TANROADS Mbona Hamjavunja Kituo cha Polisi Mbezi Louis?

Itzmusacmb

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
1,532
2,000
Wana jamvi hapa Dar es salaam maeneo ya Mbezi Louis TANROAD Imefanya zoezi la ubomoaji wa nyumba zote zilizo ndani ya Hifadhi ya Barabara ya Morogoro, ila leo nimepita wakati naenda Msoga "kula" Sikukuu ya Christmas nmeona kile kituo cha Polisi karibu na Kituo cha mafuta cha Camel oil kikiwa hakijavunjwa na kipo ndani yq Hifadhi ya barabara!!

Sasa nashangaa iweje Nyumba za pemben yake na nyuma yake zivunjwe na chenyewe kiachwe ilihali kipo ndani ya Hifadhi ya barabara?
Je sheria inatafsiri vp tukio la kituo kuachwa?TANROADS au yeyote mwenye uelewa anisaidie

NB:Naomba radhi sikupata nafasi ya kupiga picha

~Cmb
 
COPPER

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
2,122
2,000
Lazima kuna mipango inaendelea. Ni kweli kipo ktk road reserve na kimebanana sana. Naamini katika ujenzi wa Wilaya ya Ubungo suala la Polisi limezingatiwa sana.
 
mogulnoise

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
2,345
2,000
Kwani police walimzomea mkuu wakati wa kampeni?

Ile bomoa bomoa ya mbezi Luis ina elements za kulipiza kisasi kila mwezi wao tu wanabomolewa utazani wako Alepo Syria
 
Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
9,740
2,000
Wana jamvi hapa Dar es salaam maeneo ya Mbezi Louis TANROAD Imefanya zoezi la ubomoaji wa nyumba zote zilizo ndani ya Hifadhi ya Barabara ya Morogoro, ila leo nimepita wakati naenda Msoga "kula" Sikukuu ya Christmas nmeona kile kituo cha Polisi karibu na Kituo cha mafuta cha Camel oil kikiwa hakijavunjwa na kipo ndani yq Hifadhi ya barabara!!

Sasa nashangaa iweje Nyumba za pemben yake na nyuma yake zivunjwe na chenyewe kiachwe ilihali kipo ndani ya Hifadhi ya barabara?
Je sheria inatafsiri vp tukio la kituo kuachwa?TANROADS au yeyote mwenye uelewa anisaidie

NB:Naomba radhi sikupata nafasi ya kupiga picha

~Cmb
Mijitu mijambazi utaijua tu, mara nyingi majitu ya namna hii hayapendi polisi, unataka kituo kivunjwe ili uibe vizuri sio!
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
17,654
2,000
Hata ingekuwa zahanati isingevunjwa huduma ziendelee kwanza.

Kuvunjwa kitavunjwa tu.ila sababu ni kituo cha huduma lazima kiwekwe kiporo kwanza.
 
H1N1

JF-Expert Member
May 29, 2009
4,218
2,000
Hata ofisi za CCM Mbezi Luis wamezinguka.wamevunja mabanda yanayozunguka Lakini yenyewe wameiacha
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom