Tanker KC-135 Yaanguka huko Iraq-CENTCOM yatangaza!!

Tanker KC-135 Yaanguka huko Iraq-CENTCOM yatangaza!!

Echolima1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
6,929
Reaction score
6,029
Ndege ya kijeshi ya Marekani ya kujaza mafuta angani, KC-135 Stratotanker, imeanguka magharibi mwa Iraq Alhamisi, jeshi la United States Air Force limesema.

Jeshi hilo limeeleza kuwa tukio hilo halikusababishwa na mashambulizi ya adui wala makosa ya vikosi vyao, bali lilihusisha ndege nyingine ya Marekani ya aina hiyo. Afisa mmoja wa Marekani ameiambia CNN kuwa angalau wafanyakazi watano walikuwa ndani ya ndege hiyo wakati ilipoanguka.

Kwa mujibu wa taarifa ya United States Central Command, juhudi za uokoaji zinaendelea lakini haijaelezwa kama kuna wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa au kupoteza maisha.

Taarifa hiyo ilisema tukio hilo lilitokea katika anga salama wakati wa operesheni ya kijeshi inayoitwa Operation Epic Fury, ambayo ni jina lililotumiwa na Pentagon kwa operesheni za Marekani dhidi ya Iran.

Taarifa iliongeza kuwa ndege mbili zilihusika katika tukio hilo, ambapo moja ilianguka magharibi mwa Iraq na nyingine ilifanikiwa kutua salama. Jeshi limesisitiza kuwa tukio hilo halikusaabishwa na mashambulizi ya adui wala makosa ya vikosi vyao.

Source: CNN

Screenshot_20260313-044533_Google.jpg
Screenshot_20260313-044432_Google.jpg
IMG_20260313_044125_317.jpg
 
Sawa Imeanguka Tu ?
Unataka watoe majibu kwa nini imeanguka bila kufanya uchunguzi?
Umefakamia daku umeshiba sasa umeanza kuuliza Maswali Uchwara yasiyo na maana wakati taarifa ipo hapo nimekuwekea!!!
 
Ndege ya kujaza mafuta angani Tanker KC-135 imeanguka huko Iraq ikiwa kwenye Operation kuzijazia mafuta ndege vita zinazoishughulikia Iran,

Shughuli za uokozi zinafanyika CENTCOM wameeleza!!
Imekuwaje ikaanguka !!!!?

uyo Trump kakusanya pesa za Tozo nakuja kuzitupa middle east ¿¿¿

Uchaguzi upo mbele yake. Putin sijui atafanyaje kulibeba ili Zeeee kabla ya Uchaguzi wa Mabunge yao,.

Majuto mjuu!! chuki zake zinamtokea puani!!
 
Endeleea kuteseka!!!

Mada ni kuanguka kwa ndege wewe umeanza kulia-lia utafikiri na ni Mmarekani!!

Pole kwa mateso hayo!!
 
Unataka watoe majibu kwa nini imeanguka bila kufanya uchunguzi?
Umefakamia daku umeshiba sasa umeanza kuuliza Maswali Uchwara yasiyo na maana wakati taarifa ipo hapo nimekuwekea!!!
Hahahaha yaani ndege ya 4 sasa imeanguka ila zote eti ni ajali au friendly fire!! Meli imeungua mmedai ni hitilafu!! Hauoni kuna something weird.
 
Back
Top Bottom