TANROADS hawana uwezo wa kudesign barabara nzuri kama za Kenya?

Ilipoanza kujengwa mlilalamika sana na kusema hamtaki maendeleo ya vitu mnataka ya watu
 
Watu wanaowaza posho na kujineemesha wajenge barabara za kudumu na kuepusha matatizo kwa miaka 50 kweli?

Hujui kuwa mwisho wa uwezo wao kufikiri ndo kula yao?

Mbagala - Posta tu wamejenga barabara mpya za njia mbili mbili kila upande (kumbuka kwenye jiji la watu Mil 6) alafu katika kuingia posta kutoka mbagala wameweka njia moja moja kabisa kwa kila upande alafu ndo unasema una wakala wa barabara katika karne hii ya 21?

Nchi hii tuwarudishie wazungu tu waendelee kututawala.
Kuna jamaa juzi tu ametoka kuongea hii issue kijiweni hii serikali ya hovyo sana
 
1.kwanza anaedesign barabara si tanroads ni maconsultant mfano mwendokasi imekua design na tanconsult..Tanroad yeye ni clients

2. Tanroads hushirikiana na consultant kuiba hela na njia wanayotumia ni kwenye variations

3.lakini consultant huchukua rushwa pia kwa contractor na Tanroad pia hichukua hela kwa contractor

4.kwa hiyo mwishoni huwa wanabadili michoro na kujenga hizo flyover palipotakiwa kujengwa interchange

5.mfano mzuri ni interchange ya ubungo gharama zilizidi ikabidi mchoro ubadilishwe mara tatu wakisingizia gharama zimeongezeka

6.wanasiasa pia hushirikiana na mkandandarasi kula hela ya serikali...hapa wao wanamsaidia kupata kazi then wao hupewa 1 to 5% ya hela mzima wa mradi

7.hapa yumo waziri na circle ya viongozi wachache wa juu...umafia unaofanyiaka hapa unategemea kiongozi wa juu yupo na kampuni gani
Sasa kwanini wanasheria wetu wasiwe wanawashtaki hawa wakandarasi wanaotuharia nchi kama wao ndiyo moja ya sababu ya haya yote
 
Ninachofahamu ni kuwa Tanroads hafanyi mwenyewe design isipokuwa anatumia Mkandarasi Mshauri yaani Consultant


Mkandarasi Mshauri ana-design kutokana na mahitaji ya Client ambaye ni Tanroads

Lakini tunajua kuwa Tanroads anafanya kazi kwa niaba ya Serikali maana ndiyo mtoa fedha

Sasa vipi iwapo mtoa fedha amepelekewa Mahitaji ya fedha ya kujenga barabara ya njia 8 lakini akasema nina hela ya kujenga njia 4?

Huyo Tanroads atatoa wapi fedha ya kujenga hizo njia 4 nyingine?

Kuhitimisha hili ni kuwa tusiwape lawama Tanroads bila kuangalia upana wa jambo lenyewe maana gharama za kujenga barabara ya njia mbili yaani 2-lanes ilifikia shilingi bilioni 1.6 kwa kila kilomita moja.

Imagine unajenga barabara ya kilomita 20 kwa Lane 8 itakuwa shilingi ngapi?


Tujikune Mkono unapofikia
Sasa we unaona sahihi kikundi cha watu wachache kigawane billion 500 za kifisadi ama hizo hela zielekezwe kwenye ujenzi wa taifa?
 
Bongo huwezi kutana na watu wa mamlaka wanaotumia akili inapopaswa kutumia akili...

Mbezi Mwisho pale tu kuweka zile over pass ilikuwa ni baada ya kupigiwa kelele...
Wakitatua kila tatizo watakosa vya kupigia kampeni. Wimbo ni fedha hamna ila anasa zinafanyika za kununua kila toleo la Landcruiser 😂
 
Mambo ya tanzania ukifuatilia unaweza kujikata pumbu bure kwa hasira bora tuenddlee kula tu mbususu
 
Umesema sahihi

Suala la kupungua kwa maadili limechangia pakubwa kufikia huku.

Ndiyo maana leo hii barabara yenye design life ya miaka 20 unakuta baada ya miaka 5 tu unakuta imeshaanza kuzibwa Viraka
Mkuu wewe ni Mhandisi? Unajua 10% of road is allowed to perform unsatisfactorily hata kama Ina week?
 
Nilichojifunza kwenye huu Uzi watu wasio wa Fani Husika huwa kimbelembele sana kukosoa Fani zingine.
 
Mkuu wewe ni Mhandisi? Unajua 10% of road is allowed to perform unsatisfactorily hata kama Ina week?
Ndiyo Mkuu ....

Hiyo allowances inaruhusiwa japo hatutegemei kutokea mapema hivyo

Angalia kipande cha barabara kutoka Igawa pale Mbeya hadi Makambako kilivyo kizuri

Hii ina implies kuwa quality met during construction

Then angalia kipande cha barabara kutoka Iringa hadi Dodoma kupitia Mtera kilivyo kibovu

Nachotaka kusema ni kuwa 10% inachangia pakubwa sana kwenye kudhoofisha miundombinu yetu kabla ya wakati
 
Back
Top Bottom