Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

Aug 15, 2011
30
11
Tanzania imeweka rekodi ya aina yake baada ya vivutio yake vyote vitatu vilivyoingia katika shindano la kutafuta Maajabu Saba ya Asili Barani Afrika kushinda na kuingia katika orodha ya Maajabu Saba ya Asili Barani Afrika.

Aidha hifadhi ya Taifa ya Serengeti kimetajwa kuwa ni kivutio pekee kilichopigiwa kura nyingi zaidi miongoni mwa vivutio vyote vya Afrika vilivyoshindanishwa katika shindano hilo.

Akitangaza vivutio vilivyoshinda na kuingia katika orodha ya Maajabu mapya Saba ya Afrika katika sherehe zilizofanyika katika Hotel ya Mt. Meru jijini Arusha na kuhudhuriwa na watu mbali mbali mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchini wakiwemo wabunge, mabalozi na mawaziri, Rais wa taasisi ya Kimataifa ya Seven Natural Wonders yenye makao yake nchini Marekani Dr. Phillip Imler amesema ushindi wa Tanzania ni wa kishindo na imeweka rekodi ya aina yake kwa vivutio vyake vyote kuingia katika orodha hiyo ya Maajabu Saba ya Asili ya Afrika.

Dr. Imler amevitaja vivutio vingine vilivyo shinda kuwa ni pamoja Red sea reef kutoka Misri, Mto Nile wa Uganda, Delta ya Okava ngo ya Bostwana na Jangwa la Sahara lililoko kaskazini mwa Afrika
Kwa upande wake mgeni rasmi katika sherehe hizo za Utangazaji wa maajabu hayo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.

Mizengo Pinda amesema vivutio vya Tanzania vilistahili kushinda kwani pamoja na upekee wa vivutio hivyo lakini ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania inafanya vizuri sana katika kuhakikisha utalii unakuwa endelevu kwa kuhifadhi mazingira yanayozunguka maliasili zake zake na ndiyo maana ripoti ya Word Economic Forum inaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya pili duniani baada ya Brazil kwa uhifadhi wa mazingira asilia, maeneo mengi ya asili ambayo ni urithi wa dunia na maeneo mengi yanayohifadhiwa ambapo takribani asilimia 28 ya ardhi ya Tanzania ni eneo linalohifadhiwa.

Mchakato wakutafuta vivutio Saba vya Bara la Afrika ulianza mwaka 2008 kwa kuhusisha vivutio kumi na mbili (12) ambapo watu mbalimbali kote duniani walipiga kura sambamba na kura za wataalaamu UNESCO na wa Taasisi ya Kimataifa ya Uhidhafi wa Mazingira ya IUCN.

=======
Vivutio vya Tanzania ni vingi sana, kama vile milima (kwa mfano mlima Kilimanjaro, milima ya Usambara, milima ya Udzungwa), pia mbuga za wanyama (kama Mikumi, Serengeti, Ngorongoro na Manyara), tena maporomoko ya maji ya mto Ruaha na mengineyo.

Faida za kutembelea vivutio vya ndani
Je, mara yako ya mwisho kusafiri sehemu ngeni ilikuwa lini? Uliposafiri, huenda ulihisi kwamba ulihitaji kupumzika na kusahau taabu za kila siku? Je, umewahi kwenda likizo katika maeneo yoyote ya vivutio? Fikiria karne moja hivi iliyopita, watu wengi duniani hawakuwa wakipata nafasi ya kusafiri au kwenda mapumziko kama ilivyo sasa.

Walikaa karibu na kwao maisha yao yote bila kutembelea maeneo ya mbali. Kusafiri nchi za mbali kwa namna yoyote ile ikiwemo kupumzisha akili au kujielimisha lilikuwa jambo gumu na ni watu wachache tu, hasa matajiri au wafanyabiashara waliopenda kusafiri ndio waliweza kufanya hivyo. Lakini siku hizi mambo yamerahisishwa zaidi, mamia kwa maelfu ya watu wanasafiri kokote wanakotaka katika nchi yao au hata nchi nyingine, hasa kwa safari za kitalii.

Ripoti moja ya Shirika la Utalii Ulimwenguni inasema hivi: ‘Utalii huingiza fedha nyingi za kigeni ambazo ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi nyingi.” Inasema: “Mwaka 1996, utalii wa kimataifa ulichuma fedha za kigeni zenye thamani ya Dola bilioni 423 za Marekani. Mapato hayo yalikuwa zaidi ya yale yaliyochumwa kwa kuuza mafuta, magari, vyombo vya mawasiliano, nguo, na kadhalika, katika nchi nyingine.”

Ripoti inaenda mbali na kusema:: “Utalii ndiyo biashara inayostawi zaidi ulimwenguni,” na ilitokeza ‘asilimia 10 ya jumla ya pato la nchi zote ulimwenguni.’ Nadhani kila mmoja atakubaliana nami kuwa kutembelea maeneo ya vivutio kuna faida kubwa, japokuwa suala la kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio halijazoeleka sana kwa Watanzania na Waafrika kama ilivyo kwa Wazungu.

Kusafiri siyo lazima kwenda nchi nyingine, bali hata safari za ndani ya nchi au ndani ya eneo lako unaloishi zina maana kubwa, hasa kama zitafanywa kwa lengo la kujifunza. Unapofunga safari ya kutembelea vivutio na maajabu ni njia nzuri ya kuona fursa zilizoko kwenye eneo fulani unazoweza kuzifanyia kazi na ukajipatia kipato au ukaongeza kipato chako. Utalii una faida kubwa na hufaidisha pande zote. Wewe kama mtalii, unapotembelea vivutio au maajabu nchini kwako au hata katika nchi ya kigeni, utaburudika sana na kuelimika.

