Tanker KC-135 Yaanguka huko Iraq-CENTCOM yatangaza!!

Hahahaha yaani ndege ya 4 sasa imeanguka ila zote eti ni ajali au friendly fire!! Meli imeungua mmedai ni hitilafu!! Hauoni kuna something weird.
Kwa hiyo unaraka kutumia hisia Iran imeiangusha ndege hiyo huko Iraq?

Jiulize kwa nini wasiangushe wimbi la ndege zinazoshambulia miundombinu huko irani?
 
Attachments

  • IMG_20260313_142046_316.jpg
    IMG_20260313_142046_316.jpg
    139.5 KB · Views: 2
Kwa hiyo unaraka kutumia hisia Iran imeiangusha ndege hiyo huko Iraq?

Jiulize kwa nini wasiangushe wimbi la ndege zinazoshambulia miundombinu huko irani?
Ndege ya 4 hii ambazo zilikua zinashambulia iran kutokea anga la Iraq, ila zote mmesema zimedunguliwa either na jeshi rafiki ama ajali binafsi tu!!

Nadhani majibu unayo mpaka hapo.
 
Ndege ya kijeshi ya Marekani ya kujaza mafuta angani, KC-135 Stratotanker, imeanguka magharibi mwa Iraq Alhamisi, jeshi la United States Air Force limesema.

Jeshi hilo limeeleza kuwa tukio hilo halikusababishwa na mashambulizi ya adui wala makosa ya vikosi vyao, bali lilihusisha ndege nyingine ya Marekani ya aina hiyo. Afisa mmoja wa Marekani ameiambia CNN kuwa angalau wafanyakazi watano walikuwa ndani ya ndege hiyo wakati ilipoanguka.

Kwa mujibu wa taarifa ya United States Central Command, juhudi za uokoaji zinaendelea lakini haijaelezwa kama kuna wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa au kupoteza maisha.

Taarifa hiyo ilisema tukio hilo lilitokea katika anga salama wakati wa operesheni ya kijeshi inayoitwa Operation Epic Fury, ambayo ni jina lililotumiwa na Pentagon kwa operesheni za Marekani dhidi ya Iran.

Taarifa iliongeza kuwa ndege mbili zilihusika katika tukio hilo, ambapo moja ilianguka magharibi mwa Iraq na nyingine ilifanikiwa kutua salama. Jeshi limesisitiza kuwa tukio hilo halikusaabishwa na mashambulizi ya adui wala makosa ya vikosi vyao.

Source: CNN

View attachment 3557292View attachment 3557293View attachment 3557294
Sio kuanguka imeangushwa na Pro Iran
 
Unataka watoe majibu kwa nini imeanguka bila kufanya uchunguzi?
Umefakamia daku umeshiba sasa umeanza kuuliza Maswali Uchwara yasiyo na maana wakati taarifa ipo hapo nimekuwekea!!!
Nadhani wewe ndiye hujamwelewa huyo mkuu kutaka sababu ya kuanguka kwa hiyo ndege review zile jet 3 zilizondoka kule kuwait mapilot wakaeject nazo walisema hazikulengwa na adui blah blah kibao.
 
Ndege ya kijeshi ya Marekani ya kujaza mafuta angani, KC-135 Stratotanker, imeanguka magharibi mwa Iraq Alhamisi, jeshi la United States Air Force limesema.

Jeshi hilo limeeleza kuwa tukio hilo halikusababishwa na mashambulizi ya adui wala makosa ya vikosi vyao, bali lilihusisha ndege nyingine ya Marekani ya aina hiyo. Afisa mmoja wa Marekani ameiambia CNN kuwa angalau wafanyakazi watano walikuwa ndani ya ndege hiyo wakati ilipoanguka.

Kwa mujibu wa taarifa ya United States Central Command, juhudi za uokoaji zinaendelea lakini haijaelezwa kama kuna wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa au kupoteza maisha.

