TANROADS usingizi wa pono: barabara Salasala/Bagamoyo imejaa tope!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
18,173
13,776
Hapa mahali ni kero tupu.
Maungio ya barabara toka vilimani Salasala na Bagamoyo kwa karibu siku nne imekuwa tope tupu.

Mkandarasi aliyejenga hapo KONOIKE hawakufanya kazi nzuri hapo.

Makalavati ya kubeba maji toke vilimani Salasala ni madogo mno au hayapo kabisa.
Matokeo yake maji, tope, vipande vya miti hufurika barabarani kila mvua kubwa inyeshapo.
Baada ya hapo inakuwa kero ya kufa mtu, ahali hapapitiki na magari kukwama juu ya kami!!!

Kero inaendelea barabara ya Afrikana.
Maji ya mvua yanapoporomoka toka vilima vya Salasala yanakutana na vikaravati vidogo vinavyopitisha maji ya mto Ndumbwi toka Interchik.
Hapo ndo nasema TAROADS hawana wakaguzi wahandisi maana vikaravati hivi vya shule ya Msingi Afrikana vina vurugwa mara mbili au tatu kila mwaka hadi kupitika kwa taabu sana.

Lawama ziende kwa TAROADS ambao wako usingizini na hawajui la kufanya.
Hapo HAKUNA kazi tu.
 
Sehemu hixo mbili ni kero kubwa.
Juzi foleni pale Salasala/Bagamoyo ilienda mpaka Samaki Wabichi.
Na kule chini barabara ni kwa kupishana gari moja.
Wahandisi mpooo!
 
Wewe masopakyindi rudi kwenu makongolosi chunya ukawatetee Ndugu zako, huko wana shida sana, salasala unatafuta nini?,
 
Back
Top Bottom