Tanzania tunayo maeneo muhimu kwa utalii kama: hifadhi za taifa, mapori ya akiba, fukwe za bahari, maeneo ya kihistoria, milima, maziwa n.k. Unaposafiri unajifunza mambo mbalimbali ambayo isingekuwa rahisi kujifunza ukiwa nyumbani. Utajifunza jiografia, utamaduni au hata mtindo wa maisha wa watu wa eneo unalotembelea.

Si ushamba kutembelea maeneo ya vivutio katika nchi yako na kujifunza huko, kwani inasemwa kuwa kutembea umbali wa maili moja ni bora kuliko kukaa sehemu moja bila jambo muhimu hivyo, kutembla maeneo mbalimbali ni shule nzuri ya kuongeza maarifa. Ifahamike wazi zaidi kuwa, nchi zinazowahudumia watalii hujipatia fedha nyingi za kigeni, kwa kuwa nchi yoyote huhitaji fedha za kigeni ili kulipia huduma na bidhaa zinazotoka katika nchi nyingine. Kwa hiyo, unaposafiri unaweza kuboresha maisha ya watu wengine wa eneo ulilotembelea kwa njia moja au nyingine.

Fikiria vyombo vya usafiri unavyotumia safarini, hoteli utakazolala, viingilio utakavyolipa na kadhalika. Hivi vyote vinawapa kipato watu wengine na kuboresha maisha yao, hivyo, safari yako haikunufaishi wewe peke yako, bali hata watu wengine wanaohusika au kuhusishwa kwenye safari yako. Unaposafiri pia unapata marafiki mbalimbali watanaotokana na watu uliokutana nao safarini. Wapo baadhi ya watu waliowahi kupata wenza wa maisha kutokana na kusafiri; hivyo faida hii ya kusafiri haiwezi kuachwa nyuma.

Karibu kundi kubwa la watu, pengine nawe ni mmoja wao, wamewahi kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa malengo tofauti tofauti likiwamo la kuburudika, hata hivyo, moja ya safari nzuri katika safari hizo ni yenye kusudi la utalii. Utalii ni jambo linalopaswa kupendwa na kila mtu anayethamini uumbaji wa Mungu, kwa kuwa ni Mungu aliyewawekea wanadamu mazingira ya kuvutia na kustaajabisha ili tuweze kujifunza kupitia uumbaji wake.

Tanzania ni moja ya nchi zilizobarikiwa kuwa na maeneo ya kipekee katika nchi nyingi zenye utajiri wa maeneo ya vivutio, wanyamapori, milima, maziwa na hata historia katika makumbusho. Vivutio hivi ni utajiri mkubwa wa kujivunia na kila Mtanzania anapaswa kuiona thamani ya kuujali kwa kutembelea maeneo haya kujifunza na pia kuburudika.

Haipendezi kuona watu kutoka nchi za ughaibuni wakija kutalii maeneo haya ambayo sisi tumekuwa tukiyatazama tu pasipo kupata muda wa kwenda kujifunza huko. Yapo maneno ya asili na yenye kuvutia sana ambayo kama hujawahi kutembelea ni vyema ukajitahidi kutafuta nafasi ili kutembelea japo eneo moja au mawili, kwani utajifunza mengi s ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa kufikiri. Maeneo hayo ni pamoja na Msitu wa Nyumbanitu wenye kuku wa ajabu mkoani Njombe, Bwawa la Mto Nyange lenye viboko wanaocheka na mapango ya Kipatimo wilayani Kilwa, Hifadhi ya Gombe yenye sokwe wanaoishi kama binadamu mkoani Kigoma, eneo la Snake Park huko Monduli- Arusha, na Bonde la Ngorongoro ambalo ndiyo kitovu cha binadamu.

Maeneo mengine ni Maporomoko ya Maji ya Mto Ruaha, Mapango ya Amboni mkoani Tanga, eneo la Kondoa Irangi mkoani Dodoma, shimo la ajabu lijulikanalo kama Shimo la Mungu wilayani Newala, mchanga unaohama bila upepo huko Ngorongoro. Pia tunayo milima kama Kilimanjaro, Milima ya Usambara, Uluguru, Udzungwa, Oldonyo Lengai n.k. mbuga za wanyama kama Mikumi, Serengeti, Ngorongoro, Manyara, Selous, Katavi, na maeneo yenye historia kama Kilwa Kisiwani, Bagamoyo, Zanzibar na kadhalika.

Utajiri huu wa uwepo wa vivutio hivi na vingine vingi licha ya kuiingizia nchi mapato makubwa, pia ni maeneo yenye fursa kubwa na yanayofaa kutunzwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vinavyokuja. Haya yanapaswa kutunzwa na kutumiwa ipasavyo kwa kutembelewa ili neema iliyo ndani ya urithi huu, iwanufaishe watanzania hasa kwa kupanua uelewa wao wa mambo na kuburudika. Haya, yanapaswa kutunzwa kwa kutunza na kutoharibu mazingira na ma;liasili zake. Hivyo, kusafiri na kwenda kujionea vivutio mbalimbali ndani ya nchi ni burudani ya aina yake, hasa kama unasafiri kwenda kwenye eneo sahihi.

