Tangu nifike Mjini miaka mingi iliyopita sijawahi kushuhudia mgao mkali wa umeme kama huu unaoendelea leo

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Tangu nifike Mjini miaka mingi iliyopita sijawahi kushihudia MGAO mkali wa UMEME kama huu unaoendelea leo.
Ni ovyo, ovyo, ovyo kabisa. Zamani nilikuwa nawatetea sana viongozi wa Serikali lakini kwa sasa, Hapana.

Wamefeli kwa kiwango ambacho hakijawahi kuwepo huko nyuma. Hawana jipya tena.

Allah Akbar.
 
Kutomasa ni kiswahili cha 1980s mkiingia Sinema za X pale Avalon au Empire ndio Wapendanao hutomasana!
Hakuna mgao ila kuna upungufu wa umeme
 
Tangu nifike Mjini miaka mingi iliyopita sijawahi kushihudia MGAO mkali wa UMEME kama huu unaoendelea leo.
Ni ovyo, ovyo, ovyo kabisa. Zamani nilikuwa nawatetea sana viongozi wa Serikali lakini kwa sasa, Hapana.

Wamefeli kwa kiwango ambacho hakijawahi kuwepo huko nyuma. Hawana jipya tena.
Allah Akbar.
Zamani uliwatetea kwa lini?
 
Subirini tumalize mzigo wetu wa magenereta tuliteseka sana kipindi Cha mwendazake Sasa ni zamu yetu kuweni wapole

Kutesa Kwa zamu
 
Halafu unaambiwa TANESCO imepata faida kwa mara ya kwanza huku ikiwa kwenye mazingira hayahaya ya mgao wa 12hr/siku.😁.

Kale kajamaa hovyo sana, gharama za kuunganisha ndiyo zimegeuka chanzo kikuu cha mapato na hazishikiki.
 
Tangu nifike Mjini miaka mingi iliyopita sijawahi kushihudia MGAO mkali wa UMEME kama huu unaoendelea leo.
Ni ovyo, ovyo, ovyo kabisa. Zamani nilikuwa nawatetea sana viongozi wa Serikali lakini kwa sasa, Hapana.

Wamefeli kwa kiwango ambacho hakijawahi kuwepo huko nyuma. Hawana jipya tena.
Allah Akbar.
Mto Ruaha una maji mengi yanatiririka, Mtera na Kidatu maji yamejaa sijui shida iko wapi
 
Mambo yalianza kuharibika pale mama mwenye nyumba alipoamua kwenda kuokota maharage ya Mbeya yaliyo ungua na kutupwa jalalani na baba mwenye nyumba Kisha kuyakabidhi kwa bwana kipara ngwidu kwa ajili ya kuandaa chakula cha familia, kilichofuata baada ya pale ni kuumwa matumbo tuu 🚶🚶🚶🚶
 
Kazi ya serikalj ni nini? Umeme,maji, mafuta, mfumuko wa bei, tozo, bandari, rushwa, kila sehemu ukiangalia ni kama hakuna serikali.
Kwa hiyo we unaona kuna serikali? Serikali gani isiyojali watu wake sasa?
 
Nadharia ya uwiano kati ya ngivu ya utashi na ugavi hapo sasa ndipo inapoweza kudhihirika. Hapa nguvu ya utashi wa umeme ni kubwa mno wakati nguvu ya ugavi ni ndogo sana.

Nguvu ya utashi inazidi kuwa kubwa sana wakati upande wa uzalishaji ambavyo ndiyo pekee katika kuchochea ugavi wa umeme imejaa propaganda za kisiasa, ubabaishaji, ufisadi, uzembe, ujuaji, kukosa umakini, hujuma, "mismanagement" na kila aina ya uchafu unaoweza kuufikiria.

Katika kipindi cha amani JWTZ linaweza kupewa jukumu la kusimamia uzalishaji wa miradi mikubwa ya nishati ya umeme ili kupunguza longolongo nyingi za kisiasa. Wataalamu na mainjinia waliopo jeshini wanaweza kuwa ndiyo wasimamizi wakuu wa uzalishaji tu ili TANESCO ibakie na jukumu la usambazaji tu.
 
Mambo yalianza kuharibika pale mama mwenye nyumba alipoamua kwenda kuokota maharage ya Mbeya yaliyo ungua na kutupwa jalalani na baba mwenye nyumba Kisha kuyakabidhi kwa bwana kipara ngwidu kwa ajili ya kuandaa chakula cha familia, kilichofuata baada ya pale ni kuumwa matumbo tuu
Baada ya dakika chache familia yote ikapanga foleni kwenda msalani.
 
Ina maana ulikua nje ya nchi mbona wenzio tushazoea na ww endelwa kuisifia wenzio tuna mengi ww umeme nao kwako leo tu wenxio tunakatiwa daily
 
Mto Ruaha una maji mengi yanatiririka, Mtera na Kidatu maji yamejaa sijui shida iko wapi
Issue si kupungua kwa maji. Tatizo ni kikundi kidogo ambacho kimembana Bibie kwapani, hivyo hawezi kutoa maamuzi yoyote yale tofauti na matakwa ya kikundi hicho.
 
Back
Top Bottom