Tangu ianze kauli mbiu ya elimu bure binafsi sijaona manufaa yoyote katika hili maana hali imekuwa mbaya sana

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Kwa kweli tangu ianze hii kauli "mbiu ya elimu bure" binafsi sijaona manufaa yoyote katika hili maana hali imekua mbaya sana hasa hasa vijijini.

Tangu hii sera ianze kutekelezwa nchini kumekua na changamoto nyingi sana hasa hasa kwenye suala zima la miundombinu thabiti itakayomwezesha mwanafunzi kupata elimu bora na si bora elimu.

Tangu kuanzishwa kwa sera hii...kumekuwa na changamoto ya vyumba vya madarasa, maabara na hata maktaba. Huwezi amini kuna baadhi ya shule vyoo ni vichache sana kulinganisha na idadi ya wanafunzi.

Licha ya changamoto ya miundombinu, eneo jingine ambalo linachangamoto ni upate wa rasilimali watu. Shule nyingi hasa hasa za vijijini hakuna walimu wakutosha..hii ni kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.

Huwezi amini kuna shule hazina walimu kabisa...halafu cha kushangaza walimu wengi waliohitimu vyuo vikuu wako mitaani wanauza vocha na soda! Huu ni upuuzi wa hali ya standard gauge!

Katika hili serikali ijitafakari kwa kweli yaani haiwezekani serikali ishindwe kujenga madarasa, wananchi wajitolee kujenga halafu walimu hakuna...

Hii issue ya Songea imeniumiza sana....yani serikali ishindwe kujenga miundombinu wananchi wajenge....halafu shule ifungwe kisa hakuna walimu kweli?

Halafu mtindo wa kutuchukulia walimu wetu wa vyuo nakuwafanya viongozi wa siasa huo ni umama. Sasa serikali inategemea watafiti watatoka wapi?

Mwisho, serikali inatakiwa ifute elimu bure kama haina uwezo wa kuajiri na kuhudimia wananchi ipaswavyo.

Serikali iache kuhamisha walimu wa sekondari kwenda kufundisha shule za msingi wakati kuna walimu wengi wa shule ya msingi mtaani na pia kuna shule nyingi hazina walimu hata hao wa arts.

Halafu naomba ipitishwe sheria au utaratibu wa watoto wote wa viongozi kuanzia mtaa hadi raisi wasomee shule za umma...hivyo ndivyo serikali ya wanyonge inapaswa kua.

WENU KATIKA UJENZI WA NCHI
Nebuchadinezzer.

ASANTENI

ASANTENI
 
Post muwafaka, kuna wale vijana waliokua wako vyuoni kusomea ualimu, mara wakaachishwa masomo kwa sababu sikuzielewa. Vipi hatma yao, ikiwa shule zinafungwa kwa kukosa walimu. Nilifikiri, ulikua uamuzi wa haraka. Warudishwe vijana shule wamalizie. Tunasikia sifa kaongeza wanafunzi milioni mbili. Lakini wakati huo huo kafukuza walimu waandaliwa 700. Matarajio yalikua nini?
 
Daah umeongea kwa hisia kali sana mkuu....

Cha kuelewa hakuna kitu Cha bure, kila kitu kina gharama zake. Binafsi nimesoma shule za serikali kipindi hicho ada ilikuwa elfu 20 O level na 70 A level bado ilikuwa inatumika pesa nyingi kwenye mambo mengine kama tuition, vitabu, madawati na uniform.

Ukihamini elimu bure basi utapoteza future ya watoto wako.

Wajinga ndio wali wao.
 
Licha ya hivyo mkuu..
Kuna walimu wengi mtaani ambao wana vyeti, diploma na shahada lakini kazi wanazofanya hata haziendani na elimu yao na wakati mashuleni hakuna walimu si sayansi wala hati.

Yaani kazi iliyobakia ni kurudia tu chaguzi. Na kutumia vibaya kodi za wananchi.
 
Daah umeongea kwa hisia kali sana mkuu....

Cha kuelewa hakuna kitu Cha bure, kila kitu kina gharama zake. Binafsi nimesoma shule za serikali kipindi hicho ada ilikuwa elfu 20 O level na 70 A level bado ilikuwa inatumika pesa nyingi kwenye mambo mengine kama tuition, vitabu, madawati na uniform.

Ukihamini elimu bure basi utapoteza future ya watoto wako.

Wajinga ndio wali wao.
Kabisa mkuu...hakuna kiongozi hata hawa wanaojiita wazalendo ambao watoto wao wanasoma shule za elimu bure.
 
