nchi. Rais mjasiri na mzalendo zaidi ya uzalendo ambaye ukimtazama tu usoni anamaanisha hivyo.

Tulipo sasa ni bapaya mno. Tukiendelea hivi nchi itakuwa ya wababe watakaofanya lolote na popote bila woga, wasiohurumia wanyonge na wanaoangalia zaidi maslahi yao binafsi.

Source: Tanzania Daima
 
Tanzania Daima si linamilikiwa na hawa jamaa ?
tapatalk_1517147263460.jpeg
 
Mkuu ,hapa watapita tu,hawawezi kula haya matapishi
 
Back
Top Bottom