Tanzania Bara na Visiwan zimesaini mkataba wa makubaliano ya kuunganisha visiwa vya Pemba na Unguja na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,207
4,703
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimesaini mkataba wa makubaliano ya kuunganisha visiwa vya Pemba na Unguja na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano

Utiaji saini huo umefanywa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba kwa upande wa Bara na Mhandisi Shukuru Awadh Suleiman, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Miundombinu ya Tehama Zanzibar (ZICTIA) kwa upande wa Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula amesema Serikali ya Tanzania imejenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 700 na kuunganisha kwenye mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na kwenye nchi jirani za Congo, Zambia, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda na Malawi ambapo maunganisho haya yanaenda kufungua fursa za wawekezaji na watumiaji wa huduma za mawasiliano wa ndani na nje ya nchi

Naye Dkt. Mustafa Aboud Jumbe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema kuwa haya ndio matunda ya mapinduzi yanayopatikana katika nchi yetu.Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetumia zaidi ya shilingi bilioni 30 kuunganisha mikoa na wilaya zote za Unguja na Pemba licha ya changamoto zilizokuwepo.

WhatsApp-Image-2020-09-24-at-14.13.34-1-630x420.jpg
 
Hivi si tuliambiwaga na kikwete mkongo wa taifa ukikamilika mawasiliano ya simu na internet Bei itakuwa sawa na bure, hivi bado haukukamilika? Maana umepita miaka Kama nane hivi gharama zinazidi kuwa kubwa.
 
Hivi si tuliambiwaga na kikwete mkongo wa taifa ukikamilika mawasiliano ya simu na internet Bei itakuwa sawa na bure, hivi bado haukukamilika? Maana umepita miaka Kama nane hivi gharama zinazidi kuwa kubwa.
Ufisadi Huu Ambao Ni Mkubwa Kuwahi Kutokea
 
Back
Top Bottom