Unaposafiri hutaacha kujifunza, kupata burudani bora na ya kipekee na faida nyingine lukuki. Uwapo safarini unaweza kuona vitu vya kuvutia kama vile mazingira ya asili (mito, milima, mabonde, n.k.), wanyama pamoja na sanaa za eneo husika kama vile ngoma, maigizo, mavazi ya kitamaduni na kadhalika.

Ni ukweli usiopingika kuwa, Wazungu wanafahamu vyema umuhimu wa safari za kitalii, ndiyo maana wako tayari kulipa gharama kubwa ili watimize lengo hilo. Kimsingi, kutembelea vivutio humfanya mtu kuburudika na kufurahi, na tunapofurahi tutakuwa tumejiongezea siku za kuishi huku tukichochea utunzaji na ukuaji wa uchumi wa nchi.

1584084778703.png

Mlilima Kilimanjaro
1584084868639.png

Milima ya Usambara
1584084976534.png

Milima ya Udzungwa
1584085216760.png

Mbuga za wanyama

Pia unaweza soma vivutio zaidi hapa
Uzi wa Matembezi (Travel & Vacations) na Vivutio vya Utalii nchini Tanzania

Michango ya wadau
View attachment 421962

View attachment 421964

View attachment 421965

Kwa miaka mingi sasa sekta ya utalii nchini imeshindwa kuchangia pato la taifa kama inavyostahili. Kuna changamoto nyingi sana ambazo zimesababisha jambo hilo lakini naomba nitaje chache kisha na wenzangu mnaweza kuchangia na kuishauri serikali hatua za kuchukua ili kuimarisha sekta hii muhimu kwa ustawi wa uchumi wetu.

1. Sekta hii haijatangazwa ipasavyo ndani na nje ya nchi na serikali

2. Sekta hii imekumbatiwa na watu wachache na kupitia umoja wao wameifanya sekta hii kuwa kama mali yao binafsi na ni wao wanaoishauri serikali kuweka masharti magumu ili kuendelea kunufaika wao peke yao.

3. Kuna masharti magumu yanayokwaza wafanyabiashara wadogo kuingia kwenye sekta hii na hivyo kunufaisha wadau wachache

4. Miundo mbinu katika hifadhi zetu ni kikwazo katika kukuza biashara hii ya utalii

5. Vyuo vyetu vya utalii ni vichache vinatoa mafunzo duni yasiyoendana na ukuaji wa sekta hii na wahitimu wengi wanaomaliza kusoma wanakuwa na uwezo wa kufanya kazi za chini na zile nafasi kubwa kushikwa na wageni

6. Kutokuwepo kwa vivutio na mahoteli makubwa katika miji mikuu yenye hadhi ambayo ipo jirani na mbuga zetu za wanyama

7. Kutokuwepo au kutoboreshwa kwa maeneo yenye historia ya miji mbalimbali hapa nchini

8. Maonyesho ya utalii kutopewa kipaumbele na kufanywa katika mikoa miwili tu Kilimanjaro na Arusha

9. Kutokuwepo kwa taarifa za mara kwa mara kuhusu takwimu za watalii wanaoingia nchini na nchi wanazotoka zaidi ya kupatikana kwenye hotuba za waziri bungeni.

10. Ushiriki mdogo wa maonyesho ya utalii nje ambapo serikali haisaidii kuwawezesha wafanyabishara wadogo wa utalii kushiriki maonyesho haya

Nini kifanyike:

1. Serikali ijikite kwa nguvu zote kutangaza utalii katika mataifa mbalimbali ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea nchi zetu. Juhudi hizi ziende sambamba na kutoa mialiko maalum kwa watu maarufu duniani kutembelea vivutio vyetu na serikali kuchangia baadhi ya gharama na ziara hizo ziwekwe mwenye vyombo vya habari vya hapa nchini na nje.

2. Kuna fukuto la mgawanyiko katika umoja wa wafanyabiashara ya utalii kati ya wale wafanyabiashara wakubwa na wale wadogo. Na mgawanyiko huu unatokana na wafanyabishara wakubwa kutetea maslahi yao zaidi na kuwaacha wafanya bishara wadogo wakikosa pumzi. Serikali inatakiwa kutengeneza mazingira yatakayowawezesha wafanyabishara wa utalii kuwa na mazingira mazuri ya kufanya bishara zao bila kujali uwezo wao wa kimtaji, lakini pia kuwe na utaratibu wa kuwatambua wafanyabishara wanaouza safari kupitia mitandao ya kijamii na utaratibu huo iwe ni pamoja na kuwapatia leseni na utaratibu wa kulipa kodi, hii itasaidia serikali kuongeza mapato kwa ukusanyaji kodi kwani kwa miaka mingi sekta hii imekuwa ni kichaka cha wafanyabiashara wasio waaminifu kukwepa kodi kwa mbinu mbalimbali, Tunaweza kufanya utafiti kwa nchi kama Afrika Kusini na visiwa vya Mauritius na Shelisheli au Botswana ili kujua wenzetu wamewezaje kuboresha sekta ya utalii katika nchi zao na serikali inanufaikaje na mapato ya utalii katika nchi zao

3. Serikali ilegeze masharti ya kupata leseni za kuanzisha kampuni za utalii kwani siku hizi kuna aina nyingi za kuuza safari ambapo huduma nyingine zinaweza kufanywa na mtu mwingine kama huduma za ndege, huduma za magari kuna makampuni mengi ya kukodisha magari nk. Iwapo serikali itabadilisha masharti ya usajili wa makampuni ya utalii itaongeza wafanyabishara wengi katika sekta hiyo na hivyo kujiongezea kipato cha uhakika.

4. Tuna miundo mbinu mibovu sana katika vivutio vyetu vya utalii na mfano halisi ni ilipo mbuga ya Selous. Hii ni mbuga ambayo ingetumiwa na wageni wanaokuja jijini Dar kutembelea na kuona wanyama mbalimbali ukiwemo mto Rufiji. Hii ni mbuga ambayo ingeweza kutuingizia kipato kama kungetengenezwa mazingira ya kuwepo kwa Treni itakayokuwa inafanya safari zake hadi Kisaki na kurudi kila siku na pale kukawa na Hoteli kubwa na wawekezaji wa utalii wakapewa maeneo ya kujenga ofisi zao na kuboreshwa kwa barabara inayoingia Selous ingerahisisha watalii kutumia treni hadi Kisaki na pale wanapokelewa na kupelekwa mbugani na magari kwa kupitia barabara zilizoboreshwa. Naamini wageni wengi wanaoishi jijini Dar wangetumia fursa hii kutembelea Selous kila mwishoni mwa wiki. Kwa sasa njia ya usafiri wa gari unachukua saa kumi kupitia Matombo na saa 7 kupitia Rufiji ili kuingia mbugani huku ndege ndogo zikitumia dakika 45 lakini ni ghali sana watu wenye kipato cha kawaida kumudu. Serikali inaweza kuwashirikisha wadau wa utalii ili kupata mawazo yao namna nzuri ya kuboresha miundo mbinu yetu katika hifadhi zetu

5. Serikali iongeze vyuo vya utalii ikiwa ni pamoja na kuboresha mitaala ili kuinua elimu inayotolewa na vyuo hivyo. Kwa sasa vyuo vyetu vya utalii ni vichache na elimu inayotolewa humo ni ya kuwaandaa vijana wetu kuja kuwa vibarua na siyo kuwa viongozi katika sekta hiyo. Kwa sasa sekta ya utalii ndiyo inayoajiri wageni wengi kuliko sekta nyingine hapa nchini huku wengine wakiingia na kufanya kazi kiujanja. Tunahitaji mkakati makini ambao utaboresha elimu ya utalii kwa vijana wetu ili kupunguza ukosefu wa ajira. Zipo baadhi ya nafasi katika mahoteli yetu na makampuni ya utalii ili kuzishika labda ukapate elimu hiyo nje ya nchi au upate mafunzo kazini. Hii ni aibu kwa nchi yetu yenye vivutio vingi vya utalii kutegemea nguvu kazi kutoka nje huku vijana wetu wakiendelea kuwa vibarua

6. Tunahitaji katika mikoa ambayo iko karibu na vivutio waalikwe wawekezaji wa kuwekeza katika mahoteli na pia katika mikoa hiyo yatengwe maeneo ya historia ya makabila ya mkoa huo na maeneo mbalimbali yatengwe kwa ajili ya utalii na yaboreshwe ili watalii wanapokuja kabla ya kutembelea vivutio vyetu huko mbugani wapate fursa ya kujifunza utamaduni wa eneo husika na kujua asili ya eneo hilo na watu wake.

7. Serikali kwa kushirikiana na wadau wa utalii iboreshe maeneo yenye historia ya miji mbalimbali hapa nchini na kuitangaza ikiwemo ujenzi wa masanamu ya watu walioacha historia katika miji hiyo kama kule Tabora kina Mtemi Milambo au kina Kishosha Ng’wanamalundi

8. Kuwe na mkakati wa kutoa kipaumbele kwenye maonyesho ya utalii na yawe yanafanywa katika mikoa yote yenye vivutio ili kuimarisha utalii wa ndani hii iwe ni tofauti na ile ya kimataifa inayofanyika Arusha na Moshi, lakini hata hiyo ya Arusha na Moshi inapaswa kuboreshwa kwa kuiga wanavyofanya katika nchi za wenzetu

9. Taarifa za mara kwa mara kuhusu takwimu za watalii wanaoingia nchini na nchi wanazotoka ni muhimu ili kuwarahisishia wafanyabishara wa utalii kujua soko liko wapi, uwepo wa kitengo kitakachokuwa kinakusanya taarifa hizo na kuziweka mtandaoni kutasaidia kujua ni wapi tumejitangaza na wapi hatujajitangaza ili kuelekeza nguvu zetu huko.

10. Kuwe na mkakati wa kuhakikisha wafanyabishara wa utalii wanashiriki kwa wingi kwenye maonyesho ya utalii katika nchi mbalimbali ili kupata fursa ya kutangaza vivutio vyetu.

Naomba nipishe michango mingine kutoka kwa wadau mbalimbali ili tuweze kuishauri serikali namna nzuri ya kuboresha sekta hii ya utalii.


TOVUTI MBALIMBALI ZINAZOHUSU UTALII NCHINI

Tovuti Kuu ya Serikali: Watoa huduma za Utalii

National College of Tourism (NCT) | Tanzania

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Tovuti Kuu ya Serikali: Utalii


----
Habari mkuu!!!!
Hongera kwa kuanzisha uzi mzuri sana unao tukumbusha kutembelea vivutio vyetu
NIngependa tu kuongezea tu yakua kwa sasa Tanzania Bara ina jumla ya hifadhi 22 ambazo zipo chini ya mamlaka ya usimamizi wa hifadhi Tanzania yaani TANAPA na hii ni kutokana na ongezeko la hifadhi sita (6) mpya ambazo zilikua mapori ya akiba na sasa zimekua hifadhi za taifa.

