Tanzania/Afrika

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
6,565
8,427
Habarini za leo enyi ndugu waafrika
Kumekua na tabia kadhaa kwa waafrika kuukana na kuubeza uafrika wetu kiutamaduni,kisiasa,kiuchumi na mambo mengi sana kiasi inatia aibu na kuchukiza kwa mtu mzalendo

1.kuna tabia ya kujaribu kuona cha nje uzunguni kua ni bora kuliko cha kwetu,hii ni dhambi..kupenda utamaduni usio wetu kama mavazi,na namna ya kuishi kwa kuiga iga bila sababu za msingi na kusababisha hao wazungu wa mataifa ya mbali kutudharau na kutuona hatufai maana ni kama hatujielewi

2.kulingana na hayo imesababisha mzungu asiyetutakia mema kupenya kwetu na kujifanya mwema anajaribu kuwalubuni baadhi ya waafrika kwa pesa na ahadi kede kede kisha kutengeneza uchonganishi kati ya sisi kwa sisi wenyewe,inafikia mtu au mwanasiasa mmoja anajaribu kuingia kwenye mazungumzo na mzungu kwa faida yake binafsi kuivuruga nchi yake kwa maneno yasiyo na maana na kufanya kuaminisha watu kua serikali hii au ya nchi fulani(ndani ya afrika)haifai.hapa simsemi mtu lakini kuna mambo yanaonekana,chukulia hapa kwetu Tanzania,mambo chungu mzima kiongozi wa nchi anapambana nayo ili kulifanya Taifa likae sawa kwa faida ya vizazi,anaopambana nao ni wageni wanyonyaji,lakini anaibuka mwafrika mmoja na kuanza kuponda anachokitetea mkuu wa dhamana ya wananchi na kujaribu kumtetea mgeni fedhuri na baadhi ya waafrika wanashangilia

3.Hata kama kunaonyesha mapungufu kibinadamu ktk uongozi wa nchi yoyote ile hapa AFRICA lakini uzalendo kwanza..penda nchi yako Tanzania,penda East Africa,penda Africa kwa ujumla maana ndiyo nyumbani kwetu,watu mpaka wanasema na kupanga kuikimbia Africa eti wakiamini kwenda ulaya ni kwenda kufanikiwa kimaisha,wanasahau kua Africa yote ina ardhi ya kufanya kazi na kufanikiwa iwapo tutajituma na kupanga mikakati thabiti.kujaribu kuusingizia uongozi uliopo madarakani kwamba unasababisha umasikini si kweli,umasikini unatolewa na juhudi za kila mwananchi na kila muafrika.tukiwa na juhudi yawezekana kabisa siku moja hao wageni fedhuri wakaja kwa kutubembeleza na kufanya nao biashara kwa maelekezo yetu wenyewe.

4. Ingekua ni kwa uwezo wangu ningeifanya AFRICA kua ni moja au yenye nchi 5 tu.ili kila mgeni mzungu fedhuri atakaekuja kumlaghai mTanzania basi mKenya asimame,akitaka kumuibia mRwanda basi Uganda isimame kama kitu kimoja.japo tungefikia kua kitu kimoja kama waAFRICA hulu tungepiga hatua sana na hii inawezekana iwapo muafrika yoyote atakaefuatwa na mgeni kutumiwa ili kuichanganya nchi na Afrika kwa ujumla basi awe mzalendo na amfukuzilie mbali huyo mgeni na kumripoti ili asije akahama na ulaghai wake kutoka Sudan mpaka Botswana na kufanikiwa kuinyonya Afrika kupitia nchi hiyo,najua ukisoma haraka haraka bila kutafakali hutakaa ukaelewa namaanisha nini.hii siyo siasa,siyo uchonganishi,siyo hasira kwa mtu fulani bali ni uzalendo

5. MWISHO..tetea nchi yako ndani ya AFRICA,tetea asili yako na uipende kwa dhati,kwa imani yako omba kwa ajili ya AFRICA,omba kwa ajili ya uongozi wa nchi yako na nchi zingine barani AFRICA.kataa kushikiwa akili

AKSANTE

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Back
Top Bottom