Tangazo la "Haki sawa" nini hasa linadai?

Ilumine

Senior Member
Dec 27, 2008
196
4
Tangazo linalorushwa katika runinga, hasa TBC1 silipendi kabisa. Hivi hii dhana ya wanawake kujiona kama wananyimwa haki inatoka wapi? Nionavyo mimi, kuna baadhi ya wanawake ambao wanashindwa kujitambua kama wao ni wanawake, au wanadhani kwa kuwa wao ni wanawake basi kuna kitu fulani Mungu aliwapunja, sijui ni kitu gani, wanakijua wao wenyewe.
Yawezekana zikawa ni propaganda za mataifa fulani yanayotuletea 'sera' zao, ambazo kwa kweli si za kiafrika.
Sasa tangazo lile linachodai ni kuongezewa kwa nafasi za upendeleo kwa akinamama katika bunge? au linadai kitu kingine. Kama ndio 'haki sawa' basi wanawake wahimizwe 'kuchangamka' na kugombea nyadhifa mbalimbali ili iwe 50 kwa 50, na isiwe tena wengine wanaingia bungeni kwa kubebwa tu. Kama tunaendelea kudaidai namna hii nani basi anayebana hizo haki? Niambieni, kama kuna mtu anawanyima haki leo hii wanawake basi tangazo liseme waziwazi, na wao wadai haki hizo wanazonyimwa.
Kupigapiga kelele za haki sawa, haki sawa, haitoshi. Shughulikieni yule mnayemwona anawadhulumu. Kuai wanawake wapendelewe zaidi katika nafasi fulani fulani ni kinyume na msemo wenyewe wa "haki sawa".
Labda kuna watu wamepewa waviendeshe 'vitengo' ambavyo havieleweki, na wao kwa sababu wanakula mishahara kwa ajili ya hilo, inawapasa wapige kelele hata kwa mabo ambayo ni 'illogical'.
Nawasilisha hoja!
 
Mwanamke kuwa mbunge na kuingia bungeni binafsi mimi sioni mahusiano yake na msaada wa akina mama wanaoteseka vijijini kwa kukosa maji, umeme, pembejeo za kisasa nk. Lazima kuna ajenda ya siri hapa iliyofichika nyuma ya pazia!!
 
Mwanamke kuwa mbunge na kuingia bungeni binafsi mimi sioni mahusiano yake na msaada wa akina mama wanaoteseka vijijini kwa kukosa maji, umeme, pembejeo za kisasa nk. Lazima kuna ajenda ya siri hapa iliyofichika nyuma ya pazia!!

Ni kweli, gharama zinazotumika katika mambo yasiyo na manufaa, ni bora zikatumiwa katika mambo hayo ya msingi ya kuwanufaisha wanawake baadala ya kuwaridhisha 'kisaikolojia' katika mambo yasiyowanufaisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom