Tangazo la Royco cubes linakera

Tangazo la Royco cubes linakera

Mzalendowetu

Member
Joined
May 22, 2012
Posts
87
Reaction score
36
Nimekuwa nikisikia kupitia redio, tangazo linalohusu royco cubes. Tangazo hili linafananisha royco cubes na nyama, kwamba ukitumia royco cubes kuweka kwenye mboga za majani, ladha ya mboga hizo inabadilika na kuwa ni kama ya nyama.

Kwa mtazamo wangu, ladha ya mboga ya majani inabaki palepale na endapo ukitumia royco ladha ya mboga ya majani kubadilika kuwa kama ya nyama, basi royco haifai.

Lakini pia, kitendo cha kufananisha ladha ya nyama na royco ni kuitangaza zaidi nyama, ambayo sijui ni nyama gani, kuliko kuitangaza royco.

Ni maoni yangu tu hayo!
 
Me mwenyewe Huwa nashangaa, kama uko na hamu ya nyama c ununue hata robo, uondoe ki-hamu....
 
Ni ushamba wa waliondaa tangazo kwa kudhani,matembele yakiwa na radha ya nyama ndio mpango.

Kumbe hawajui hili tangazo kwa wanaojitambua ni upuuzi.
 
pia hawa jamaa wa Salama,sijui walifikiri nini bidhaa zao kuweka harufu za vyakula
 
ha ha ha ha wanataka kubadili maji kuwa maziwa ha ha ha a
 
Ni vizuri kama bidhaa hiyo itatumiwa ktk mboga za majani ambazo huweza kupikwa kwa kuchanganya na nyama, mf; mchicha, lakini matembele hapana kwa kweli, pia binafsi sipendi haya madude hata kidogo
 
kwa tusiokula nyama basi hata kuiskia hatutaki
 
Back
Top Bottom