Hifadhi zilizoongezeka ni
1. Burigi chato National park
2. Nyerere National park
3. Ibanda-kyerwa National park
4.Rumanyika-Karagwe National park
5. Kigosi National park
6. Ugalla river National park.

Pia Tanzaia tumebarikiwa kuwa na bonde la Ngorongoro ambalo lenywe linasimamiwa na (NCAA) yaani Ngorongoro Conservation Area Authority lilianzishwa mwaka 1959 ikiwa lengo lake kubwa ni kulinda lasilimali za wanyamapori pamoja na kuulinda utamaduni wa kimaasai. Hii ni sehemu pekee kwa Afrika ambayo wanyama pamoja na binadamu jamii ya kimaasai huishi kwa pamoja.

Pia Taznzania tumebahatika kuwa na maeneo yanayojulikana kama Game Reserve.
Haya ni maeneo yaliyo anzishwa kwa lengo kubwa la kuhifadhi na kulinda Wanyamapori na mazingira.
Katika maeneo haya ndo sehemu ambapo uwindaji wa wanyamapori hufanyika lakini ni kwa kibali maalumu.
mfano wa sehemu hizo ni Moyowosi game reserve, Usangu game reserve nk.

Pia tuna sehemu za kuvutia zijulikanazo kama Marine park and reserve.
Haya ni maeneo yyalianzishwa kwa sharia ya Marine park and reserve act no.29 of 1994 ikiwa na lengo la kulinda maeneo haya hasa kwakua ni maeneo muhimu kwa uzalianaji wa samaki, kulinda matumbawe, kulinda mikoko, kulinda mazalia ya ndege na viumbe vidogo vidogo vya majini.
Maeneo haya ni
1.Bongoyo island marine reserve
2.Mbudya island marine reserve
3.Pangavini island marine reserve
4.Funguyasini island marine reserve
Hivo vyote vinapatikana dar es saalam

Pia vipo
1. Mafia island marine park-Mafia pwani
2.Mnazi bay Ruvuma estuary marine park-Mtwara


Nikipata mda ntaeelezea kuhusu Wildlife management areas,Game controlled areas,Forest reserve na Historical sites.
----
Utalii wa Ndani nilishatembelea Ngorongoro, Pazuri sana Manyara kama tulibaniwa hatukuweza fika ziwani ila tulilala hostel na Tarangire tulitalii ila tulibaniwa pia hatukuweza fika chemchem ya maji ya moto hivyo kiufupi sikupapenda ilikuwa Mwaka elfu moja mia tisa na tisini na tano.

Ngorongoro tulitelemka na gari moja matata four wheel drive umbo lake kama la lile bus lililotumika kwenye movie ya War bus langi ya green. tulizungunga na tuliweza teremka tukaona viboko,Simba,Tembo,Nyati Swala na wanyama wengi Kifaru hatukumuona kudadeki bila kusahahu Masai..

Safarini niliweza kuona Mazao ya Sunflower maeneo ya Karatu niliweza kuwa level moja na Mawingu yana kiubaridi ila yapo kama Moshi(Ukungu) kihewa kizito kizito hivi

tulifika Snake park tukaona Nyoka wa aina mbali mbali Na Ngamia pia

Pale Momera Kwa Dr. Nagi Tanzanite kuna wanyama ila pamechoka.

Sina Deni kubwa kwa Serikali kuhusu Utalii wa Ndani Bado Mikumi japo nilishawahi pita kwa Treni na wanyama niliwaona... Kusini pia bado kwa kina Livingstone nakobado sijafika... Kilipoanguka Kimondo napo sijawahi fika japo Mbeya nilishawahi fika lol
 

Attachments

  • Photo 1.jpg
    Photo 1.jpg
    45.5 KB · Views: 707
  • photo 2.jpg
    photo 2.jpg
    53.8 KB · Views: 723
  • 1584085093864.png
    1584085093864.png
    20.6 KB · Views: 8
  • 1584085110067.png
    1584085110067.png
    20.6 KB · Views: 12
Tungeweza kupata hata vitano kutoka kwetu laiti kama tungetaka. yani hapo ndio tumeamua kidogo tumeingiza vitatu tungeamua sana? Tutafakari tuchukue hatua.
 
Bila shaka Ngorongoro na mlima Kilimanjaro ndivyo vingine - ninahisi tu.
 
Suala ni moja tu,vinatusaidia vipi katika kukuza uchumi wa nchi yetu?????

Good point Mkuu! Hilo ndio suala la msingi. Inabidi serikali ielewe kwamba sasa inabidi kutumia hela ili kuingiza hela. Lazima watoe promotion na advertising kabambe kupita vyombo vya habari vya kimataifa kama CNN, Al Jazira, BBC na Sky News, na magazeti ya kimataifa kutia ndani magazeti ya kwenye ndege (airline magazines). Kuna airlines kama South African Airways ambayo gazeti lao la "Sawubona" linashinda tuzo za best airline magazine kila wakati, wanaweza wakaingia makubaliano nao kutoa makala za hivyo vivutio.

Pia Tanzania Tourism Board wanaweza kufanya makubaliano na airlines, mahoteli na mbuga za utalii kwa ajili ya "tourism packages", ambapo Wizara ya mambo ya ndani wanaweza kutoa free visa kwenye hizo packages.

