Tangazo muhimu kwa wakazi wa DSM

Tangazo muhimu kwa wakazi wa DSM

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,667
Reaction score
167,605
1000735_10201322596454285_1918003751_n.jpg

TANGAZO KWA UMMA SOMA WEWE MWANA DAR ES SALAAM!!!!!!!!

MABADILIKO YA MAKUTANO YA BARABARA YA MOROGORO NA BIBI TITI KUANZIA TAREHE 01/08/2013
HAKUNA GARI LITAKALORUHUSIWA KUPINDA KULIA KWENYE MAKUTANO YA MOROGORO NA BIBITITI KUANZIA TAREHE 01/08/2013. SOMA MCHORO HAPO CHINI NA ULIZA MASWALI AU FIKA OFISI ZA DART UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA AU TANROADS AIRTEL BUILDING MOROCCO GHOROFA YA NNE KITENGO CHA BRT
 
Mkuu asante kwa taarifa!! Ngoja niwachapishie wenye magari yao; wasijekuanza ubishi na matrafiki bureee!!!
 
ndo raha ya kuwa na mabosi kama hawa...taarifa twazipata mapemaaaaaaaaaaaaaa! asante sana mkuu!
 
badala yake nipite wapi ili nielekee Ubungo nikitokea kwa serena hotel?

Ali Hassan Mwinyi - Kinondoni Makaburini - Kawawa - Morogoro

au

Ali Hassan Mwinyi - New Bagamoyo Rd - Sam Nujoma

na nyinginezo nyingi
 
Hee, Morogoro road inafungwa!!

Mmmh ukisema hivyo utakuwa unakosea, si unajua Morogoro Rd ni ndefu sana...

Nadhani hawa watakuwa wanakifunga kipande kifupi tu, pengine ni hapo makutano ya Akiba hadi Fire.

Wangelikuwa wanafunga sehemu kubwa basi wangetoa na alternatives kwenye junctions nyinginezo.

Pia ukisoma vizuri hayo maelezo utaona bado kuna upande wa Morogoro Rd utakuwa unatumika, hususani kwa wale wanaotokea Ubungo kuja Bibi Titi na kuelekea uelekeo wa Posta Mpya.
 
asante kwa maelezo
 
Hii inaonekana itakuwa ya kudumu, ukitazama huo mchoro kutakuwa hakuna uwezekano kwa gari inayotoka Serena kwenda Ubungo kupinda hapo kwa sababu ya hizo barabara za mabus yaendayo kasi.
Mchezo huu unaweza pia kuwa kwa barabara itokayo Muhimbili, itakuwa hakuna kupinda kulia kwenda Ubungo.
 
Basi Morogoro Rd yote itafungwa kwa wanaoelekea Ubungo
 
Mkuu unaweza ukawa sawa, kama design ya michoro yao ni hivi Morogoro rd itafugwa kwa barabara zielekeazo Ubungo.
 
Mkuu asante kwa taarifa!! Ngoja niwachapishie wenye magari yao; wasijekuanza ubishi na matrafiki bureee!!!

Hii barabara sijaipenda sana kwavile
1. ni nyembamba kuliko ilivyokuwa zamani (upana wake ni mdogo kuliko Mandela rd na Nyerere rd) ambazo ni za mfumo wa barabara mbili,
2. sijaona sehemu maalum za kuvuka barabara kwa ajili ya waenda kwa miguu, ukiacha lile dude linalojengwa pale UBT, wameweka vitofali (kerb) mwanzo-mwisho, watu wengine wataruka hayo matofali je walemavu wanaotumia baiskeli za magurudumu matatu watavukia wapi?
3. Kwa magari Hakuna sehemu za kuchepuka kwenda kulia au kushoto ukiacha pale maeneo ya Mwembechai, mfano umetokea Ubungo ukishapita Shekilango hautaweza kuingia mitaa ya upande wa kulia hadi ufike Magomeni karibu na Usalama
kwa hivyo barabara hii inausumbufu sana kwa madereva na waenda kwa miguu, hususan walemavu wa aina nilotaja hapo juu.
 
Back
Top Bottom