TANROAD Dsm, tengenezeni barabara ya Mbezi Mpiji-Magohe

jingojames

JF-Expert Member
Mar 12, 2010
887
451
Kwa wakala wa Barabara-TANROAD, DSM!

Haya ni malalamiko na kilio cha wakazi wa Kata ya Mbezi ambao wengi wanatumia Barabara hii kwa muda mrefu barabara hii imekuwa haifanyiwi matengenezo ya mara kwa mara(periodic maintenances) na hivyo kuwa katika hali mbaya sana ktk kipindi chote cha mwaka na kupelekea mamia ya watumiaji wa barabara hii kuteseka kwani magari ya abiria yanagoma kupita njia hiyo na hata wananchi wanaotumia magari yao binafsi yanapata itilafu kila siku kwasababu ya ubovu wa barabara hiyo!

Watumiaji wa Barabara hii tunaomba Wakala wa Barabara -mkoani DSM wampe Mkandarasi mwenye utalaamu ,uwezo na vifaa hili ukarabati unaofanyika uwe ni wa uhakika na serikali na wananchi waone value of their money!

cc: Waziri Wa Ujenzi Mhe.Makame Mbarawa.
cc: Mkurugenzi Mkuu-TANROAD.
 
Tatizo nililogundua ni wakandarasi wanaojenga hizi barabara za ndani!! Wanajenga "dispozabo roads" haiwezekani barabara za lami zichimbike kwa mvua!!

Huu ni uhuni wa hali ya juu!! Barabara zingine zina miaka miwili tu ila baada ya msimu wa mvua hazipitiki teena!! Zina vishimo vya kuchezea "mdako" vya hatari.

Kandarasi za kiTZ hazina maana kabisa
 
Back
Top Bottom