Tanzania Daima acheni upotoshaji, siyo kila orodha ni ya vyeti feki

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,600
3,651
Nimefuatilia uandishi wa gazeti la Tanzania Daima, kwakweli unatia kichefuchefu kwenye hili suala la uhakiki wa vyeti vya form 4 na 6.

Wao Tanzania Daima kila orodha wanaipa HEADING YA VYETI FEKI.

Nakumbuka siku iliyotilewa hiyo Report na Waziri Kairuki kwa Mh Rais alieleza vizuri sana.

1. Kundi la kwanza VYETI FEKI ( Watumishi zaidi ya 9000)
2. Kundi la pili VYETI VYENYE UTATA (Cheti kimoja kinaonekana kutumiwa na watu wawili au zaidi) hapa wapo watumishi 1500. Hawa wana vyeti Halali ila vimegongana.
3. Kundi la tatu INCOMPLETE ( hawa ni wale ambao uhakiki wao haujakamilika)

Kila kundi lina maagizo yake tofauti.
1. Kundi la Kwanza, Hawa wanatakiwa kujiondoa kazini na kama hawaja ridhishwa na uhakiki huo wakate RUFAA.
2. Kundi la pili; hawa wanatakiwa kwenda NECTA na vyeti vyao ORIGINAL ili kumjua mmiliki halali wa vyeti hivyo.
3. Kundi la tatu, hawa wanatakiwa kukamilisha uhakiki wao.
Sasa ndugu zangu TANZANIA DAIMA nani iyewaambia kila orodha ni VYETI FEKI?

****************************
NUKUU SIKU RIPOTI ILIPOTOKA
"Zoezi hili halikuhusisha Viongozi wa Kisiasa wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa/Wilaya na Madiwani ambao wanatakiwa kujua kusoma na kuandika tu!
Ripoti hii inaonesha kuwa tayari watumishi wa Umma 400035 wamehakikiwa.
Matokeo ya uhakiki yamegawanyika kwenye makundi manne:
1. 376969 sawa na 94.23% wana vyeti halali. Baraza limehakikisha kuwa magamba ya vyeti vilivyohakikiwa vilitolewa na NECTA na taarifa zao zinaendana na zilizopo kwenye vyeti.
2. 9932 sawa na 2.4% wamebainika kuwa na vyeti vya kughushi. Vyeti vyao havifanani na vinavyotolewa na NECTA.
3. Vyeti 1538 vinatumika na zaidi ya mtumishi mmoja ambayo ni sawa na 0.3% ya vyeti vilivyohakikiwa. Hawa tunasema wana vyeti vyenye utata.
4. 11569 waliwasilisha vyeti pungufu. Hawa waliambatanisha vyeti vya utaalamu kama udaktari au ualimu pekee bila vyeti vya kidato cha nne wala cha sita.
Kwa mujibu wa kanuni ya adhabu, adhabu ya mtu aliyefanya kosa la kughushi cheti ni kifungo Jela miaka 7.
Waziri Kairuki amekabidhi ripoti na boksi lenye majina ya watumishi na taarifa zao kamili kama wako wapi na wanapatikana wapi."
 
Nimefuatilia uandishi wa gazeti la Tanzania Daima, kwakweli unatia kichefuchefu kwenye hili suala la uhakiki wa vyeti vya form 4 na 6.
Wao Tanzania Daima kila orodha wanaipa HEADING YA VYETI FEKI.
Nakumbuka siku iliyotilewa hiyo Report na Waziri Kairuki kwa Mh Rais alieleza vizuri sana.
1. Kundi la kwanza VYETI FEKI ( Watumishi zaidi ya 9000)
2. Kundi la pili VYETI VYENYE UTATA (Cheti kimoja kinaonekana kutumiwa na watu wawili au zaidi) hapa wapo watumishi 1500. Hawa wana vyeti Halali ila vimegongana.
3. Kundi la tatu INCOMPLETE ( hawa ni wale ambao uhakiki wao haujakamilika)
Kila kundi lina maagizo yake tofauti.
1. Kundi la Kwanza, Hawa wanatakiwa kujiondoa kazini na kama hawaja ridhishwa na uhakiki huo wakate RUFAA.
2. Kundi la pili; hawa wanatakiwa kwenda NECTA na vyeti vyao ORIGINAL ili kumjua mmiliki halali wa vyeti hivyo.
3. Kundi la tatu, hawa wanatakiwa kukamilisha uhakiki wao.
Sasa ndugu zangu TANZANIA DAIMA nani iyewaambia kila orodha ni VYETI FEKI?
Define fake first, then apply your facts to the definition!
 
Wewe ni muandishi gani usiyeelewa maana ya Feki?
Mtamtia hasara DJ Mbowe.

FAKE= Not Genuine, COUNTERFEIT
Avoid being mechanical when presenting your arguments! We are not discussing Mbowe. Anyway, You need to agree on the definition of terms before making any attempt to construct any syllogism.
Kwaheri tunapishana sana tafuta size yako
 
Almost ambao hawajapeleka vyeti,wengi walifoji wengine washaacha kazi na hapo wameandikiwa incomplete.
Kama mtu aliacha kazi jina lake haliwezi kuwa hapo.
Hapo kuna jamaa zangu 12 wana vyeti vyote lakini ameandikiwa incomplete.

Ukiibiwa cheti unatakiwa kuwa na Police Lost Report halafu unaendanayo NECTA., toka lini mtu akaibiwa cheti Original halafu akakaa Kimya?

Hata ukienda na loss report jamaa wa NECTA hawatoi original, wanakuambia wao wanacertify basi kupitia mwajiri wako.
 
Avoid being mechanical when presenting your arguments! We are not discussing Mbowe. Anyway, You need to agree on the definition of terms before making any attempt to construct any syllogism.
Kwaheri tunapishana sana tafuta size yako
Mbona ume panic? Jifunzeni Uandishi wenye weledi. Mkubali tu kuwa mmetokota kwenye uandishi
 
Kama mtu aliacha kazi jina lake haliwezi kuwa hapo.
Hapo kuna jamaa zangu 12 wana vyeti vyote lakini ameandikiwa
Mtu anaacha kazi baada ya kuwasilisha vyeti pungufu,maana anajijua stuation yake.Jina lazima lirudi as alishawakilisha vyeti pungufu.
 
Siyo kweli, nawajuwa watu walikabidhi vyeti vyote, sema kuna uzembe mkubwa wa MAAFISA UTUMISHI kwenye hili zoezi.
Ulikuwa nao wakati wanakabidhi vyeti vyote?Au wamekuambia tu,thubutu ulifikiri watakuambia kuwa walikabidhi vyeti pungufu?hili jambo ni la aibu,watu wengi wana vyeti feki na waliogopa kuviwasilisha.
 
Mtu anaacha kazi baada ya kuwasilisha vyeti pungufu,maana anajijua stuation yake.Jina lazima lirudi as alishawakilisha vyeti pungufu.
Nakubaliana na wewe kama jamaa aliwasilisha halafu akakimbia, lakini hao jamaa zangu 12 wapo na vyeti vyao hawajakimbia lakini ndio incomplete
 
Nakubaliana na wewe kama jamaa aliwasilisha halafu akakimbia, lakini hao jamaa zangu 12 wapo na vyeti vyao hawajakimbia lakini ndio incomplete
HR's hawakwepi lawama katika zoezi hili...wengi wa ma HR uwezo wao wakutenda kazi kwa weledi ni mdogo
 
Back
Top Bottom