Na pia tulisaini makubaliano ya anga na USA, kitu gani kinawazuia kufuatlilia direct flights kati ya Washington na Dar? Sio mbali, South African Airways wanafanya safari hizo. Waziri wa utalii atumie nafasi kuzungumza na balozi wa Marekani ili kuitumia nafasi hii vilivyo kwa kuangalia uwezekano wa direct flights za airline za Marekani kuja Dar. Na pia waangalie uwezekano wa kurejesha flights za Lufthansa, kwa kuwa Germans nao wanafanya sana utalii (je mliwafukuza Lufthansa kwa kuwa walipompekua Diria alipogundulika kutumia nafasi yake kufanya biashara haramu?). Acheni siasa katika biashara, wajerumani hawabembelezi mtu bwana, wanaishi kwa sheria wale!

Kama Mkurugenzi wa Shirika la Utalii haiwezi kazi mie nipo waniteue!

Vivutio tunavyo tunaishia kuvikalia tu na kupeleka hela kwenye mambo yasiyozalisha, ovyooo!
 
Daa!! umesema kweli mkuu maana mambo hii hata mie nmesomea na the way talk it seems lke you can lead well basi anza taratibu.
 
Hongera TZ.
Inasikitisha kuona hadi leo hatuwez kuneemeka na utalii au maliasili zetu. Vipusa vinauzwa kwa magendo na wakubwa, zamani walikuwa wanauza ngozi za wanyama siku hizi wanauza wanyama hai, baadhi ya maeneo yameuzwa kwa ubia.. sijui baada ya miaka itakuwaje..Ila mi nilichangia kura kaadhaa at least tupate promotion.. na kuweka uzalendo
 
Bado vipo vingi ambavyo havijatangazwa mfano Pori la akiba selous(Large concentration of wildlife duniani),ziwa Victoria(caldera ziwa kubwa linaloninginia duniani).Lake Tanganyika(deepest lake duniani,lenye viumbe vinavyofanana na vilivyopo baharini),sehemu alipochukuliwa mifupa ya kiumbe Dinosaur ambayo mifupa yake ndiyo pekee iliyokamilika na ambayo wajerumani waliiba huko Kilwa na hawataki kuirudisha TZ).mwenye kujua vingine atujuze?
 
Kile cha wanafunzi walioenda form one bila kujua kusoma walikikumbuka?

Hakina tija, si bora hiki: kiongozi wa nchi hajui kwanini nchi yake ni masikini!, mgonjwa wa mguu anafanyiwa upasuaji wa kichwa na kinyume chake!
 
Nanukuu...!!

''Pamoja na Tanzania kuwa ni nchi ya pili (2) kwa vivutio vya utalii duniani baada ya nchi ya Brazil lakini bado ipo nyuma kwa utoaji wa huduma za utalii ikiwa ni nchi ya mia moja na kumi (110) kati ya nchi mia moja thelathini na tatu (133) hali inayoweza changia kupunguza pato la taifa ilinalotoka na sekta ya utalii''

Hii habari ni kwa mujibu wa ITV Tanzania leo.

Nimejikuta napata uchungu sana juu ya hili, nikaona kama JF tuna haja ya kulijadili hili na kuona udhaifu uko wapi mpaka nchi hii inafikia kushindwa vibaya namna hii katika maswala yahusuyo maendeleo.

Hivi kivutio kimewekwa na Mungu, Tanzania kupitia wizara ya Utalii tumeshindwa kabisa kuboresha na kutangazia ili kupata watalii?? Bajeti ya wizara ya Maliasili na utalii kazi yake ni nini hasa??

Kwa wanaofahamu vyema naomba watujuze nini hasa kazi ya WIZARA YA MALIASILI NA UTALII?? Yule waziri wa utalii hayumo humu atupatie ufafanuzi wa kina juu ya hili!! Ni aibu aibu aibuuu
=============================================



Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Kwa Mwaka 2014/2015

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili nami nichangie hoja hii ya mapendekezo ya mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Mheshimiwa Spika alitoa agizo kwa Serikali kwamba Mpango huu ni wa Serikali nzima lakini sasa hivi kuna full Ministers wapo wanne tu. Sasa sijui tunafanya kitu gani hapa jamani! Full Ministers wapo wanne tu kati ya Mawaziri 29 yaani sijui tumechoka, kuna mchokomchoko fulani hivi katika jamii ambao unasikitisha sana, sijui tunakwenda wapi? Wa tano ndiyo anaingia sasa
hivi Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo letu kubwa, ni umakini wa mipango tunayopanga hapa. Mapendekezo ya mpango huu yana kurasa 62, zaidi ya kurasa 47 ni kama copy and paste za mwaka jana na kurasa 13 au 14 ndiyo mpango wenyewe tunaotegemea wa mwaka ujao wa fedha. Kurasa 62 kwa Wabunge na makabrasha mengine kusoma inakuwa ni kujirudiarudia sana. Naomba tu kusema kwamba, dunia ya leo kuna kitu kinachoitwa KISS (Keep It Short and Simple), waweke kwenye majedwali ambayo yanarahisisha Waheshimiwa Wabunge kuweza kufuatilia kwa umakini na urahisi kuliko hii vuta nikuvute.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Bajeti, tumechambua kwa makini na niseme kabisa mawazo yetu ya Kamati ya Bajeti nayaunga mkono na tuangalie vipaumbele ambavyo ni muhim. Nizungumzie vipambaumbele viwili yaani bandari pamoja na reli kwa Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe ambaye ameingia hapa sasa hivi. Kama tunataka uchumi wetu uweze kuingia kwenye karne ya 21, ukaingia kwenye kipato cha kati, hatuna budi kuwekeza kwa kiwango kikubwa kwenye bandari na reli.

