Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411

Askari wa mamlaka ya bandari mkoa wa Mtwara kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa imefanikiwa kukamata Korosho tani 29 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 80 zilizokuwa zimeingizwa bandarini kinyume na utaratibu ili kusafirishwa nje ya nchi, huku vibali vya usafirishaji vikionyesha si halali.
Akizungumzia tukio hilo kaimu meneja wa bandari mkoa wa Mtwara Juma Kijavara amesema Korosho hizo ziligunduliwa na askari wa mamlaka ya bandari majira ya saa mbili usiku baada ya mihuri iliyopigwa kwenye vibali vya kusafisha Korosho kuonyesha si halali na hivyo kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya mkoa.
Kufuatutia tukio hilo mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akiambatana na kamati yake ya ulinzi na usalama ya mkoa walifika eneo la bandari ili kudhibitisha tukio hilo, huku kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara George Salala amesema wanawashilikia watu sita pamja na magari yaliyotumika kusafirisha Korosho hizo.
Hata hivyo kamanda amesema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na kuaidi kutoa taarifa rasmi hapo baadae, huku akiomba bandari, TRA, na wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kukomesha biashara ya kangomba ambayo inanyonya wakulima, sambamba na kuikosesha serikali mapato.
Chanzo: ITV