Tanesco Kama mnaandaa hoja za kupiga dili kupitia mradi wa dharula wa kuzalisha umeme nazani mlishapata. Choteni mahela mtutoe kwenye mgao huu mkali.

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Kwanza hii nchi inawasomi wa kutosha. Inamaana hawakujiandaa kabisa kwa chochote kuhusu umeme maji yakipungua? Kwa uzoefu mgao ukiwa mkali hivi ujue Kuna Jambo linatafutwa. Mikataba ya haraka haraka ya Bei juu iliyojaa utata inataka kupitishwa ili watu wapige mahela. Kila kitu kimekamilika Sasa. Mgao mkali kuwahi kutokea tokea napata akili. Hii Sasa hapana.
Kama Kuna Iptl mpya au Richmond au Escrow pitisheni chap maana huku uchumi wa masikini unakufa.
Vivyozi hatunyoi, barafu hazigandi, samaki wanaoza.
Kabla ya Richmond tuliambiwa mabwawa hayatajaa hata mvua inyeshe mfululizo masika na kiangazi kwa miaka 10. Na Mungu alivyo fundi mvua iliponyesha mwezi 1 tu kidogo mabwawa yapasuke.
 
Back
Top Bottom