Tanzania Airports Authority

Tanzania Airports Authority

Mourice Moses

New Member
Joined
Aug 10, 2016
Posts
4
Reaction score
0
🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁
 
Hata hivyo mpo wengi sana ndege yenyewe ipo moja tu! jiongeze sio mpaka ufukuzwe kazi ndo ujue kipaji chako

Wewe unachanganya mambo na ni vyema mjifunze kuongea mkiwa na details kuna TAA, TCAA, TMA, na ATCL , uyu anazungumzia TAA ambayo inahusika na kuhudumia viwanja vya ndege, TAA navyojua hawana ndege wala hawahusiki na mambo ya anga, pale TAA nimeshaomba tender ya usafi mpaka nimechoka ila anapataga mtu mmoja tu naisi anaonga sana yani haiwezekani ukamzidi hii kampuni nazani ni ya mtu pale TAA si bure
 
KUSITISHWA KWA AJIRA YA MUDA KATIKA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA July 1, 2016. MPAKA SASA 26 August 2016 WAFANYAKAZI HAO HAWAJALIPWA MAFAO YAO.

Ndugu Mheshimiwa:

Je hivi serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajiri ya kuwanyonga wanyonge?

Tafadhari husika na kichwa cha habari hapo juu, Mimi ni kijana wa Kitanzania ninaependa kujibidiisha katika kazi, na pia siku zote ninapenda kuwa sauti ya wanyonge, nikipigania haki zao kwa namna yoyote. Ninaandika Barua hii kwako ili niweze kufikisha taarifa ambayo kwa namna moja ama nyinginge yaweza kuwa imefichwa…!

Tangu tarehe 1 July 2016, Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania ilianza kutoa Barua za usitisho wa ajira kwa waajiriwa wa muda, yaani ajira ya Mikataba. Mamlaka imekuwa ikiajiri wafanyakazi wa mikataba kama zilivyo taasisi zingine ama Mamlaka zingine kwa muda sasa, TAA imekuwa ikitoa ajira hizo kulingana na aina ya kazi zinazoendelea katika viwanja vyake. Wapo wafanyakazi wenye mkataba wa Miezi Mitatu, Miezi Sita, na wengine Mwaka Mmoja. Lakini mpaka kufikia leo Tarehe 26 August 2016, wafanyakazi hao hawajapewa stahiki zao.

Mheshimiwa, kuna vijana wengi sana ambao wameathirika katika hili, maana wengi wao wana familia zinazo wategemea na wengine wapo katika kujiendeleza kimasomo, kwa maana mfanyakazi wa muda amekuwa akijisomesha kupitia pesa yake anayo lipwa na sio kutoka kwa muajiri wake, kama ambavyo inavyofanyika katika taasisi mbalimbali.

Barua hizo za usitisho wa ajira kwa wafanyakazi wa muda, baadhi ya maneno husomeka kama ifuatavyo, “Nakuarifu kuwa huto ongezewa Mkataba mwingine wa Ajira na hivyo ajira yako imefika kikomo. Hii ni kutokana na mabadiliko ya kiutendaji ya Serikali yanayofanyika sasa

Swali langu kama mtetezi wa haki za wanyoge, katika kuhakikisha nafikisha ujumbe katika serikari yangu. Je serikari ya awamu ya tano ipo kwa lengo la kukandamiza wanyonge na kuua mitazamo yao ya maisha ama ipo kwa ajili ya kupambana na Wabadhirifu, Wahujumu uchumi pamoja na wafanyakazi hewa katika mazingira ya ajira? Iko wapi kauli ya Mheshimiwa Raisi wakati wa siku ya wafanyakazi katika Hutuba yake juu ya kuwapa moyo wafanyakazi wanao jituma?

HAYA NI MAMBO BAADHI AMBAYO WAMEKUWA WAKIKOSA WAFANYAKAZI HAO, LICHA YA KUJITUMA KWA BIDII ZOTE KATIKA KUHAKIKISHA MAMLAKA INAKUWA KTK HALI NZURI YA KIUCHUMI.

1.Posho zisizokidhi mahitaji ya wafanyakazi, kutokana na kutokuwa na Overtime kwa wafanyakazi hao.

Mheshimiwa hali hii inasikitisha sana kwa maana imekuwa kawaida kwa wafanyakazi wa mamlaka ya viwanja vya ndege hasa wale waliopo JNIA kutokuwa na overtime, na hali inaumiza hasa kama mfanyakazi atakuwa hana posho inayoweza kuwa na faida kwake. Wafanyakazi wa JNIA TB II wamekuwa wakifanya kazi hata zaidi ya masaa 12, bila kuwa na posho yoyote, na hali hii imezoeleka, na wapo viongozi katika mamlaka hiyo wanaonyonya haki za wafanyakazi hao.

2.Kutokuwa na viongozi wanao jali haki na stahiki za mfanyakazi.

Mheshimiwa: una vijana ambao walikuwa ni madereva tena wenye vigezo vyote, ambao wameitumikia Mamlaka hiyo takribani Miaka kumi sasa, lakini kutokana kutokuwa na kuto kuwa na utu, wameachishwa kazi, na sasa ni Mwezi wa pili hawajalipwa stahiki zao, na wapo njia panda kutokana na Mamlaka kuwagawa watu ktk matabaka, na kuto kuzingatia vigezo vya ajira na stahiki za mfayakazi.

Ktk kiwanja cha Ndege JNIA Terminal II, kuna vijana walio tolewa VETA, ili waweze kusaidia katika shughuri mbalimbali za kimitambo na umeme, ili kuboresha mitambo na kusaidia uendeshaji wa mamlaka ya TAA, kwa taarifa nilizo nazo Madaraja ya kupaki ndege, yanayo tumiwa na abilia, Vijana hao kwa sasa wamekuwa waki operate na kufanya matengenezo tangu mwezi wa Tisa mwaka 2015, hao vijana ni miongoni mwa walio timuliwa na Mamlaka hiyo, Bila kujali wanaiingizia Mamlaka kiasi gani kupitia Madaraja hayo ya kupaki ndege.

Swali langu katika serikali, Je cheti cha VETA hakitambuliki katika ajira za serikalini? Ama Mamlaka hiyo ilikuwa inahitaji kuuwa ufundi na utendaji wa kazi kwa vijana hao? kwa maana Mitambo inayopatikana hapo JNIA, ni vigumu kuikuta sehemu zingine kama mitambo ya kusukuma mabegi ya abilia Coloso na Conveyor belt, na Madaraja hayo ya kupita abilia akiwa anapanda ama kushuka katika ndege (Aerobridge for Passengers)

Licha ya hao vijana kutelekezwa na mamlaka hiyo na kuto kuwajali haliyakuwa walifuatwa Veta chang’ombe ili waje kuokoa jahazi la kumwagika kwa maji ktk sehemu ya kuondokea abilia, Serikali ya awamu ya tano katika kuongeza jitihada ya kupambana na ingizo la madawa ya kulevya, Wapo Maafisa usalama ambao wanao jituma zaidi ambao walistahili zawadi kutokana na ufanisi wao wa kazi, lakini hatima yake Mamlaka imewaachisha kazi na wao pia ikidai kuwa huo ni utaratibu wa kutoka serikalini, Swali langu ni Je kwanini wanao kandamizwa ni wanyonge tu, ama ndio kusema myonge hana kauli? Na kwanini wapo walioweka watu wao na wengine kuweka hata mahawala zao kama inavyo semekana na hawajatolewa hadi sasa? Ama siku zote myonge ndie anae umia? Tafadhari naomba ufuatilie haya ninayo kujuza, kwani watu wanaichafua serikari kiutendaji.

