Tanzania, China zaimarisha Ushirikiano: TAZARA na Biashara Vyapewa Kipaumbele

Tanzania, China zaimarisha Ushirikiano: TAZARA na Biashara Vyapewa Kipaumbele

Makumbele

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2009
Posts
239
Reaction score
1,056
DAR ES SALAAM – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amefanya mazungumzo muhimu na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mheshimiwa Wang Yi, Ikulu jijini Dar es Salaam, huku pande zote mbili zikisisitiza azma ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kuboresha miundombinu.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Januari 10, 2026, ajenda kuu ilikuwa ni ufufuliaji wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), ambayo inatajwa kama alama ya urafiki wa muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili.

Rais Samia ameeleza dhamira ya dhati ya Tanzania kufufua na kuimarisha uendeshaji wa reli hiyo. Lengo kuu ni kukuza shughuli za kiuchumi zinazotegemea usafiri huo na kuongeza mchango wake katika maendeleo ya kikanda.

"Tuna dhamira ya kuendeleza ushirikiano wa kimkakati wa muda mrefu na China. Tunahitaji kupanua wigo wa mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la China na kuboresha mizania ya biashara," alisisitiza Rais Samia.

Kwa upande wake, Waziri Wang Yi amesema Serikali ya China ipo tayari kusaidia maboresho ya reli ya TAZARA ili kuleta ufanisi utakaochangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi. Alimhakikishia Rais Samia kuwa China itaendelea kuwa mshirika muhimu katika miradi ya kipaumbele nchini.

"TAZARA ni alama muhimu ya historia ya urafiki wetu. China inaunga mkono jitihada za maendeleo za Tanzania na tutasaidia katika sekta za miundombinu, maji, nishati safi ya kupikia, pamoja na kutoa mikopo nafuu na misaada ya maendeleo," alisema Waziri Wang Yi.

Takwimu za Uchumi Zazidi Kupaa

Mazungumzo hayo yanakuja wakati ambapo uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili unazidi kuimarika. Takwimu zinaonesha kuwa thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) nchini Tanzania imefikia dola za Marekani bilioni 1.7 katika mwaka uliopita.

Aidha, biashara kati ya Tanzania na China imekua kwa kasi, ambapo mauzo ya bidhaa za Tanzania kwenda China yameongezeka kwa takribani asilimia 85 kati ya mwaka 2020 na 2025. Hata hivyo, uagizaji wa bidhaa kutoka China nao umeongezeka kwa asilimia 120, hali inayochochea msukumo wa Rais Samia wa kutaka kuboresha mizania ya biashara kwa kuuza bidhaa zaidi nchini China.

Viongozi hao wamehitimisha mazungumzo yao kwa kuthibitisha dhamira ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano wa kimataifa na wa pande nyingi kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na China.
 
Tunashukuru kwa ajili ya TAZARA. Lakoni pia tunaomba Huyo mheshimiwa wa China atusaidie na SGR ifike Rwanda please
 
Nampongeza sana rais mama samia kwa kunyakua ushindi wa tyrant of the year
 
Back
Top Bottom