Tangazo la mamlaka ya maji mwanza (mwauwsa)

Tangazo la mamlaka ya maji mwanza (mwauwsa)

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Jana nimepata clip yenye tangazo kutoka Mamlaka ya Maji Mwanza(MWAUWSA) ikiwatangazia wadau wa maji kuwa tarehe 28.3.2019 siku ya alhamisi saa nne Ukumbi wa Nyanza kutakuwa na mkutano ili wadau waweze kutoa maoni yao kuhusiana na mabadiliko ya ankara za maji katika Jiji la Mwanza.

Binafsi naona kama wanataka wadau wachache ndo wapate tangazo hili ili baadaye waweze kupandisha ankara za maji kwa hoja kuwa mbona wadau walihudhuria kwenye mkutano.

Nawashauri kama ifuatavyo:-

(1) Tangazo lao lipitie kwenye luninga ya Star times, Star TV na ITV na tangazo lirudiwe mpaka siku ya Jumatano jioni.

(2) Magari ya matangazo yapite kila kona ya Jiji la Mwanza na kusisitiza kuwa wadau wahudhurie mkutano huo siku ya Alhamisi vinginevyo siyo busara wachache kufahamu juu ya mkutano huu
 
Back
Top Bottom