TANGAZO LA UFADHILI MAFUNZO YA KILIMO NCHINI ISRAEL

TANGAZO LA UFADHILI MAFUNZO YA KILIMO NCHINI ISRAEL

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,728
Reaction score
4,181
Hello jf jitahidini kuwapa ndugu zenu au mtu yeyote. Hii fursa ni nzuri sana...ni kama ajira ya moja kwa moja. Israel wako vizuri sana katika kilimo. Nitafurahi kama kati yetu humu jamvini atapata nafasi hii, mwanae au mtu mwingine yeyote wa karibu
Akaja cku moja kuleta feedback
TAARIFA KWA UMMA

TANGAZO LA MAFUNZO YA KILIMO NCHINI ISRAEL

UTANGULIZI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatangaza ufadhili wa mafunzo katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini Israel. Mafunzo hayo ni ya miezi 11 kuanzia mwezi Septemba, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Israel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mafunzo hayo yatahusisha pia vitendo (field attachment) kwenye mashamba makubwa ya mazao mbali mbali yakiwemo ya matunda, mbogamboga, ufugaji, uvuvi na mazao mengine ya biashara kwa ujira maalum.

SIFA NA VIGEZO VYA MWOMBAJI

Awe ni raia wa Tanzania mwenye umri wa kati ya miaka 20-35 pamoja na cheti cha kuzaliwa na Kitambulisho cha Uraia.
Awe amehitimu mafunzo ya Kilimo katika ngazi ya shahada ya Chuo Kikuu,Stashahada au Astashahada ya Vyuo vya kilimo vinavyotambulika nchini.
Awe na afya njema.
Awe na ujuzi wa kuandika na kuongea lugha ya Kiingereza.
Awe na uwezo wa kufanya kazi na watu wa tamaduni mbalimbali.
Awe tayari kurejea nchini baada ya mafunzo yake.

UTARATIBU WA KUFANYA MAOMBI

Maombi yote yatumwe kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yakiwa yameambatishwa na nakala za nyaraka zifuatazo:


i. Cheti cha kuzaliwa na uraia.

ii. Vyeti vya kitaaluma.

iii. Hati ya Kusafiria au uthibitisho wa maombi ya pasipoti.

iv. Cheti cha kuthibitisha afya kutoka hospitali inayotambulika.

v. Barua ya kuonesha sababu za kushiriki mafunzo hayo (Motivation letter) kwa lugha ya Kiingereza.

vi. Wasifu (Curriculum Vitae).

vii. Picha mbili ndogo (Passport size).

viii. Majina na anwani za wadhamini watatu wanaoishi nchini akiwemo mwalimu wa Chuo ulichohitimu.

Maombi yote yatumwe kupitia anwani ifuatayo: -

Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Jengo la LAPF
Ghorofa ya 6,
Barabara ya Makole,
S.L.P 2933,
DODOMA.

Au kwa baruapepe; mafunzo.israel@nje.go.tz

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12 Aprili, 2019

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
 
Mhitimu wa mafunzo ya kilimo ndio kozi gani?, Vyuo vya kilimo kwa,sasa vinatoa kozi mtambuka kwenye sekta kadhaa!

Wanaenda kujifunza nini! Mi mtu wa food science toka SUA kinaweza kisinihusu!
 
Mhitimu wa mafunzo ya kilimo ndio kozi gani?, Vyuo vya kilimo kwa,sasa vinatoa kozi mtambuka kwenye sekta kadhaa!
Wanaenda kujifunza nini! Mi mtu wa food science toka SUA kinaweza kisinihusu!
Jiongeze
 
Fikiri ndani ya box kabla ya kujaribu vinginevyo, miaka 30 ni mtaalam mbobezi kwenye fani unapanga safari bila kujua anaenda kusoma nn kwa mwaka mzima.

Hata kama wana tija kwenye kilimo sisi
tunahitaji kujua vijana wanaenda kujifunza nn huko na tutayatekeleza vp wakurudi.
 
Fikiri ndani ya box kabla ya kujaribu vinginevyo, miaka 30 ni mtaalam mbobezi kwenye fani unapanga safari bila kujua anaenda kusoma nn kwa mwaka mzima.
Hata kama wana tija kwenye kilimo sisi
tunahitaji kujua vijana wanaenda kujifunza nn huko na tutayatekeleza vp wakurudi.
ndio maana nikajibu ajiongeze.
Sio kila kitu utafuniwe waweza kuingia kwenye website zao kwa information zaidi
 
Back
Top Bottom