Nafikiri Idara ya Mambo ya Kale walipaswa kuzingatia taratibu na sheria za kuweka mabango barabarani. Haijalishi kwamba watalii hawatajua kama kuna kitu cha kufanyia utalii hapo. Maana TANROADS wasipofanya hivyo, raia wengine nao watakuja na mabango yao hapo, kisa bango la idara hiyo limeachwa ili litangaze utalii.