Tanroads barabara ya Samaki Wabichi - Mbezi Juu - Goba - Kimara/Mbezi Louis iangaliwe

Sendeu

Member
Jun 29, 2009
59
2
Ndugu zanguni sisi wakazi wa maeneo tajwa hapo juu kero na shida tunayoipata ya usafiri kwenye hii barabara ni mungu tu anaejua maana tunaishi kama vile tuko porini ilhali sisi ni walipa kodi wa nchi ya TZ na kodi zetu zinakatwa kwenye mishahara,kwenye matumizi nk.

Tunaomba japo greda tu la kufukia mashimo kwenye barabara hii kwa sababu tunajua mchakato wa lami bado ni mrefu kwa nchi hii jinsi ilivyo na urasimu.

Ningeshauri pia japo kila gari inayopita kwenye barabara hiyo itozwe japo sh. 500/=ili barabara itengenezwe pawepo na kizuizi cha kuchangisha mchango huo ili barabara iwekwe kifusi km kweli serikali imeshindwa kuweka hicho kifusi.

mhe.Magufuli au Mwakyembe ukitoka Dodoma kwenye semina elekezi jaribu kupita kwenye barabara hiyo ukitokea Mbezi au Kimara Temboni hadi Samaki Wabichi (Tank bovu) uone mwenyewe jinsi hali ilivyo mbaya.

wabunge mh. Mnyika na Mdee pigeni kelele hii barabara iwekwe kifusi na ishindiliwe kwani hii inaunganisha majimbo yenu yote mawili Ubungo na Kawe.

Bosi wa Tanroads mkoa Mh. Nyabakari tupia macho hili tatizo.

Bosi wa Tanroads mh. Mfugale Patrick tafadhali tumia busara zako kuwezesha japo kifusi kwenye barabara hii-tuna imani na wewe sana tunajua hutatuangusha

nawasilisha Asanteni!!!!!
 
Back
Top Bottom