3. Swala la kujiendeleza kielimu.

Imekuwa ni ngumu kwa mfanyakazi wa muda katika Mamlaka hiyo kujiendeleza kielimu, na hata akifuatilia amekuwa akiambiwa watu wa mikataba huwa si rahisi kwenda kujiendeleza kielimu, sasa chakushangaza kila kukicha kama tutambuavyo teknolojia inaongezeka, ufanisi hauwezi kuwepo kama mfanyakazi hato jiendeleza kielimu. Mheshimiwa usishangae kukutana na mtu anafanya kazi Ktk kiwanja cha ndege hali ya kuwa hajui kuhusu chochote kwenye mambo ya Aviation, na hiyo ndio TAA.

4.Hitimisho la Barua hizo

Barua zimehitimisha kwa kusema kuwa “Nakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya” Swali langu, hivi ni kheri ipi inayo zungumzwa katika kumuachisha kazi mtu alie na vigezo vya kazi? Je, hao mamlaka wanatambua juu ya ugumu wanao upata vijana katika kutafuta kazi? Na kwanini wamewapotezea muda? Maana wapo ambao wana miaka mpaka saba ktk ajira hizo, Kinacho sikitisha mpaka sasa ni mwezi wa pili hawajalipwa mafao yao.

Tafadhari, serikali inatakiwa kuingilia kati swala hili, ili baadhi ya watendaji wa serikali wasiichafue serikali ya hapa kazi na kutafsilika vibaya. Nendeni TAA HQ mkajionee mambo yanayo endelea huku, kuna watu wanahitaji kufanya yao.
TAA kazi za muda izo walio wengi mnapata kwa kupachikwa na ndugu zenu hapo bila vigezo, watu wanapata kazi kwa kujuana tu, angalia wengi wenye ajira za muda mfupi lazima ana undugu na mtu flani mkubwa japo wapo wachache wenye kupewa kulingana na uwezo ila wengi ni kujuana pole sana kwa kutumbuliwa pia kwanini msiende mahakamani kufungua kesi? Chukueni izo barua nendeni kwa wanasheria wawasaidie maana najua lazima kuna muda wakulipwa mafao yenu tangu kuachishwa kazi pia mafao ya mifuko ya jamii nayo mpewe yote.
 
Hata hivyo mpo wengi sana ndege yenyewe ipo moja tu! jiongeze sio mpaka ufukuzwe kazi ndo ujue kipaji chako
Umechemka hujui hataa kinachoongelewa HII sio atcl Mpwa taa n mamboya viwanja vya ndege awahusiki NA uendeshaji wakampuni ya ndege
 
TAA kazi za muda izo walio wengi mnapata kwa kupachikwa na ndugu zenu hapo bila vigezo, watu wanapata kazi kwa kujuana tu, angalia wengi wenye ajira za muda mfupi lazima ana undugu na mtu flani mkubwa japo wapo wachache wenye kupewa kulingana na uwezo ila wengi ni kujuana pole sana kwa kutumbuliwa pia kwanini msiende mahakamani kufungua kesi? Chukueni izo barua nendeni kwa wanasheria wawasaidie maana najua lazima kuna muda wakulipwa mafao yenu tangu kuachishwa kazi pia mafao ya mifuko ya jamii nayo mpewe yote.
SINAKAUZOEFU SANA ILA NINA KAIDIA AMA KITAWASAIDIA AMA LAH
KWANZA POLENISANA SANA MUNGU NDIE MTETEZI WA HAKI...

UNAPOSEMA ULIKUWA NA MKATABA NA UMEFANYA MIAKA KUMI BADO NAPATA KITHUNGUTHUNGU HAPO..MNAPOPEWA MIAKA MIWILI LET SAY..UKIMALIZA MKATABA LAZIMA UNAPEWA MAFAO YOTE NDIO UNARENEWA MKATABA ....

SASA NAWASIWASI MMEFANYA MIAKA KUMI MIKATABA AIJAISHA MDA HIIO N AJIRA KAMILI AUTOMATICALLY BILA KUJIJUA...........