Bandari zetu zote zinahitaji kama dola bilioni tatu. Bandari ya Dar es Salaam dola bilioni 1.5 na reli inahitaji kama dola bilioni 7. Jumla tukitafuta dola bilioni 10 tutaondokana na huu wasiwasi tunalionao, tutafungua lango kuu la reli ya kati au lango kuu la uchumi na usafiri ambao ni rahisi kuliko wote duniani kwanza ni wa maji, pili ni wa reli.

Ujenzi wa barabara ambao tunausifia sana, usafirishaji wa zaidi ya kilomita 600 huwa ni hasara. Angalia haya malori makubwa yanavyozidi kuharibu barabara zetu kwa hiyo tunarudia kwenye umaskini uleule yaani tunajenga barabara ya kuja Dodoma, ya kwenda Kaskazini hata ya kwenda Kusini. Kwa hiyo, bila kura na reli ambayo itasafirisha mizigo na kwa urahisi ambao ni cheap, tutakuwa hapa tunajidanganya tu kwamba barabara zimejengwa lakini tunazunguka kwenye umaskini uleule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza kwa Serikali, wanasema deni ni himilivu lakini kwa mapana zaidi, timu iwe ni ya maabara au ni ya wapi, fedha zipatikane, generation hii iwekeze kwenye bandari, geographically tupo vizuri, tuwekeze kwenye reli vizuri ili tuondokane na hizo ngonjera za vuta nikuvute za kukopa dola 100,000, 200,000 au 1,000,000 lakini tukope heavily na tuwekeze, mikopo hii duniani ipo na siyo lazima tufuate masharti ya IMF na World Bank tu, sisi ni Taifa ambalo tukiamua tunaweza. Sisi nchi yetu hii ambayo imekuwa ni kiongozi katika Bara la Afrika, mbona tunakuwa na majibu mepesimepesi kwa maswali ambayo ni magumu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka tarehe 9/4/2013 tulivyokwenda kumwapisha Uhuru Kenyatta nilikuwepo na Waziri Sitta alikuwepo na Mheshimiwa Lowassa na wengine. Wimbo wa Afrika uliopigwa, beti ya kwanza ni wimbo wa Tanzania, ni wimbo wa Afrika leo kwamba Mungu ibariki Afrika, ndiyo wimbo wa Afrika. Sasa kama tumepewa heshima hiyo na Bara la Afrika, sisi Tanzania tunafanya nini?


Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiangalia ngonjera zilizotokea jana hapa kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki, hakuna kosa kuwa na ushirikiano kati ya Kenya na Tanzania wala Kenya na Uganda, ukiangalia nchi zote za Afrika Kenya ni ya kwanza kwa uwekezaji wa Tanzania FDI yaani Foreign Direct Investment, kwa dunia ni ya pili, lakini majibu hapa nani kampa talaka huyu, nani kamuoa huyu, economic diplomacy ipo wapi? Let us be sincere! Kauli hizi zinaleta maafa makubwa kwa Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa uongozi wetu wa Taifa la Tanzania sawa, tuna kilomita za mraba zaidi ya 945,000, Kenya 581,000, Uganda 236,000, Burundi 27,000 na Rwanda ni 26,000, sawa sisi tumewazidi kwa zaidi ya kilomita za mraba 73,000 lakini tumewazidi hivyo, tunaitumiaje fursa tuliyonayo katika kuonyesha kweli tunaongoza katika ukanda huu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie kwenye sekta ya utalii, Tanzania ni ya pili kwa vivutio vya utalii duniani baada ya Brazil lakini ukiangalia tupo nafasi ya ngapi kwenye vivutio hivi katika kuleta mapato kwenye Taifa hili katika ushindani? Sisi ni wa pili duniani lakini tunashika nafasi ya 110 kati ya nchi 133. Mauritius ni ya 131 kwa vivutio vya utalii duniani kati ya 133 lakini ni ya 53 katika sekta ya utalii.

Sasa ukiangalia hii sekta ya utalii leo hii, wenzetu wa Kenya ni wa 28 kwa vivutio vya utalii lakini in terms ya uingizaji wake wa pato la Taifa ni 103 imeishinda Tanzania, sisi ni wa pili duniani. Sasa sekta hii ya utalii mbona kigugumizi? Mwaka jana hapa kwenye bajeti na tusingependa itokee tena kwenye bajeti inayokuja kwamba tunaanza tena kukamua watalii hawa wakati tunajaribu kuikuza sekta hii ya utalii, tunajaribu tuangalie sekta ya anga itakuwa namna gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, angalia leo hii KLM kutoka Amsterdam kuja Kilimanjaro, kuja Dar es Salaam ni aghali kuliko kutoka Amsterdam kwenda Nairobi. Sasa kwenye utalii humu tunawekezaje? Costal line yenye kilomita 1,424, mahoteli ya kitalii yapo wapi? Wazawa watalii wanaowekeza humu ndani, mzawa anapewa nafasi ya kujenga hoteli lakini hapewi eneo la kujenga hoteli, inakuwa ni urasimu tu.

Wizara ya Ardhi na Wizara ya Utalii wanatenga maeneo, wanakubaliana mwekezaji amekuja immediately anapewa eneo ili kuondokana na huu urasimu, urasimu, urasimu, urasimu!

