Tanzania bara iuende chama chake cha soka...Raisi ZFA

Nokla

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2012
Posts
3,190
Reaction score
1,780
Rais huyu ndugu Ravina amesema kwamba Zanzibar tayari wana ZFA na au Tanganyika waunde chama chao na kuiacha TFF ishughulike na timu ya taifa, pamoja na kurudisha ligi ya Muungano ili iweze kusimamia vema ligi hiyo na kuunda timu bora ya taifa....

Je wewe unaonaje hii???
 
Michezo siyo moja ya masuala ya Muungano. Akae kimya huyo mpayukaji.
 
kupayuka ni tusi eh!

Tell him! Tumechoshwa na mambo ya Zanzibar, walijifanya wajanja wakapata uanachama wa CAF vichwa vikavimba, wakaelekea FIFA wakanoa, leo wanakuja na issue ya chama cha soka cha Tanganyika. Nasisitiza michezo siyo issue ya Muungano, hata kuita wachezaji wa Zanzibar Taifa Stars ni upendeleo tu, hatulazimiki kuwaita.
 
Michezo siyo moja ya masuala ya Muungano. Akae kimya huyo mpayukaji.

Kama sio moja ya masuala ya Muungano kwa nini kuna timu ya taifa inayojumuisha wachezaji toka Bara na Visiwani? Na kwa nini palikuwa na Ligi ya Muungano? Kaa kimya ww mpayukaji.
 
Tell him! Tumechoshwa na mambo ya Zanzibar, walijifanya wajanja wakapata uanachama wa CAF vichwa vikavimba, wakaelekea FIFA wakanoa, leo wanakuja na issue ya chama cha soka cha Tanganyika. Nasisitiza michezo siyo issue ya Muungano, hata kuita wachezaji wa Zanzibar Taifa Stars ni upendeleo tu, hatulazimiki kuwaita.

Wabongo tuwe tunafikiria kabla ya kuropoka. Jamaa(rais wa ZFA) anachosema kina uzito. unaposema TFF unamaanisha Tanzania kwa ujumla (zenji na bara) na ndivyo FIFA wanavyotambua. Watu kama ww ndo wale mnaojua kutype bila kufikiria kwa kina mtu anachozungumzia.
 
Mkuu Rubaman, sina bifu na wewe, wala sina malaria na wala sijalewa. Issue ya michezo si ya Muungano na ndiyo maana tuna BMT na BMZ. Kuingiza issue ya michezo kinyemela katika Muungano ni uvunjaji wa katiba ya Muungano, Wazanzibar wote wanalijua hili. Mwenye data kwamba michezo ni issue ya Muungano azianike hapa jamvini. Huko nyuma tulifanya makosa kuanzisha ligi ya Muungano kinyume cha katiba, haturudii makosa tena.
 
Tell him! Tumechoshwa na mambo ya Zanzibar, walijifanya wajanja wakapata uanachama wa CAF vichwa vikavimba, wakaelekea FIFA wakanoa, leo wanakuja na issue ya chama cha soka cha Tanganyika. Nasisitiza michezo siyo issue ya Muungano, hata kuita wachezaji wa Zanzibar Taifa Stars ni upendeleo tu, hatulazimiki kuwaita.

mi nadhani wazenj wapo sahihi kwenye hili suala kwani kama michezo sio suala la muungano inabidi TFF ivunjwe na wao wapate uwakilishi ndani ya fifa
 
Watu hawajelewa, kuna TFF ambayo inasimamia Tanzania na bado pia ndio inayosimamia ligi kuu bara, sasa kama kuna Baraza la michezo kwa nini ligi bara isimamiwe na TFF, kama hivyo basi na hiyo TFF izisimamie klabu za Zanzibar, au muungano upo kwenye timu ya taifa tu?
 
Back
Top Bottom