TANROADS yakanusha mti kulia ukikatwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Taarifa ya kuwapo kwa mti uliodaiwa kulia machozi ya damu wakati ukikatwa zimekanushwa na Meneja wa TANROADS mkoani hapa.

Meneja huyo wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Marwa Rubirya amesema habari za mti huo si za kweli na kuwa mti huo umeshakatwa.

"Huu ulikuwa uzushi hakuna kitu kama hicho sema kilichotokea ni kwamba mashine iliyopelekwa awali ilikuwa haina nguvu ikilinganishwa na ugumu wa mti huo,"amesema Rubirya

Hata hivyo aliwataka wananchi kuacha kuzusha mambo ambayo hayana ukweli na kuibua hisia zisizo na msingi wowote.
 
ujinga kweli kuna watu na akili zao kabisa wakaacha mambo ya msingi kwenda kushangaa huo mti mtu anatoka kazini anaishi nyegezi anaenda kushangaa mti iloganzala
 
Habari hizi za uzushi zinachangiwa sana na vyombo vyetu vya habari vinachangia pakubwa sana kusambaa habari za uzushi. Pia maafisa habari wa serikali wanachelwa sana kujibu mambo mbalimbali mpaka unakuta ule uwongo umesamba sana.
 
Ni mwanza eneo la Pansiasi, mti uligoma kung'oka kwa greda, walioshuhudia walnasema mti ulikuwa unaongea kwa kusema mnatutoa hapa mnatupeleka wapi? hiyo ilikuwa ni jana
 
Acha mi niwe mjinga Ila nilienda na greda lilishindwa kweli! Na sauti za ajabu ajabu zilikuwa zinasikika
 
Habari hizi za uzushi zinachangiwa sana na vyombo vyetu vya habari vinachangia pakubwa sana kusambaa habari za uzushi. Pia maafisa habari wa serikali wanachelwa sana kujibu mambo mbalimbali mpaka unakuta ule uwongo umesamba sana.
Yani waandishi wa habari vimeo sana,, kuna wakati nilimsikia jamaa anasema kwenye radio ilikuwa tukio la mtu kudondoka kutoka ghorofa ya juu ya jengo linalojengwa basi katika kuitimisha hiyo habari, akasema eti haya mambo ni lazima yatokee jengo lolote likiwa linajengwa usidhani maghorofa yanasimama bila kumwagwa damu!duhh wabongo imani za kishirikina zimeteka akili zetu sana.
 
Back
Top Bottom