Tano Bora ya wabunge wazalendo kwa taifa letu!

Tano Bora ya wabunge wazalendo kwa taifa letu!

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
4,210
Reaction score
556
Habarini wana jf, kwa hali ya mambo inayoendelea katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni wazi kuwa wabunge wengi wamepoteza sifa ya uwakilishi kwa wananchi katika jengo lile la bunge mjini dodoma, wabunge wengi wameonekana kuwa wasemaji wa serikali na si wa wananchi! Kufuatia hali hiyo kwa uchunguzi wangu usio rasmi, nimegundua wako baadhi ya wabunge wachache bado wana moyo wa uzalendo kwa wananchi na taifa lao kiujumla! Wafuatao ni wabunge watano bora kwa uzalendo na utumishi uliotukuka kwa wananchi wao waliowatuma bungeni:

1. Mh. Tundu Lissu(chadema)-singida mashariki.
2. Mh. John Mnyika(chadema)- Ubungo.
3. Mh. Deo Filikunjombe(ccm)-Ludewa
4. Mh. Kangi Lugora(ccm)-Mwibara.
5. Mh. Halima mdee(chadema)-kawe!

Pongezi ziende kwa wananchi waliotuchagulia wabunge hao, pia pongeze ziende kwa waheshimiwa wahusika! Mungu awalinde na kuwapa baraka zake! Nawasilisha.
 
Nakuunga mköno, lakini naona namba 1 na 2 wangekuwa namba 3 na 4, zaidi ya hapo, namba tano ungeweza kumpa Ester bulaya, any way nadhani umejitaidi kuangalia kwa umakini!
 
Nakuunga mköno, lakini naona namba 1 na 2 wangekuwa namba 3 na 4, zaidi ya hapo, namba tano ungeweza kumpa Ester bulaya, any way nadhani umejitaidi kuangalia kwa umakini!

Esta bulaya anataka jimbo hataki tena vitu maalum kwa hiyo asiingie mchakatoni mpaka tumuone atakapo kuwa rasmi. Nawasilisha.
 
Ni kweli kwamba uliowataja wanafaa kwenye top 5. Lakini Godbless Lema angetakiwa kuwa mzalendo namba moja, ni kiongozi ambaye ameonyesha kwa vitendo kuwatetea wanyonge. Amedhiriki hata kuyaweka rehani maisha yake kwa ajili ya wanyonge, amewekwa ndani kwa kuonewa, lakini hajakata tamaa.
 
Tumepokea pongezi zake nasi tutaendelea kuwatetea watanzani na Tanzania yenyewe mpaka ukombozi wa nchi yetu utakapopatikana.
UMK, kny wabunge waliotajwa.
 
Lema awemo pia na hata ZZK ingawa ni kigeugeu na kama pandikizi vile!ana report kwa JK moja kwa moja labda kama miaka 2 hii wamepingana kwenye mitazamo!
 
sitowapongeza wabunge mpaka pale ubunge iwe ajira ya kujitolea ndio tutajuwa kama kweli wanakwenda bungeni kutuwakilisha sisi walala hoi vyenginevyo ubunge ni njia ya mkato wa wizi wa waTZ
 
Mawazo yenu ya kibavicha mnakuja kutuwekea hapa kwanini msikutane huko mkapeana pongezi zenu kuliko kuchafua jukwaa letu?
 
Umekosea kuweka maccm hayachelewi kubadilika anyway ni mtazamo wako

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nadhani kila mmoja angeandika tano bora wake baadaye tutaona mwenye kura nyingi zaidi
 
Lema awemo pia na hata ZZK ingawa ni kigeugeu na kama pandikizi vile!ana report kwa JK moja kwa moja labda kama miaka 2 hii wamepingana kwenye mitazamo![/QUOTE ] mkuu,naunga mkono, lakini kwa top five, kwenye uzalendo naona zitto hayupo, zitto kuna baadhi ya mambo anayumba!
 
Mawazo yenu ya kibavicha mnakuja kutuwekea hapa kwanini msikutane huko mkapeana pongezi zenu kuliko kuchafua jukwaa letu?
Thibitisha kama mi ni Bavicha, pili muda wote usiwaze masuala ya vyama tu, pia wazia na uzalendo katika taifa letu, tatizo watanzania wengi wamelewa uvyama kiasi kwamba umoja,mshikamano wa taifa letu unawekwa rehani! Ndugu tanzania kwanza, mengine baadae!
 
Mimi naona wabunge wazalendo ni 1. Edward Lowassa 2. Andrew Chenge 3. Stephen Wassira 4. John Shibuda 5. Mwigulu Nchemba.
 
kama ze future prez mh Zitto hayumo, list hiyo ionyeshe familia yako.

Lissu hana kitu cha kuonyesha
 
1: G. LEMA, 2: T. LISU, 3: J MNYIKA, 4: F MBOWE, 5: K LUGOLA 6: ESTER BULAYA, 7: H MDEE, 8:MSIGWA 9😀 FILIKUNJOMBE, 10: E WENJE. Hiyo ndo ten best. Nahisi mtahoji kwa nini cja muinclude Z KABWE?.Sababu ni kwamba huyu jamaa ananunulika kirahisi mno, kwa hiyo cyo mtu wa kumuamini.ILA AKIJILEKEBISHA ANAWEZA KUWA MTETEZI MZURI WA WATANZANIA.
 
Mimi naona wabunge wazalendo ni 1. Edward Lowassa 2. Andrew Chenge 3. Stephen Wassira 4. John Shibuda 5. Mwigulu Nchemba.
...hii nadhani ni tano bora kutoka chini - umemsahau stella Manyanya -kachakachuliwa mpaka kamsahau Yesu siku hizi. Getrude Lwakatare naona anamkana Yesu kimyakimya hajauonyesha umma waziwazi kama Manyanya-
 
Back
Top Bottom