Taarifa hiyo ilisema tukio hilo lilitokea katika anga salama wakati wa operesheni ya kijeshi inayoitwa Operation Epic Fury, ambayo ni jina lililotumiwa na Pentagon kwa operesheni za Marekani dhidi ya Iran.

Taarifa iliongeza kuwa ndege mbili zilihusika katika tukio hilo, ambapo moja ilianguka magharibi mwa Iraq na nyingine ilifanikiwa kutua salama. Jeshi limesisitiza kuwa tukio hilo halikusaabishwa na mashambulizi ya adui wala makosa ya vikosi vyao.

Source: CNN

View attachment 3557292View attachment 3557293View attachment 3557294
Imeanguka
Imeangushwa
 
Kwa hiyo unaraka kutumia hisia Iran imeiangusha ndege hiyo huko Iraq?

Jiulize kwa nini wasiangushe wimbi la ndege zinazoshambulia miundombinu huko irani?
Vipi zile jet 3 zilizoangushwa kule kuwait nazo zilikuwa tatizo la kiufundi au hali ya hewa😂
 
Ndege ya 4 hii ambazo zilikua zinashambulia iran kutokea anga la Iraq, ila zote mmesema zimedunguliwa either na jeshi rafiki ama ajali binafsi tu!!

Nadhani majibu unayo mpaka hapo.
Iran hajaangusha ndege ya Israel hata moja!!!
 
Vipi zile jet 3 zilizoangushwa kule kuwait nazo zilikuwa tatizo la kiufundi au hali ya hewa😂
Iran haijawahi kuangusha ndege ya Israel hata moja na kama kuna siku wataweza basi mitandaoni watu siku hiyo hawatalala na picha za hiyo ndege zitasambazwa sana sana.

Kwa ujumla Iran Hana uwezo wa kudungua ndege- vita za Israel labda wazi dengue kwa Hisia tu basi!!
 
Imeanguka
Imeangushwa
Kwa Maneno mnaruhusiwa kuiangusha hiyo ndege!!
Hata huyo waziri Mkuu wa Israel mlimuua kwa Maneno bado tu hamjatutangazia mazishi yake kwa maneno.

Hata kama iwe Imeangushwa na Iran inakuwaje ikaangukie Iraq? Maswali kama haya Mabumunda kama wewe hamuwezi kujiuliza!!
 
Nadhani wewe ndiye hujamwelewa huyo mkuu kutaka sababu ya kuanguka kwa hiyo ndege review zile jet 3 zilizondoka kule kuwait mapilot wakaeject nazo walisema hazikulengwa na adui blah blah kibao.
Ndege-vita 3 hiyo ilikuwa friendly-fire kitu ambacho ni kawaida kwenye vita kwa akili yako unataka kutuaminisha Iran alizidungua? Jiulize kwa nini ziliangukia Kuwait? Tumieni akili zenu vizuri siyo kulialia Kufuga Midevu na Majini tu
 
Sawa mkuu Sibishani na mjinga! Kwa hiyo na hizo ndege za kujaza mafuta zilizolipuka zikiwa kwenye runway ilikuwa ni friendly-fire? Achana na zilizodunguliwa nazo tuseme ni friendly-fire. Nakuomba cease fire nayo ni friendly-fire? Huyo Trump wako haeleweki kama wewe usivyoeleweka. Babu yako Netanyahu yupo wapi? Wamerusha footage akiwa anavidole 6😂😂😂😂! Pathetic
 
Iran haijawahi kuangusha ndege ya Israel hata moja na kama kuna siku wataweza basi mitandaoni watu siku hiyo hawatalala na picha za hiyo ndege zitasambazwa sana sana.

Kwa ujumla Iran Hana uwezo wa kudungua ndege- vita za Israel labda wazi dengue kwa Hisia tu basi!!
Sawa mkuu Netanyahu
 
Back
Top Bottom