Mheshimiwa Mwenyekiti, inasikitisha sana kwa kweli, tujitahidi tuone ni namna gani badala ya kusikiliza upande mmoja tu kuhusu hili sokomoko lililotokea tarehe 24 na 25 mwezi wa Juni kule Kampala na 28 Agosti, 2013, Jumatano, kule Mombasa kuhusu Rwanda, Uganda na Kenya.

Tumesikiliza upande mmoja wa Serikali lakini ukiangalia Wakenya walivyowekeza hapa waweza kutuacha hivihivi, hapana! Tuone hii ni changamoto chanya na sisi tuamke tuwekeze seriously kwenye bandari yetu, tuwekeze seriously kwenye reli yetu na kutoka Dar es Salaam kwenda Bunjumbura na kwenda Congo ni karibu zaidi na ni punguzo la zaidi ya kilomita 1000 kwa hiyo economically mfanyabiashara yeyote atakuja kwenye bandari ya Dar es Salaam. Sasa tusilalamikelalamike tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna nguzo kuu sita za umaskini wa fikra. Nguzo ya kwanza ni majungu, ya pili ni fitina, ya tatu ni umbeya, ya nne ni kusema uwngo, ya tano ukishasema uwngo unajenga chuki katika jamii na ya sita ni uvivu wa kufikiri. Let us be sincere, tujiulize tunaongea nini na nani, mahali gani, wakati halafu athari yake itakuwa ni nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuwe Taifa linaloongoza Bara la Afrika. Uwezo huo tunao, tusiangalie wazo limetoka kwa nani, angalia quality ya wazo lenyewe, angalia fikra zenyewe, tushirikiane wote. Naamini pamoja tukiamua Taifa la Tanzania tunaweza, uwezo tunao ilimradi tuachane na hizi tofauti ndogondogo za kiitikadi kwenye mpango wa kitaifa tunawekeza fikra zetu zote kwa pamoja kwa kuwa Taifa hili ni letu sote kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia muda huu.

Eng. James FrancisMbatia[NCCR-MAGEUZI] Nominated by the President
 
Kama waziri usika ana jihusisha na biashara ya meno ya tembo tuna tegemea nn!....
 
Nanukuu...!!

''Pamoja na Tanzania kuwa ni nchi ya pili (2) kwa vivutio vya utalii duniani baada ya nchi ya Brazil lakini bado ipo nyuma kwa utoaji wa huduma za utalii ikiwa ni nchi ya mia moja na kumi (110) kati ya nchi mia moja thelathini na tatu (133) hali inayoweza changia kupunguza pato la taifa ilinalotoka na sekta ya utalii''

Hii habari ni kwa mujibu wa ITV Tanzania leo.

Nimejikuta napata uchungu sana juu ya hili, nikaona kama JF tuna haja ya kulijadili hili na kuona udhaifu uko wapi mpaka nchi hii inafikia kushindwa vibaya namna hii katika maswala yahusuyo maendeleo.

Hivi kivutio kimewekwa na Mungu, Tanzania kupitia wizara ya Utalii tumeshindwa kabisa kuboresha na kutangazia ili kupata watalii?? Bajeti ya wizara ya Maliasili na utalii kazi yake ni nini hasa??

Kwa wanaofahamu vyema naomba watujuze nini hasa kazi ya WIZARA YA MALIASILI NA UTALII?? Yule waziri wa utalii hayumo humu atupatie ufafanuzi wa kina juu ya hili!! Ni aibu aibu aibuuu

Usijisikie uchungu. Elewa kwamba Watanzania tunapenda kujisifia kwenye vyombo vya habari, kama waingerrza na timu yao ya Taifa.

Angalia hapa:
http://en.m.wikipedia.org/wiki/World_Tourism_rankings

Utaona kuwa wenzetu wanaongelea kuingiza watalii zaidi ya milioni ishirini kwa mwaka, sisi tukijitahidi sana eti watalii milion moja. Miaka mingine tunaingiza watalii laki sita na ushee.

Tatizo letu ni kukariri kwamba watalii watakuja kupanda mlima kilimanjaro na kutembelea Serengeti na Ngorongoro pamoja na Zenji.
Vivutio vingine hatuvi-promote. Miji yetu michafu, ipo ugly, usalama wa wasiwasi, hoteli za wasiwasi halafu chache, barabara za kuvifikia vivutio vingine za shida...na matatizo mengine kibao. Sasa ukute sector yenyewe inasimamiwa na ma-much know- wabishi, wanasikiliza ushauri ukitolewa na wakubwa tu, sisi akina yakhe tukiwashauri tunadharauliwa kwa vile hatujui na hatujasomea utalii....

Lakini hii ndio nchi yetu, na ndivyo tulivyo.
 
Tanzania maeneo matatu tu yangeweza kuinua uchumi wetu kama yangekuwa na Viongozi weledi na wenye mapenzi mema na nchi yao.
.Maliasili na Utalii
.Madini na viwanda
.Mifugo na kilimo
 
Tanzania maeneo matatu tu yangeweza kuinua uchumi wetu kama yangekuwa na Viongozi weledi na wenye mapenzi mema na nchi yao.
.Maliasili na Utalii
.Madini na viwanda
.Mifugo na kilimo

Umenena vyema mkuu! Tumekosa viongozi wenye weledi na mapenzi mema kwa nchi yao
 
Mi nadhan serkali imeshndwa kutangaza vyema baadh ya vvutio vngne vya utalii wao wamekarir mikum,selou,n.k wanxahau vvtio vngne km michor ya mapngon kule handen,ziwa ngoz n.k
 
Back
Top Bottom