Tangazo la kazi lililotangazwa na Clouds FM

Tangazo la kazi lililotangazwa na Clouds FM

big result now

Senior Member
Joined
Sep 8, 2013
Posts
107
Reaction score
70
Kuna tangazo la kazi linatangazwa clouds fm,wanasema makampuni yaliyowekeza kwenye gesi yanatangaza nafasi za kazi kwa watanzania,

sharti ni lazma uchukue form na kusoma course zao,kuchukua form ni shilingi elfu ishirini kwa mtu mmoja na kozi ni miezi mitatu ada yake ni sh 500,000,madai yao ni kwamba baada ya kumaliza kozi unaajiriwa moja kwa moja,moja ya namba ya kuongea na muhusika ni 0766308426.

Hawajasema majina ya makampuni hayo ila niliyempigia simu alinijibu wana nafasi 500,hawajataja website ya makampuni hayo na namba za simu si za kiofisi bali ni mtu binafsi,nakili kwamba wanatoa maelekezo ofisi zao zilipo,

wana jamii forum kama yupo azijuaye nafasi hizi kwa undani atoe taarifa kamili or kwa mliopo dar mnaweza kuwatafuta hawa jamaa kwa taarifa zaidi,siwaamini afu kama nawaamini kidogo,tujuzane wana jamii forum sababu ninahisi kama clouds wanatumiwa either kwa kujijua or kutojijua kuwalaghai vijana wanaotafuta ajira.
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Wezi hao. Msiwe kama TOMASO mpaka aguse ndio aamini.
 
,,hata mimi nilijaribu kuwapigia lakini hawaeleweki,,,,,

kwa hili hata clouds wanahusika kutapeli vijana,,,ETI WANASEMA WEBSITE INAHITILAFU,,,,,,WAONGO TU,,,,,
 
Inaonyesha kama hawa jamaa wana chuo kinafundisha course za mambo hayo na wanatumia loope hole hiyo kutangaza kwamba wana nafasi za kazi ili wapate wanafunzi kirahisi. Ila nilivyosikia lile tangazo linaonyesha hawana connection na wenye makampuni hayo ni makanjanja tu hao. Nijuavyo mimi kama makampuni yangehusika lazima kungekuwa na ufadhili (sponsorship), clouds itakuwa wameletewa tangazo na wamelipwa chao wanatangaza bt i don't think kama wanaijua vizuri hii issue.
 
Please clouds kama hilo tangazo limelipiwa mwezi mli simamishe xoz hao jamaa ni makanjanja tu tena wahuni kabisa
 
Clouds FM ni matapeli wanashirikiana na matapeli wengine kuwaibia wa-tz

Cc: TCRA
 
Last edited by a moderator:
Hiv wanajamvi chombo cha habari kinaweza kutangaza kitu bila kukihakiki? hawa clouds wanajidai wamjini sana hawana lolote wez tu hao wanashrkiana na wez kuwaibia vijana wa tz walosomesha na kodi za walipa kodi wavuja jasho.Kwan hapo clouds hakuna watu wenye taaluma za uandish wa habari au ndo hao watoto wa mjomba/shangazi.
 
Paza sauti,,pinga udhalimu wa clouds fm,,,,wanaelewa kabisa kwamba mtu aliyepeleka tangazo haeleweki,,wanakubalije kuliweka hewani???

Au la,,,hili dili wanalipiga clouds fm wenyewe,,,wanatumia mwanya kula hela za watu bure,,,
 
Kiukweli tangazo nimelisikia ila wale jamaa wanataka kufanya biashara kwenye hicho chuo chao baada ya kuona watu wengi kwa sasa wanafocus kwenye oil,na gas so ni njia ambayo wanatumia kama vile vyuo vyetu kama sinon college wanaotangaza ajira uhakika wakati wizi mtupu
 
Nasikia harufu ya kutapeliwa hapo. Kwa uzoefu wangu wa oil and gas industry, hizi kamapuni huwa zina training school zao, na recruitment zao ni either fresh graduate ambao then wanakuwa trained kutokana na assigned segment au watu wenye experience; zaidi ya hapo naona watu wanataka kutumia fursa kiukanjanja.
 
Inawezekana Ruge kahamia na kwenye fursa za vyuo, maana asione kichaka.
 
wana nafasi ya watu 500 na ukimaliza unapewa ajira? kwenye nchi hii yenye wanafunzi zaidi ya 20,000 ambao degree zao/diploma zimekuwa kipolo?
 
mna uhakika huu ni utapeli?

angalieni msije kuwa mnazichezea fursa kwa uoga wenu.
 
hawa naona gia yao ipo kama ya shirika linalijiita shirika la madini tanzania,nao walikuwa na tangazo kama hilohio lakin mwisho wa siku hakuna cha ajira wala nini,ni wizi mtupu
 
Jamaa wapo kazin na fursa zao,
redio hii bhana,ni afadhal zile community redioz za huko mikoan na vijijin,
 
Back
Top Bottom