Post muwafaka, kuna wale vijana waliokua wako vyuoni kusomea ualimu, mara wakaachishwa masomo kwa sababu sikuzielewa. Vipi hatma yao, ikiwa shule zinafungwa kwa kukosa walimu. Nilifikiri, ulikua uamuzi wa haraka. Warudishwe vijana shule wamalizie. Tunasikia sifa kaongeza wanafunzi milioni mbili. Lakini wakati huo huo kafukuza walimu waandaliwa 700. Matarajio yalikua nini?
Tuko busy kununua wapinzani ...

tupo kwenye right track ..so endeleeni kusubiri
 
Yote sawa ila kumbukeni .... KITU CHA BURE NI BURE KWELI KWELI
Hapo umenena mkuu...
Lakini mbona nchi kama Libya kipindi cha Gaddafi elimu ilikuwa bure na bora pia?

Issue sio elimu bure issue kubwa nivelimu bora...kama hakuna hela za kutosha watuambie sisi tuchangie ili walimu waajiliwe.

Ukiangalia kila mwaka walimu wa kutosha wanahitimu,
Serikali inaajiri kulenga lenga.

Bora wafute tuuu maana haina maana yyte ile kusoma bila kulipa 20,000 halafu walimu hawatoshi.

Huwezi amini kuna shule nilienda kufanya research zangu kulikuwa na mwalimu mmoja tu wa maths just imagine!
 
Huu ni mpango mzima wa wakoloni weusi kuzalisha wajinga wengi ili waendelee kutawala. Serikali ni kiini macho tu; hili ni kundi SIRI la watu wachache.
 
Hapo umenena mkuu...
Lakini mbona nchi kama Libya kipindi cha Gaddafi elimu ilikuwa bure na bora pia?

Issue sio elimu bure issue kubwa nivelimu bora...kama hakuna hela za kutosha watuambie sisi tuchangie ili walimu waajiliwe.

Ukiangalia kila mwaka walimu wa kutosha wanahitimu,
Serikali inaajiri kulenga lenga.

Bora wafute tuuu maana haina maana yyte ile kusoma bila kulipa 20,000 halafu walimu hawatoshi.

Huwezi amini kuna shule nilienda kufanya research zangu kulikuwa na mwalimu mmoja tu wa maths just imagine!

Mkuu Nebuchadinezzer, hongera kwa findings ya tafiti yako. Sasa ni marufuku bila kibali maalum. Sidhani kama anatambua kua anauwa ubunifu higher education. inakua ngumu wanafunzi kufanya utafiti. bila research inabikia kubahatisha. na ni dhidi ya katiba freedom of information. Kutojali katiba ndio mfumo wa utawala huu.
 
Kwa kweli tangu ianze hii kauli "mbiu ya elimu bure" binafsi sijaona manufaa yoyote katika hili maana hali imekua mbaya sana hasa hasa vijijini.

Tangu hii sera ianze kutekelezwa nchini kumekua na changamoto nyingi sana hasa hasa kwenye suala zima la miundombinu thabiti itakayomwezesha mwanafunzi kupata elimu bora na si bora elimu.

Tangu kuanzishwa kwa sera hii...kumekuwa na changamoto ya vyumba vya madarasa, maabara na hata maktaba. Huwezi amini kuna baadhi ya shule vyoo ni vichache sana kulinganisha na idadi ya wanafunzi.

Licha ya changamoto ya miundombinu, eneo jingine ambalo linachangamoto ni upate wa rasilimali watu. Shule nyingi hasa hasa za vijijini hakuna walimu wakutosha..hii ni kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.

Huwezi amini kuna shule hazina walimu kabisa...halafu cha kushangaza walimu wengi waliohitimu vyuo vikuu wako mitaani wanauza vocha na soda! Huu ni upuuzi wa hali ya standard gauge!

Katika hili serikali ijitafakari kwa kweli yaani haiwezekani serikali ishindwe kujenga madarasa, wananchi wajitolee kujenga halafu walimu hakuna...

Hii issue ya Songea imeniumiza sana....yani serikali ishindwe kujenga miundombinu wananchi wajenge....halafu shule ifungwe kisa hakuna walimu kweli?

Halafu mtindo wa kutuchukulia walimu wetu wa vyuo nakuwafanya viongozi wa siasa huo ni umama. Sasa serikali inategemea watafiti watatoka wapi?

Mwisho, serikali inatakiwa ifute elimu bure kama haina uwezo wa kuajiri na kuhudimia wananchi ipaswavyo.

Serikali iache kuhamisha walimu wa sekondari kwenda kufundisha shule za msingi wakati kuna walimu wengi wa shule ya msingi mtaani na pia kuna shule nyingi hazina walimu hata hao wa arts.

Halafu naomba ipitishwe sheria au utaratibu wa watoto wote wa viongozi kuanzia mtaa hadi raisi wasomee shule za umma...hivyo ndivyo serikali ya wanyonge inapaswa kua.

WENU KATIKA UJENZI WA NCHI
Nebuchadinezzer.

ASANTENI

ASANTENI
SERA ZILIZOPO SASA NI KUPAMBANA NA WALIMU KAMA GAIDI!!!
 
Elimu bure haipo kwa ajili ya kumkomboa mwananchi, ipo kwa ajili ya kuongeza mtaji wa kisiasa.....tafakari, chukua hatua.
 
Back
Top Bottom