TANROADS Ruvuma: Ziko wapi fedha za barabara ya Peramiho- Litumbandyosi - Kingole?

TANROADS Ruvuma: Ziko wapi fedha za barabara ya Peramiho- Litumbandyosi - Kingole?

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,959
Reaction score
876
Ndugu wana JF habari za Jumatatu

Barabara ya Peramiho – Litumbandyosi – Kingole ni barabara ya mkoa. Kila mwaka imekuwa inatengewa fedha za ukarabati na wazabuni wanapewa tenda ya barabara hii. Cha ajabu ni kuona haitengenezwi kwa miaka karibu 8. Ziko wapi fedha zinazotengwa kwa ajili ya barabara hii?

Ni maajabu ya Musa tu hadi leo hii, barabara hii inatengenezwa kwa jembe la mkono na wakazi wa kijiji cha Kingole. Mara ya mwisho barabara hii kutengenezwa kwa greda ilikuwa ni mwaka 2006. Hadi leo barabara hii ni shida kupitika. Gari inayokwenda kijiji hiki mwisho wake ni mwezi ujao.Kifuku kinavyokaribia wakazi wa kijiji hiki wanajua kabisa kuliona tena gari ni majaliwa.

Sasa nani anakula fedha ya barabara hii? Mfano katika msimu ulioisha mwezi June 2014 barabara hii ilitengewa jumla ya shilingi 524,110,000/= na mkandarasi aliyeshinda zabuni hiyo alikuwa ni Ovans Construction Ltd wa S.L.P 170 Mbinga. Mkataba ulisainiwa tarehe 27.8.2013 kwa makubaliano ungeanza tarehe 3.9.2013 na kumalizika tarehe 30.6.2014. Contract namba ya tenda ni AE/001/2013 – 14/RV/W/25/10. Fedha hizi zilikuwa zitengeneze barabara ya Paradiso hadi Litumbandyosi pia. Kilichotokea ni kuwa barabara ya Litumbandyosi hadi Kingole haijatengenezwa. Na huku ndiko wakuu wa TANROADS wanakokula pesa. Hakuna wa kusemea wala anayefuatilia.

Wakazi wa Kingole wakati Fulani waliamua kutengeneza wao kwa jembe la mkono lakini diwani wao James Stewart Yaparama aliposikia watu wake wamechukua uamuzi ule akaamua kwenda kuwasitisha akisema barabara hii imetengewa fedha, hivyo itatengenezwa. Diwani haishi kijijini hapo anaishi Songea. Hadi tunapoandika hakuna kilichofanyika na msimu umeisha. Barabara ni tabu tupu, huwezi kwenda na gari ndogo huko halitarudi. Nani nakula fedha hii kama si mzabuni na TANROADS kwa pamoja. Ndiyo wanakula.

Niingize siasa kidogo za kijiji hiki. Wakazi wa kijiji hiki ni wafuasi wa CCM wazuri sana. Na hawaoni tatizo na maisha ya aina ile ya kukosa hata usafiri wa uhakika wa kusafirisha mazao yao. Kila chaguzi zikifika wao wanachagua CCM na wakiona mtu ana mwelekeo wa upinzani wanamtafutia kosa na kumshitaki akaozee Kitai gereza la kilimo.
 
Muulize mbunge wao Wa peramiho na naibu Waziri Wa elimu na mafunzo ya ufundi ndugu Mh.jenister mhagàma kuwa kile kijiji hakupata kula ya CCM mwaka 2005? Na mwaka 2010?
 
Nategemea mbunge atengenezi budget na wala hana ella ya kkutengeneza barabara ,zaidi ni wizara ya ujenzi chini ya wakala wao TANROADS wa kuulizwa zaidi.Kwanini amuulizi Manager wa wakala TANROADS amekaa mda mrefu ndo kikwazo chunguza
 
Kwanini ruvuma barabara imekuwa ni ndoto kwa wananchi....especially tunduru...wana ukawa tuleteeni mbunge
 
Hivi wewe huoni miradi ya barabara inavyokwenda acha hizo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
kuna mpango wa barabara ya lami toka songea-masasi kama si tunduru nadhani.bado upo on progress sijafika siku nyingi but nadhani sasa imefika hadi namtumbo na zaidi.
upande wa mbinga nadhani sasa lami imeisha niliacha kipande kidogo mara ya mwisho kufika huko imepita hadi kigonsera na kupitiliza.dar songea hakuna usumbufu zaidi ya kuziba viraka nadhani ambavyo vingi viko iringa/njombe
 
Back
Top Bottom