MNACHOTAKIWA LINDEN SALARYSLIP ZENU KAMA MLIKUWA MNAKATWA NSSF PPF NK WATAWAPA(HAIHUSIKI NA WENYE VYETIHEWA))HAO WAMEAPIZWA AWALIPWI ..ANYWAY SIJUIZABABU ZAIDI

NA KAMA MLIKUWA NA MKATABA WA MIAKA KUMI OMBENI MSOME SHERIA ZA MAMLAKA ZINASEMAJE MTU AKIWA AMEMALIZA MDAWAKE ANALIPWAJE ..HILI N WAZO HATA MKIWA NA MWANASHERIA MSIKINBILIE MAHAKAMAN KABLA AMJAPATA UHAKIKA WA HILI....SASA MKIPATA MNAWEZAJUA MNAANZAJE...NAPENDA SANA MAELEWANO KATIYAMWAJIRI NA MWAJIRIWA YAISHE MAPEMA NAJUA SHIDA ZAKE NAJUA MAFIOSO YAKE PALE CMI NINI KINACHOENDELEAGA NAWAPENDA NAOMBA MOLA HAKIZENU ZIPATIKANE INSHALLAH
 
SINAKAUZOEFU SANA ILA NINA KAIDIA AMA KITAWASAIDIA AMA LAH
KWANZA POLENISANA SANA MUNGU NDIE MTETEZI WA HAKI...

UNAPOSEMA ULIKUWA NA MKATABA NA UMEFANYA MIAKA KUMI BADO NAPATA KITHUNGUTHUNGU HAPO..MNAPOPEWA MIAKA MIWILI LET SAY..UKIMALIZA MKATABA LAZIMA UNAPEWA MAFAO YOTE NDIO UNARENEWA MKATABA ....

SASA NAWASIWASI MMEFANYA MIAKA KUMI MIKATABA AIJAISHA MDA HIIO N AJIRA KAMILI AUTOMATICALLY BILA KUJIJUA...........

MNACHOTAKIWA LINDEN SALARYSLIP ZENU KAMA MLIKUWA MNAKATWA NSSF PPF NK WATAWAPA(HAIHUSIKI NA WENYE VYETIHEWA))HAO WAMEAPIZWA AWALIPWI ..ANYWAY SIJUIZABABU ZAIDI

NA KAMA MLIKUWA NA MKATABA WA MIAKA KUMI OMBENI MSOME SHERIA ZA MAMLAKA ZINASEMAJE MTU AKIWA AMEMALIZA MDAWAKE ANALIPWAJE ..HILI N WAZO HATA MKIWA NA MWANASHERIA MSIKINBILIE MAHAKAMAN KABLA AMJAPATA UHAKIKA WA HILI....SASA MKIPATA MNAWEZAJUA MNAANZAJE...NAPENDA SANA MAELEWANO KATIYAMWAJIRI NA MWAJIRIWA YAISHE MAPEMA NAJUA SHIDA ZAKE NAJUA MAFIOSO YAKE PALE CMI NINI KINACHOENDELEAGA NAWAPENDA NAOMBA MOLA HAKIZENU ZIPATIKANE INSHALLAH
Sijui kama atakuwa amekuelwa asilimia mia. , nawaza tu lakini.
 
Pole kijana kwa yaliyokukuta.Ila nikufahamishe kwamba hili linafanuika ktk taasis zote za serikali kwa sasa hivyo umewasemea umati mkubwa tu wa vijana kama wewe
 
hawa wa ajira za mkataba wengi wao hawana vigezo ,waliingia kiujanja ujanja,ni vema serikali ingewatoa wote wa mkataba as bado wapo wengi wamebaki ndani ya mamlaka ya viwanja vya ndege na ajira zitangazwe upya ,zishindaniwe na watu wote.
 
Back
Top Bottom